Yanga yapigwa nyundo ya Tsh. Milioni 82 na CAF

Yanga yapigwa nyundo ya Tsh. Milioni 82 na CAF

Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la soka Afrika (CAF) imeitoza Klabu ya Yanga faini ya jumla ya dola Elfu 35 (takribani Tsh milioni 82) kwa matukio kadhaa kuhusiana na klabu ya Rivers United ya Nigeria.

1. Yanga SC imetozwa faini ya dola Elfu kumi kwa matumizi ya fataki na vitochi kwenye mchezo dhidi ya Rivers United katika dimba la Benjamin Mkapa.

2. Yanga imetozwa faini ya dola Elfu 35 ($ 25,000) kutokana na tukio la basi la timu waliokuwa wamepanda Rivers United kuvamiwa na kuibiwa pesa takribani dolla 5200 na kupuliziwa kemikali inayodaiwa kuwa ni sumu

Pesa hizo zinapaswa kulipwa ndani ya siku 60 huku Yanga ikipewa siku tatu za kukata rufaa baada ya siku ya kutolewa kwa Uamuzi huom

Aidha CAF imeisisitiza Yanga kuhakikisha usalama wa Timu pinzani kuelekea mchezo wa Nusu fainali ya #CAFCC dhidi ya Marumo Gallants katika dimba la Benjaminn Mkapa ambapo visa kadhaa vimeripotiwa hukusiana na uwanja huo.
Hawa wehu nini, Wydad Casablance wapiga fataki na Tochi dhidi ya Simba, wamechukuliwa hatua gani?

Kuvamiwa na kupuliziwa sumu Yanga wanahusika vipi? Kwani yanga ni kampuni ya ulinzi? Walipuliziwa sumu halafu wakabaki hai?!

Wakate rufaa!!
 
Sawa, lakini soka la Africa lina safari ndefu sana. Yaani mtu anajisemea tu kuwa kaibiwa ela na kuaminika tu. Sijui ni kipi kilichofanyika ili kuchunguza kama kweli kulikuwa na ela. Na sijui hatua ipivwamefanya ili kujua kama waliyofanya hayo ni Yanga na sio Rivers wenyewe wamesuka mpango.
Nilisema siku ile mkanibishia, mngetoa ulinzi wa kutosha ikiwemo mahali basi lilipopaki mngekuwa na pa kujitetea na hata hii incident isingetokea au walinzi wangekuwa wa kwanza kutoa mrejesho nini kimetokea. Hii ni wahuni wenu tu mliwatuma ila ni ujinga mkubwa sana mmefanya aisee.

Tukiyaacha hayo, huu uwanja wa Mkapa ukiendelea hivi utakuja kufungiwa, matukio ya hovyo yamezidi sana msimu huu mmoja.
 
Sawa, lakini soka la Africa lina safari ndefu sana. Yaani mtu anajisemea tu kuwa kaibiwa ela na kuaminika tu. Sijui ni kipi kilichofanyika ili kuchunguza kama kweli kulikuwa na ela. Na sijui hatua ipivwamefanya ili kujua kama waliyofanya hayo ni Yanga na sio Rivers wenyewe wamesuka mpango.
Afrika kuna upuuzi mwingi sana, eti wameibiwa dola 5000
 
Simba SC ilizikwa ile siku ya Simba (Simba Day)!
118fe697ae204d0ca9a45e289e3e01a5_345243350_556654289916613_2075794506801275514_n.jpg
 
Uzuri tumewalioa kisasi nje ndani! Pesa kitu gani bhana. Na bado kuna nafasi ya kukata rufaa. Naamini Wanasheria wa timu watakaa na kuisoma hiyo hukumu kwa kina.
Yanga ina wanasheria basi? Ongea na morrison akueleze walivyo weupe
 
Majambazi yamepigwa nyundo
UTO
BAHLABANE BA NTWA [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Back
Top Bottom