Yanga yapigwa nyundo ya Tsh. Milioni 82 na CAF

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la soka Afrika (CAF) imeitoza Klabu ya Yanga faini ya jumla ya dola Elfu 35 (takribani Tsh milioni 82) kwa matukio kadhaa kuhusiana na klabu ya Rivers United ya Nigeria.

1. Yanga SC imetozwa faini ya dola Elfu kumi kwa matumizi ya fataki na vitochi kwenye mchezo dhidi ya Rivers United katika dimba la Benjamin Mkapa.

2. Yanga imetozwa faini ya dola Elfu 35 ($ 25,000) kutokana na tukio la basi la timu waliokuwa wamepanda Rivers United kuvamiwa na kuibiwa pesa takribani dolla 5200 na kupuliziwa kemikali inayodaiwa kuwa ni sumu

Pesa hizo zinapaswa kulipwa ndani ya siku 60 huku Yanga ikipewa siku tatu za kukata rufaa baada ya siku ya kutolewa kwa Uamuzi huom

Aidha CAF imeisisitiza Yanga kuhakikisha usalama wa Timu pinzani kuelekea mchezo wa Nusu fainali ya #CAFCC dhidi ya Marumo Gallants katika dimba la Benjaminn Mkapa ambapo visa kadhaa vimeripotiwa hukusiana na uwanja huo.
 
Watalipa Pia Haina Mashiko Maana Yanga Imeshashinda Hiyo Game
 
Kumbe utopolo ndio wanapulizia wageni dawa halafu wananyanyua pua zao kila siku kuwasema Msimbazi, bora CAF wamemaliza utata.
 
Weka source ya hii taarifa
Siku hizi mnakwepa kodi hiyo ni pesa ndogo.
FvhSfsnXsAgACB0.jpg
FvhSfskWIAApPCS.jpg
 
Nyie ni vibaka.
Sawa, lakini soka la Africa lina safari ndefu sana. Yaani mtu anajisemea tu kuwa kaibiwa ela na kuaminika tu. Sijui ni kipi kilichofanyika ili kuchunguza kama kweli kulikuwa na ela. Na sijui hatua ipivwamefanya ili kujua kama waliyofanya hayo ni Yanga na sio Rivers wenyewe wamesuka mpango.
 
Mbona kuna wale wajinga walijisemea kwamba Simba Sc imewapulizia dawa vyumbani wakagoma kuingia ndani, na kujilaza nje kizembe lakini CAF hawakuichukulia hatua Simba?

Utopolo kubalini tu nyie ni vibaka.
 
Mo na CAF ni 10 daima damdam. Huyo kibaka wenu hajui hata ofisi za CAF ziko wapi. Anaendaje buguruni kwenye ofisi ya CUF kulipia faini timu yake iliyopigwa na CAF?
 
Hopefully na Wydad wamepewa adhabu kwa kuwasha moto
Otherwise ni wivu[emoji124]
Kwani Simba walilalamika?
Mmeadhibiwa kwa kuwa Rivers walilalamikia vitendo mlivyowafanyia na maafisa wa CAF walienda kushuhudia na wakajiridhisha kuwa mmepulizia kemikali ya sumu

Sent from my Infinix X626 using JamiiForums mobile app
 
Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la soka Afrika (CAF) imeitoza Klabu ya Yanga faini ya jumla ya dola Elfu 35 (takribani Tsh milioni 82) kwa matukio kadhaa kuhusiana na klabu ya Rivers United ya Nigeria.

1. Yanga SC imetozwa faini ya dola Elfu kumi kwa matumizi ya fataki na vitochi kwenye mchezo dhidi ya Rivers United katika dimba la Benjamin Mkapa.

2. Yanga imetozwa faini ya dola Elfu 35 ($ 25,000) kutokana na tukio la basi la timu waliokuwa wamepanda Rivers United kuvamiwa na kuibiwa pesa takribani dolla 5200 na kupuliziwa kemikali inayodaiwa kuwa ni sumu

Pesa hizo zinapaswa kulipwa ndani ya siku 60 huku Yanga ikipewa siku tatu za kukata rufaa baada ya siku ya kutolewa kwa Uamuzi huom

Aidha CAF imeisisitiza Yanga kuhakikisha usalama wa Timu pinzani kuelekea mchezo wa Nusu fainali ya #CAFCC dhidi ya Marumo Gallants katika dimba la Benjaminn Mkapa ambapo visa kadhaa vimeripotiwa hukusiana na uwanja huo.
hao CAF wametuingizia zile pesa zetu za nusu,tuanzie hapo kwanza
 
Uzuri tumewalioa kisasi nje ndani! Pesa kitu gani bhana. Na bado kuna nafasi ya kukata rufaa. Naamini Wanasheria wa timu watakaa na kuisoma hiyo hukumu kwa kina.
 
Back
Top Bottom