- Source #1
- View Source #1
Wakuu kuna hii barua inasambaa katika mitandao ya kijamii, uhalisia ukoje?
- Tunachokijua
- Kuanzia Machi 3, 2026 kumekuwa na barua/taarifa kwa Umma yenye utambulisho wa klabu ya Yanga ikieleza kuwa klabu hiyo imemtimua kocha wake Mkuu Pedro Goncalves na hivyo klabu hiyo itaongozwa na kocha msaidizi Patrick Mabedi kwa muda.
Uhalisia wa madai hayo?
Baada ya ufuatiliaji wa kina imebainika kuwa taarifa hiyo ya kutimuliwa kwa kocha mkuu wa Yanga si ya kweli.
Taarifa hiyo kwa umma hajitolewa na klabu ya Yanga kama inavyoelezwa, pia hakuna chanzo chochote cha kuaminika kilichotangaza habari za kufukuzwa kwa kocha Pedro.
Taarifa hiyo imehaririwa kutoka katika taarifa rasmi ya Oktoba 18, 2025 baada ya klabu hiyo kumtimua kocha wake wake mkuu wa kikosi cha kwanza, Romain Folz.
Ili kubainisha namna Taarifa hiyo ilivyohaririwa wameondoa Tarehe ambayo ilikuwa ni Otoba 18, 2025 pia jina la Pedro limeandikwa kwa fonts tofauti ukilinganisha na fonts nyingine zilizotumika.