Yanga yamsajiri kipa wa Serengeti Boys Ramadhani Kabwili 'aka' Kaseja!

Yanga yamsajiri kipa wa Serengeti Boys Ramadhani Kabwili 'aka' Kaseja!

Wonderful

JF-Expert Member
Joined
Apr 8, 2015
Posts
7,347
Reaction score
5,986
C__Data_Users_DefApps_AppData_INTERNETEXPLORER_Temp_Saved Images_RAMADHANI KABWILI.jpg

YANGA SC imekamilisha idadi ya makipa watatu baada ya kumsaini na kipa wa timu ya vijana chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys, Ramadhani Awam Kabwili.
Mlinda mlango huyo atakayetimiza umri wa miaka 17 Desemba 11, mwaka huu alidaka mechi zote za Serengeti Boys kwenye Fainali za Vijana Afrika chini ya umri wa miaka 17 nchini Gabon na kusifiwa mno kwa kiwango kizuri alichoonyesha.
Meneja wa Yanga, Hafidh Saleh ameiambia Bin Zubeiry Sports – Online leo kwamba wamesajili Kabwili baada ya kuachana na makipa wao wawili wa muda mrefu, Ally Mustafa ‘Barthez’ na Deo Munishi ‘Dida’ waliomaliza mikataba yao.


Ramadhani Awam Kabwili amesajiliwa Yanga SC baada ya kufanya vizuri na Serengeti Boys

Hafidh amesema Kabwili anaungana na kipa mwingine mpya, Mcameroon Youthe Rostand aliyesajiliwa kutoka African Lyon na Benno Kakolanya ambaye anakwenda kwenye msimu wa pili tangu asajiliwe kutoka Prisons ya Mbeya.
Yanga SC, mabingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara wameanza mazoezi leo Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam kujiandaa na msimu mpya, ingawa hawakuwa na kipa ata mmoja baada ya
Rostand na Kakolanya kutotokea, wakati Kabwili yuko na timu ya taifa ya wakubwa, Taifa Stars mjini Mwanza.
Kabwili ameitwa kwa mara ya kwanza Taifa Stars, ambayo Jumamosi itamenyana na Rwanda ‘Amavubi’ katika mchezo wa kwanza wa kuwania tiketi ya kucheza Fainali za ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN), michuano inayohusisha wachezaji wanaocheza ligi za nchini mwao pekee.
 
Tunakupa pole dogo , tarajia Yanga watakuachia ukifulia kama Ngasa, sahau ndoto za kucheza nje ya nchi
Ili acheze nje, ni lazima achezee Simba kwanza ehh?

Hivi hii ndio club strategy ya kuvutia wachezaji?[emoji23][emoji23]

Watu wanafuata MATAJI.
 
Kanaenda kuua kipaji hako katoto

Sent from my SM-N920C using JamiiForums mobile app
 
Kila la heri huku Bondeni FC. Lakini kaa ukijua kuwa zile ndoto zako za kucheza soka nje ya nchi ndo zimefifia. Ni king'anganizi hao jamaa
 
Ili acheze nje, ni lazima achezee Simba kwanza ehh?

Hivi hii ndio club strategy ya kuvutia wachezaji?[emoji23][emoji23]

Watu wanafuata MATAJI.
Haya mataji ya kupewa na Malinzi yalishawahi kukusaidia nini zaidi ya kuaibisha taifa

Sent from my Lenovo A2010-a using JamiiForums mobile app
 
Ili acheze nje, ni lazima achezee Simba kwanza ehh?

Hivi hii ndio club strategy ya kuvutia wachezaji?[emoji23][emoji23]

Watu wanafuata MATAJI.

Kwa mfano Ngasa ,Cannavaro hayo mataji ya kibongo yamewasaidia nini ?

Kwako wewe mataji na makombe ni bora kuliko huyo dogo kupata nafasi ya kudaka as kipa wa kwanza
 
Wacha wivu wewe

Sio wivu ni mtoto mdogo tunampa ushauri bora hata asajiliwe Jkt Ruvu, au timu nyingine yeyote ambayo atakuwa golikipa namba moja itamsaidia kupata uzoefu zaidi, chukulia mfano Manyika junior alikuwa kipa mzuri sana lakini naona kipaji kimeshapotea maana simba walimiweka kipa namba 3 yaani msimu mzima hadaki.
 
Sio habari nzuri kwa maendeleo yasoka la nchi. Vijana hawa ilifaa wapelekwe nje kabisa bado wakiwa na umri wa kufundishika
 
Back
Top Bottom