Yanga yamsainisha Dickon Ambundo

Yanga yamsainisha Dickon Ambundo

Riz king

JF-Expert Member
Joined
Dec 30, 2018
Posts
276
Reaction score
549
Hizi sajili ninahofu nazo sana naona tunaenda kutolewa kwa aibu champions league na pia kuizawadia Simba kikombe cha 5 mfululizo.

===
Ambundo amewashusha presha mashabiki kwa kuwaambia kuwa kila kitu kitakuwa sawa kwa msimu ujao wa 2021/22.

Nyota huyo ambaye ni ingizo jipya kutoka Dodoma Jiji, jana Agosti 11 alitambulishwa rasmi kwa kusaini dili la miaka miwili.

Alikuwa katika kikosi cha kwanza ambacho kilishiriki Kagame Cup Challenge 2021 na kuishia hatua ya makundi.

Katika mechi tatu ambazo alicheza alitoa pasi moja ya bao lilifungwa na mshikaji wake Wazir Junior.

Ambundo:"Bado Yanga wanapaswa watulie kuna mambo mengi mazuri yanakuja. Kushindwa kutwaa taji la Kagame sio mwisho wa mapambano,".

1628746843794.png
 
Hizi sajili ninahofu nazo sana naona tunaenda kutolewa kwa aibu champions league na pia kuizawadia Simba kikombe cha 5 mfululizo
Wewe umecheza mpira?
Wewe unacheza mpira?
Wewe utacheza mpira?
Ulitaka wamsainishe Nani mchezaji wa ndani ambaye wewe unheridhika kuliko Ambundo?
 
Japo Simba tutaenda tena kuchukua ubingwa wa 5 mfululizo, ila Ambundo ni bonge moja la mchezaji

Toka alipokuwa Gor Mahia alikuwa akionekana ni mwenye kipaji
 
Ambundo ni mchezaji mzuri sana na amethibitisha hivyo kwenye ligi iliyoisha. Lakini nimemtizama kwenye Kagame Cup akiwa na Yanga mara nyingi alikuwa anataka acheze na jukwaa kitu ambacho kitamuharibia. Yeye acheze mpira wake uliomfanya akasajiliwa Yanga basi na aongeze bidii kwenye mazoezi na kujiamini. Asipokuwa mwangalifu kwenye hizi timu kubwa ukikosea kidogo tu huwa wanaanza kumzomea mchezaji baadae wanaanza kumzomea kocha akikupanga kinachofuata ni benchi kwa mchezaji na mwisho ni kutemwa mwishoni mwa msimu. Kwa hiyo Ambundo apunguze kucheza na jukwaa atafanikiwa kwani uwezo anao mkubwa tu.
 
Back
Top Bottom