Yanga yatakiwa kumlipa Luc Eymael Sh. 340m, wakishindwa kufungiwa kusajili

OKW BOBAN SUNZU

Platinum Member
Joined
Aug 24, 2011
Posts
53,868
Reaction score
121,001
Kocha wa zamani wa Yanga, Luc Eymael amesema kuwa timu hiyo haijafungiwa kusajili madirisha matatu na Shirikisho la Kimataifa la Soka (FIFA) kwa kosa la kuchelewa kumlipa madai yake.

Na badala yake, Eymael ameiambia Mwanaspoti kuwa uamuzi uliotolewa na FIFA ni kuishinikiza Yanga kulipa madai yake ili isikumbane na adhabu hiyo.

Kauli hiyo ya Eymael imekuja muda mfupi baada ya mtandao mmoja wa Afrika Kusini kudai kuwa Yanga imefungiwa kusajili kwa madirisha matatu kwa kosa la kutomlipa kocha huyo.

"Nadhani walioandika taarifa hiyo wameripoti kinyume. FIFA walitoa uamuzi na pande zote tumejulishwa kwamba Yanga wanatakiwa kunilipa stahiki zangu ndani ya siku 45 na iwapo wakishindwa kufanya hivyo, kuna adhabu kubwa zaidi watapewa ikiwemo ya kufungiwa kusajili."

"Kwa hiyo hawajafungiwa kusajili. Wamejulishwa uamuzi wa kutakiwa kunilipa fedha zangu," alisema Eymael.
 
Kocha wa zamani wa Yanga, Luc Eymael amesema kuwa timu hiyo haijafungiwa kusajili madirisha matatu na Shirikisho la Kimataifa la Soka (FIFA) kwa kosa la kuchelewa kumlipa madai yake...
Yanga kwa nini wanakuwa na tabia za dhuluma? Wamlipe pesa zake huyo mzungu. Yanga ni matapeli ndiyo maaana Fei Toto kaamua kujiweka pembeni na haya mauzauza.
 
Nakutukana na Hela unanilipa.....
Hutaki unafungiwa usajili.
Kwanini Hersi anapambana kuaminisha watu yanga ina msuli wa fedha? ( sote tunajua hela pale hamna)
@Illmatic kusema kweli sasa hivi pale Yanga pana bonge moja la ukata. Ni suala la muda tu.
 
jibu swali ndipo uulize swali.

NIMEKUULIZA KATI YA HAYA MAJINA MAWILI UNACHAGUA JINA GANI?

(A) MBWA
(B) MBUMBUMBU.
Sasa unanilazimisha nichague kitu ambacho sitaki? Sio kila kitu lazima uchague bali unachagua unachokitaka. Kwahiyo kama wewe utachagua kati ya hayo majina mawili basi ni mapenzi yako
 
Kocha wa zamani wa Yanga, Luc Eymael amesema kuwa timu hiyo haijafungiwa kusajili madirisha matatu na Shirikisho la Kimataifa la Soka (FIFA) kwa kosa la kuchelewa kumlipa madai yake.

Na badala yake, Eymael ameiambia Mwanaspoti kuwa uamuzi uliotolewa na FIFA ni kuishinikiza Yanga kulipa madai yake ili isikumbane na adhabu hiyo.

Kauli hiyo ya Eymael imekuja muda mfupi baada ya mtandao mmoja wa Afrika Kusini kudai kuwa Yanga imefungiwa kusajili kwa madirisha matatu kwa kosa la kutomlipa kocha huyo.

"Nadhani walioandika taarifa hiyo wameripoti kinyume. FIFA walitoa uamuzi na pande zote tumejulishwa kwamba Yanga wanatakiwa kunilipa stahiki zangu ndani ya siku 45 na iwapo wakishindwa kufanya hivyo, kuna adhabu kubwa zaidi watapewa ikiwemo ya kufungiwa kusajili."

"Kwa hiyo hawajafungiwa kusajili. Wamejulishwa uamuzi wa kutakiwa kunilipa fedha zangu," alisema Eymael.
Eymael aliiongoza Yanga kumaliza katika nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi kuu Tanzania Bara ingawa alitimuliwa baada ya kutoa lugha ya kashfa kwa mashabiki wa Yanga.

Source Mwanaspoti
 
Back
Top Bottom