Yanga yamtangaza Waziri Bashungwa kuwa mgeni rasmi huku Bodi ya Ligi ikimtangaza Waziri Mchengerwa

Ghazwat

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2015
Posts
23,718
Reaction score
66,267
Kuelekea kwenye mchezo wa April 30, 2022 kati ya Watani wa Jadi, Yanga SC na Simba SC mchezo wa Ligi Kuu Tanzania, ambao utapigwa kwenye Dimba la Benjamin Mkapa Jiji Dar es salaam, hatimaye Mawaziri wawili watangazwa kuwa wageni rasmi kwenye mchezo huo.

Klabu ya Yanga ambaye ndo mwenyeji wa mchezo huo baada ya kumtangaza mgeni rasmi, Mheshimiwa Innocent Bashungwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi.

Bodi ya Ligi nao wamemtangaza mgeni rasmi, Mheshimiwa Mohamed Mchengerwa Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo.

Kulipewa Mwana Kulitaka Mwana

Screenshot_20220429-191045~2.jpg
20220429_191227.jpg
 
Kuelekea kwenye mchezo wa April 30, 2022 kati ya Watani wa Jadi, Yanga SC na Simba SC mchezo wa Ligi Kuu Tanzania, ambao utapigwa kwenye Dimba la Benjamin Mkapa Jiji Dar es salaam, hatimaye Mawaziri wawili watangazwa kuwa wageni rasmi kwenye mchezo huo.

Klabu ya Yanga ambaye ndo mwenyeji wa mchezo baada ya kumtangaza mgeni rasmi, Mheshimiwa Innocent Bashungwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi.

Bodi ya Ligi nao wamemtangaza mgeni rasmi, Mheshimiwa Mohamed Mchengerwa Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo.

View attachment 2205122View attachment 2205123
Simba nao wamemtangaza Manara kama mgeni rasmi
 
Hizi habari za mgeni rasmi ifikie wakati vilabu vyetu na TFF na bodi ya ligi iachane nazo. Yaani imekaa kisiasa sana badala ya kimichezo
Niliona mgawanyiko baada ya Simba SC kumtangaza mgeni rasmi Mheshimiwa Kinana.

Kwakweli hili jambo kama litaachwa ni bora kuliko kuendelea kuwepo
 
Wanasiasa ni Public figure. Au kwa mtazamo wako unataka waalikwe akina nani?

Yaani sawa tu na nyinyi mnavyo mualika Job Ndugai, Tulia Ackson na Kassim Majaliwa kama wageni rasmi kwenye matukio yenu. Hivyo hakuna tatizo katika hili.
 
Sijui wanawazaga nini lakini hili huwa haliwatendei haki mashabiki hasa ukiangalia wageni rasmi wanaoletwa ni watu walio kwenye mlengo wa kisiasa tena wa chama cha aina moja. Ukiangalia hata anachokifanya uwanjani hakuna cha maana
 
Wanasiasa ni Public figure. Au kwa mtazamo wako unataka waalikwe akina nani?

Yaani sawa tu na nyinyi mnavyo mualika Job Ndugai, Tulia Ackson na Kassim Majaliwa kama wageni rasmi kwenye matukio yenu. Hivyo hakuna tatizo katika hili.
Umechukulia kama vile ni maoni yaliyowasilisha na mwanasimba ndio maana umejibu kishabiki hivyo.
 
Niliona mgawanyiko baada ya Simba SC kumtangaza mgeni rasmi Mheshimiwa Kinana.
Kwenye mchezo huu, kwani mwenyewe mamlaka ya kumtangaza mgeni rasmi ni nani?
Michuano ya CAF, klabu mwenyeji inakuwa na nguvu kuliko FA yake, so huwa inatangaza. Kwenye michuano yote ya ndani, FA ina mamlaka yote, so TFF inamtangaza, bna sio klabu. Hapo Yanga wamechemka
 
Hii timu ni utopolo kweli.
Wenye akili wawili tu nao wamezeeka hata hawawezi kuwa viongozi tena,wangeiokoa timu na huu utopolo
 
Back
Top Bottom