Yanga yamalizana na Malimi Busungu, asaini usiku wa jana

Yanga yamalizana na Malimi Busungu, asaini usiku wa jana

Wonderful

JF-Expert Member
Joined
Apr 8, 2015
Posts
7,347
Reaction score
5,986
Malimi Busungu akisaini miaka miwili kukipiga Jangwani.

====================
====================

Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM

YANGA SC imeipa pigo lingine Simba SC, baada ya kufanikiwa kuinasa saini ya mshambuliaji Malimi Busungu (pichani) wa Mgambo JKT ya Tanga.

Katibu wa Yanga SC, Dk Jonas Tiboroha ameiambia BIN ZUBEIRY jioni hii kwamba wamemalizana na Busungu.

Dk Tiboroha amesema Busungu amesaini Mkataba wa miaka miwili leo kuhamia kikazi Yanga SC- maana yake Simba SC waliokuwa wanamuwania pia ‘imekula kwao'.

"Huyu kati ya wachezaji ambao walipendekezwa na benchi la Ufundi. Tumefanikiwa kumalizana naye leo hii," amesema Tiboroha.

BIN ZUBEIRY inafahamu Simba SC ilifanya mazungumzo na mshambuliaji huyo, lakini wakashindwana dau.
[TABLE="class: tr-caption-container"]
[TR]
[TD="align: center"]
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="align: center"]Malimi Busungu sasa anapatikana Jangwani, Dar es Salaam na atakuwa anavalia jezi za rangi ya kijani na njano

[/TD]
[/TR]
[/TABLE]

Busungu amekuwa mchezaji tegemeo wa Mgambo JKT kwa misimu mitatu na wiki hii aliitwa katika kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars.

Busungu anakuwa mchezaji wa nne kusajiliwa Yanga SC ndani ya wiki moja na ushei, baada ya awali timu hiyo kuwasajili winga kipa Benedictor Tinocco wa Kagera Sugar, beki Mwinyi Hajji Mngwali wa KMKM na mshambuliaji Deusi Kaseke kutoka Mbeya City.

Chanzo: BinZubeiry Blog
 
Attachments

  • busungu+saini.jpg
    busungu+saini.jpg
    6.9 KB · Views: 1,138
Upumbavuuuu mtupu amna mtu umo ila kwa sbb alikuwa anatakiwa na simba ndio wanambolokewa
 
Safi yanga mukamnunue na yule mfungaji bora mara mbili wa zenji .anaitwa janja ni.bonge la kifaaaaaa
 
Upumbavuuuu mtupu amna mtu umo ila kwa sbb alikuwa anatakiwa na simba ndio wanambolokewa

Simba wamekuwa wakiwatwist sana Yanga kwenye usajili. Waongea tu kuwa wanataka kumsajili mtu fulani Yanga wanaenda mbio sijui hawajui scouting angalau ya kibongo bongo. Malimi ni wa kawaida sana, sijui namna gan atatumika hapo
 
Pale mbele yupo tambwe yupo Sherman yupo msuva wamemuongeza kaseke bdo kuna dogo walmsajili kabla ligi aijaisha wanaaribu hela zao na kuua vipaji vya madogo uyo busungu chizi kama javu alishindwa kuonekana atakuwa yeye amuulize tegete
 
Tetesi za yanga kumtaka busungu zilianza tangu wakati ligi inaendelea,kushindwa kwenu kugombania mchezaji na yanga ndo kunakufanya utoe vijisababu kama hivyo vya akina sungura
 
Mbona nyinyi mmeua kipaji cha serukuma hatusemi, timu yoyote lazima iwe na wachezaji wa kikosi cha kwanza na cha 2 kutokana na juhudi za mchezaji
 
Tetesi za yanga kumtaka busungu zilianza tangu wakati ligi inaendelea,kushindwa kwenu kugombania mchezaji na yanga ndo kunakufanya utoe vijisababu kama hivyo vya akina sungura

Mkuu hawa mambumbumbu achana nao. Yanga ilimtaka Busungu hata kabla Simba hawajaamka. Hata Kaseke na mwenzake aliyesaini simba walikuwa na mawasiliano na Yanga kabla Simba hawajaingilia kati. Hii ni kwa mujibu wa wachezaji wenyewe.
 
Pale mbele yupo tambwe yupo Sherman yupo msuva wamemuongeza kaseke bdo kuna dogo walmsajili kabla ligi aijaisha wanaaribu hela zao na kuua vipaji vya madogo uyo busungu chizi kama javu alishindwa kuonekana atakuwa yeye amuulize tegete

Msimu uliopita washambuliaji wa Yanga walikuwa ni Sherman,Tambwe,Tegete,Javu na Mrwanda. Msimu huu Mrwanda,Tegete na Javu wanaachwa so lazima replacement
 
ni malimi wa changarawe morogoro? amna kitu apo bora wangemchukua ata midonge
 
Huyo Dogo anajua ila nyie simba mmezoea wachezaji wa mia mbili
 
Back
Top Bottom