Yanga yatwaa ubingwa VPL msimu wa 2015 / 2016

Hizi raha za Yanga zimezidi sasa,maana hadi nashindwa kushangilia.
Ubingwa kawaida yetu...
Na tuzidi kuwa wa kimataifa milele..
Amiin [emoji120]
 
Klabu hii inaitwa YOUNG AFRICANS SPORTS CLUB na siyo Dar Young African

Hebu niongeze hapa: Klabu hii inaitwa YOUNG AFRICANS SPORTS CLUB na siyo Dar young African. Jina jingine linalotumika ni YANGA lakini hili siyo rasmi. Klabu hii ina copyright kwa YOUNG AFRICANS SPORTS CLUB, YANGA na rangi zake za njano na kijani na pia neon JANGWANI. Imesajili pia nembo yake. Ukitumia nenbo ya klabu hii, rangi zake, majina yake (YOUNG AFRICANS, YANGA, JANGWANI) kwa shughuli za biashara ni kosa na unaweza kushitakiwa mahakamani na kulipa fedha kwa mamilioni. Maana yangu ni kuwa wale wote wanaojinufaisha kwa kufanya biashara ya jezi, scarf na bidhaa nyingine zote zenye nembo au majina ya klabu hii au rangi zake wanafanya kosa...Nilichoandika hapa nina uhakika wa asilimia 100. Klabu hii ilijsajili copyright yake karibu miaka nane iliyopita...Kwanini watu wanajinufaisha kwa kuuza jezi na bidhaa nyingine zenye alama ya klabu hii jni jambo ambalo linatushangaza baadhi tunaofahamu suala hili. Majipu yako mengi.... Halafu waandishi wa habari wakiwemo wa magazeti, redio na vituo vya televisheni ndio wanaopotesha jina la klabu, utawasikia na kusoma wakitaja DAR YOUNG AFRICANS bila hata iabu, huo ni upotoshaji mkubwa wa jina la klabu hii.
 
Kwa Faida yako na wenzako wa Kizazi cha Facebook acha nikupe historia kamili ya Yanga.

Katika miaka ya 1920 Mpaka 1925 vijana wa enzi zile tulikuwa na kawaida ya kukutana maeneo ya Jangwani kufanya Mazoezi ya Hapa na Pale ya Mpira wa Miguu. Vijana wa enzi hizo tulikuwa na desturi ya kukutana viwanja vya jangwani kufanya mazoezi na baada ya muda tukaamua kuunda timu yetu iliyoitwa Jangwani Boys. Ndani ya kipindi kifupi timu yetu iliteka hisia za wengi, wanachama wengi walijitokeza kujiandikisha uanachama. Miongoni mwa waliovutiwa na kujiunga na uanachama alikuwa ni Tabu Mangala (Ambaye sasa ni Marehemu) na ilipofika Mwaka 1926 tulifanya mkutano wetu wa kwanza katika eneo ambalo sasahivi kuna shule ya sekondari ya Tambaza.

Miongoni mwa yaliyojadiliwa kwenye mkutano huo ni kuboresha timu yetu ya Jangwani Boys ambayo waachezaji wake wengi walikuwa ni wafanyakazi wa bandarini na Mashabiki wengi walikuwa ni wabeba mizigo wa Bandarini. Baada ya mkutano huo, timu ilibadilishwa jina na kuitwa Navigation, iliyotokea kuwa moto wa kuotea mbali katika timu za waafrika enzi hizo, kabla ya uhuru wa Tanganyika. Timu kama Kisutu, Kitumbini, Gerezani na Mtendeni zilikuwa hazifui dafu kwa Wana wa Jangwani.

Ikiwa inatamba kwa jina la Navigation, wanachama walikuwa wanatembea kifua mbele na kuwatambia wapinzani wetu. Baadae timu ilibadilishwa jina kutoka Navigation na kuitwa Italiana kwasababu Italy enzi hizo ndiyo iliyokuwa inavuma katika Medani ya Soka. Italiana FC ilipata Mafanikio makubwa sana na ya haraka na tuliwashangaza wengi sana na kupanda ligi daraja la pili Dar es salaam.

Mwanzoni mwa miaka ya 1930 italiana FC ikabadili jina na Kuwa Dar es salaam Youngs na wengi walikuwa wanatujua au kututambua kwa jina la New Youngs. Kila timu ilipokuwa inabadili jina ilikuwa pia ikifanya vitu vipya na kushangaza uwanjani. Tukiwa na jina la Dar es salaam Young au New Youngs tuliweza kutwaa kombe la Kassum, lililoshirikisha timu mbalimbali za Dar es Salaam.

Hatimaye ukawadia Mwaka mbaya kwa Dar es salaam Young au New Youngs mwaka 1938 baadhi ya Wachezaji walijitoa na kwenda kuanzisha Sunderland au Simba SC ya sasahivi na hapo ndipo upinzani wa Jadi ulipoanzia. Katika kipindi hicho cha mwaka 1938 sisi tuliobakia tuliamua kubadili jina kutoka Dar es Salaam Young au New Young na Kujiita Young Africans, jina ambalo mashabiki wetu wengi walishindwa kulitamka vizuri na kujikuta wakisema Yanga.

Pia kwa kukumegea tu kidogo Rais wa Awamu ya NNE mh. Jakaya Mrisho Kikwete alikuwa ni Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili wa Young Africans mwaka 1976 na ndiye alifanikisha kusajiliwa kwa Mchezaji mahiri na Machachari Uwanjani Shaaban Katwila. Nadhani Mpaka hapo utakuwa umepata jibu Kwanini Naiita Yanga ya Leo Dar Young Africans.

Kwa wewe kwasababu zako za kibiashara na issue zenu za kisasa sijui brand sijui copyright iite uitakavyo. Mimi nitaendelea kuiita Dar Young African mpaka mwisho wa uhai wangu kwani ndio jina lililoibeba klabu enzi hizo kabla ya uhuru.
 
Heeeeh, makubwa...Nadhani hatujaelewana...ngoja niishie hapo...JF ina mambo, mijadala ya aina hii mtu unaweza ukajikuta unamwaga hadharani ID yako...nakushukuru comrade, mchana mwema.
 
Back
Top Bottom