Watani wameamua kutumia kanuni ya 'Heri shetanii unayemfahamu kuliko malaika usiyemfahamu'.
Wanadai kuwa haiwezekani Yanga wachukue ubingwa mara 3 mfululizo utafikiri wanacheza peke yao. Kwa kipindi kirefu Hanspope na wenzake wameshindwa kabisa kupata wachezaji ndani na nje ya nchi wenye uwezo wa kuipatia Simba kombe. Hebu angalia wachezaji kama akina Sserunkuma na wenzake hawakufua dafu. Wakamkumbuka Hamisi Kiiza aliyecheza kwa mafanikio akiwa Yanga naye hakufua dafu. Wakamleta Okwi akaishia kupata mabao 4 tu dhidi ya Yanga na kombe 1 kati ya 4 kwa muda wote aliocheza Simba. Wakatuaminisha kwamba kuna mtu anaitwa Kiongera, akija huyo Yanga kwishney! Huyo naye hakufua dafu. Wakajinasibu kuwa Mavugo ndiyo mwisho wa yote, baada ya kucheza msimu mmoja wote tunaufahamu uwezo wake.
Baada ya juhudi zote kushindikana, sasa mnyama kaamua kuingia kwenye kundi la timu ya wananchi na Azam pamoja na kurudia matapishi ya Okwi akiamini wachezaji hao watampa kikombe.
Haijafahamika wakikosa kikombe sijui hali itakuwaje!!!😉😉😉😉😉😉😉