Yanga yakataa kuvaa nembo nyekundu, ni kinyume na Katiba yao

Mi naomba kueleweshwa; hivi jezi ni nyekundu au nembo ndo nyekundu?
Naomba kuwaelewesha Yanga kwamba nembo ya mdhamini siyo sehemu ya jezi.
Timu inapotambulisha jezi zake kinachioneshwa ni rangi za timu na nembo ya timu hivyo kinachobandikwa baada ya hapo ni matangazo tu na siyo sehemu ya jezi.
 
Tunahitaji ushahidi gani kujua kama uongozi mzima wa Yanga hawatumii akili
 
Bora tukacheze ndondo lakini sio kuvaa nyekundu sawa na muislam bora ufe njaa kuliko kula kitimoto
Umeenda upande siyo, umeharib! Uislam ni elim, si ushabiki. Uislam hautaki mtu afe njaa ilhali kitimoto/nyau n.k wapo mbele'ake.
 
Uongo.Jezi ni sehemu yote ya nguo ikiwepo nembo na maandishi mengineyo.suala la nembo na rangi zake FIFA zimetoa option ya kukaa na vilabu na kujadili kama suala linatatulika lakin sio ubabe wa TFF.
 
Mimi bana niwe tofauti na wengine,
Kwanza naupenda upinzani huu wa kwetu hapa. Timu iko na hali mbaya lakini haiko radhi kuvaa nembo za watani zao, potelea mbali wakose udhamini.

Ilishatokea hii kabla na hawa hawa Vodacom wakawabunia nembo yenye rangi zao, wafanye tu na sasa. Nawaza pia ingekua ndio timu yangu Simba imelazimishwa kuvaa nembo ya mdhamini yenye kijani na njano hata mie nisingefurahi pia.

Kama ushabiki na ushindani wetu hapa Tanzania unahusisha mpaka rangi za jezi basi hili liheshimiwe tu. Mdhamini anatakiwa afahamu hili. Hivi hawadhani kua Yanga kucheza huku wamevaa jezi zenye nembo inayofanana na mtani wake inaweza kuwaathiri kisaikolojia?

Busara itumike kwenye hili kama ilivyowahi kutmika siku za nyuma.

 
Wewe Mikia FC tulia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…