Yanga yamtema Chirwa, Kalengo achukua nafasi yake. (Dili Halikufanikiwa)

Yanga yamtema Chirwa, Kalengo achukua nafasi yake. (Dili Halikufanikiwa)

Wonderful

JF-Expert Member
Joined
Apr 8, 2015
Posts
7,347
Reaction score
5,986
kalengo.jpg

Yanga imefanikiwa kupitisha jina la mshambuliaji wa zamani wa Zesco, Winston Kalengo.

Kalengo ametua Yanga baada ya jina lake kuwasilishwa katika nusu saa ya mwisho kabla ya dirisha ya usajili.
Taarifa zinaeleza, Yanga imepitisha jina hilo la Kalengo anayechukua nafasi ya Mzambia, Obey Chirwa.

Yanga imemrudisha Chirwa FC Platnums kwa mkopo, safari hii akiwa analipwa nusu mshahara na Yanga na Wazimbabwe hao watamlipa nusu mshahara.

Mjadala mkubwa kuhusiana na hilo, ndiyo ulichelewesha Yanga kuwasilisha jina hilo katika hatua za mwisho na imeelezwa Yanga wameliwasilisha katika majina ya wachezaji wao saa 5:36, ikiwa ni dakika 24 kabla ya usajili huo wa dirisha dogo kufungwa.

Pamoja na kufanya vizuri Zambia akiwa na Zesco, Kalengo aliwahi kucheza soka la kulipwa nchini Congo Brazaville na anaelezwa kuwa mkali wa kupiga mashuti, mwenye njaa ya mabao.

UP DATES:
Uongozi wa FC Platinums ya Zimbabwe, umegeuza dili la mshambuliaji Winston Kalengo kutua Yanga baada ya kukataa kulipa mshahara wa Obey Chirwa.
Yanga ilikubaliana na FC Platinums kuwa itampeleka Chirwa kwa mkopo kwa kuwa ilimtoa hapo ili Wazimbabwe wawe wanamlipa mshahara na kama ikitokea dili, wanaweza kumuuza.

“Kweli mwisho ikawa safi na Yanga ikaanza mipango ya kumsajili Kalengo. Kila kitu kimeenda safi na jina limepelekwa lakini inaonekana poa. Lakini mwisho FC Platinums wamekataa kulipa mshahara, sasa inakuwa vigumu kulipa watu wawili.

“Maana Chirwa aende FC Platinums tumlipe, Kalengo naye awe Yanga tumlipe. Imekuwa vigumu na uongozi umetaka kulipa mchezaji mmoja tu, hii imechangia Chirwa kubaki,” kilieleza chanzo.

Yanga ilikuwa imekubaliana kila kitu na Kalengo pamoja na Zesco na lengo lilikuwa ni kuongeza nguvu katika ushambulizi, jambo ambalo linaonekana limekwama
 
Yaani milioni 200 kwa nusu msimu. Kweli wajinga ndio waliwao.
Di Maria £50 mil kwa msimu mmoja kisha kauzwa kwa hasara....
je Musa Ndusha amenunuliwa kiasi gani na amecheza mechi ngapi? Naomba jibu.....!!!!
 
Ndusha amenunuliwa milioni 20 na ametolewa kwa mkopo. Simba hawalipi mshahara wake.Chirwa Yanga wanalipa nusu mshahara pamoja na kumnunua milioni 200.De Maria aliuuzwa na hakucheza nusu msimu bali msimu mzima. Kuna tofauti kubwa sana ya milioni 20 na milioni 200.Kutetea ni kujaribu kutetea ujinga.
 
Yaani milioni 200 kwa nusu msimu. Kweli wajinga ndio waliwao.
Kwenye soka hilo ni jambo la kawaida, utashangaa ikiwa wewe si mfuatiliaji wa soka la wenzetu huko mbele.
Victor Moses wa Chelsea alinunuliwa na zaidi ya misimu minne alikuwa akicheza kwa mkopo katika timu tofauti tofauti za epl
Kwa sasa karudishwa, na sasa ni mchezaji tegemeo kwa chelsea ya Conte
 
Tuanzie kwa bei. Nitajie mchezaji wa huko unakosema wewe aliyenunuliwa ghali kwa bei za huko halafu baada ya nusu msimu akatolewa kwa mkopo. Kwa mifano ya huku milioni 200 ni ghali sana kwa wachezaji wetu .Cha kushangaza ni Chirwa kununuliwa kwa milioni 200 halafu atolewe kwa mkopo,tena timu iliyomnunua ilipe nusu mshahara wake.
 
Ndusha amenunuliwa milioni 20 na ametolewa kwa mkopo. Simba hawalipi mshahara wake.Chirwa Yanga wanalipa nusu mshahara pamoja na kumnunua milioni 200.De Maria aliuuzwa na hakucheza nusu msimu bali msimu mzima. Kuna tofauti kubwa sana ya milioni 20 na milioni 200.Kutetea ni kujaribu kutetea ujinga.
Hujajibu amecheza mechi ngapi?
Ndusha amepelekwa kwa mkopo timu gani Huyo Musa Ndusha?
Nimekuamnia Di Maria ameuzwa kwa hasara usiwe mvivu wa kusoma
 
UZUSHI : Taarifa zinazoenea kuwa klabu ya Yanga SC imemsajili Winston Kalengo na kumtoa kwa mkopo Obrey Chirwa sio za kweli, Yanga imefunga usajili wake wa dirisha dogo kwa usajili wa Emanuel Joseph Marthin na Joseph Zullu 'Mkata Umeme' huku ikiachana na Mbuyu Twite.

Kikosi kinaendelea na maandalizi ya mchezo wa ligi kuu Tanzania bara katika uwanja wa Uhuru jijini Dar.

KILA LA HERI YANGA AFRIKA.

Habari si za kweli zimekanushwa
 
Ni ujinga kusisitiza Ndusha kacheza mechi ngapi?Unajua wazi Ndusha alikuwa na matatizo ya kupata leseni yake ndio maana alicheza mechi moja. Anakwenda Oman kucheza kwa mkopo na hujamsikia akipinga au?Di Maria alitaka mwenyewe kuuzwa ndio akauuzwa kwa hasara. Hivyo Man United wakipata hasara inahalalisha Yanga wapate hasara ya kutomtumia mchezaji waliyemnunua millioni 200?
 
Tufunge mjadala Yanga wamekanusha hizo habari sio za kweli.
 
UZUSHI : Taarifa zinazoenea kuwa klabu ya Yanga SC imemsajili Winston Kalengo na kumtoa kwa mkopo Obrey Chirwa sio za kweli, Yanga imefunga usajili wake wa dirisha dogo kwa usajili wa Emanuel Joseph Marthin na Joseph Zullu 'Mkata Umeme' huku ikiachana na Mbuyu Twite.

Kikosi kinaendelea na maandalizi ya mchezo wa ligi kuu Tanzania bara katika uwanja wa Uhuru jijini Dar.

KILA LA HERI YANGA AFRIKA.

Habari si za kweli zimekanushwa
Afadhali zimekuwa ni uzushi .Ingekuwa ni kioja pamoja na juhudi zako za kujaribu kuutetea. Ushabiki unafanya mashabiki wengi kutotumia common sense na kuendelea kutetea ujinga.
 
Di Maria £50 mil kwa msimu mmoja kisha kauzwa kwa hasara....
je Musa Ndusha amenunuliwa kiasi gani na amecheza mechi ngapi? Naomba jibu.....!!!!
Hapo wasijibu kuhusu Sserunkuma, Kagwa na wengineo, mikia huwa inafikiria kutumia mikia na siyo vichwa.
 
Di Maria £50 mil kwa msimu mmoja kisha kauzwa kwa hasara....
je Musa Ndusha amenunuliwa kiasi gani na amecheza mechi ngapi? Naomba jibu.....!!!!
Ndusha ni pesa ya nyanya wala haina athari. Ila kwa pesa ya yanga kwa sababu tunajua chanzo chake ni ufisadi hatuna la kusikitisha manji amekua mtu was ufisadi toka anazalia
 
DIRISHA DOGO LA USAJILI LIMEFUNGWA SAA 6 USIKU WA KUAMKIA LEO.

HIKI NDIO KIKOSI CHA YANGA MSIMU HUU.

Makipa
-Ali Mustafa
- Deogratius Munishi
- Beno Kakolanya

Walinzi
- Nadir Haroub
- Vicent Andrew
- Vicent Bossou
- Pato Ngonyani
- Mwinyi Haji
- Juma Abdul
- Hassani Kessy
- Oscar Joseph
- Kelvin Yondani

Viungo
- Saidi Juma
- Saimoni Msuva
- Yusuph Mhilu
- Haruna Niyonzima
- Thabani Kamusoko
- Juma Mahadhi
- Deusi Kaseke
-Justin Zullu
- Geofrey Mwashuiya

Washambuliaji
- Donald Ngoma
- Obrey Chirwa
- Mateo Anthony
- Malimi Busungu
- Amisi Tambwe
- Emanuel Martin

° BENCHI LA UFUNDI.

Kocha Mkuu.
George Lwandamina

Msaidizi Maalum.
Noel Mwandila.

Kocha Msaidizi.
Juma Mwambusi.

Meneja.
Hafidh Saleh

Kocha wa Makipa.
Juma Pondamali.

Daktari wa timu.
Dr. Edward Bavu.

°Mkurugenzi wa ufundi.
Hans Van Pluijm
 
Back
Top Bottom