Daniel Mbega
JF-Expert Member
- Mar 20, 2013
- 338
- 180
YANGA imekula ‘kiporo’ kwa tonge moja tu, tena bila mboga. Imeichapa Mtibwa Sugar bao 1-0 katika mechi yake hiyo ya kiporo cha Ligi Kuu na kufanikiwa kufikisha pointi 59 ikiwa na michezo 24 sawa na mahasimu wao Simba na matajiri wa Bongo, Azam FC.
Simba, ambayo inaikaribisha Toto African kesho Jumapili kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, ina pointi 57 wakati Azam inashika nafasi ya tatu ikiwa na pointi 55 na haichezi mpaka Aprili 27.
Kwa habari zaidi, soma hapa => Yanga pointi 59 saafi, yawapigia hesabu Waarabu | Fikra Pevu