SoC03 Yangu majuto

Stories of Change - 2023 Competition

Fide Simbili

New Member
Joined
Jul 26, 2022
Posts
4
Reaction score
4
Karatasi nalivuta, Natamani kuandika,
Mambo yaliyonikuta, mwili unatetemeka,
Nani wa kuyafuta, Machozi yananitoka,
Ninaishia kujuta, Kila ninapokumbuka,

Nilikua mgomvi, Makundi kutengeneza,
Nilikua ajizi, mazuri kuyapoteza,
Nilikua jambazi , wanyonge kuwaumiza,
Nilikua bazazi , uongo kuendeleza,

Niliua wazazi, Baraka kuzipoteza,
Nilihama makazi, Mali zao kuziuza,
Sikuitaka kazi, Vya watu kuendekeza,
Sasa nipo kitanzi, Nashindwa kuyaeleza,

Mwili wapata ganzi, Ndugu kuwapoteza,
Natokwa na Machozi, Sina nilichobakiza,
Ninashindia andazi, Pesa nilishapoteza,
Waliokua wapenzi, Wote nimewapoteza,

Sasa ninajiuliza, Nini kinaendelea,
Macho yametanda Giza, Kila nikitizamia,
Dunia ya miujiza, Wapi nilipofikia,
Napaswa kuyaeleza, Tusije kuyarudia,

Serikali yahimiza, Upendo kuendeleza,
Tuepuke kuteleza, Sheria itatufunza,
Sheria kuzigeuza, Amani tutapoteza,
Tuudumishe Umoja,mema kuyaendeleza
 
Upvote 1
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…