Tetesi: Yani mimi kila ikifika zamu yangu kwenye foleni mtoa huduma ndio anaondoka

Tetesi: Yani mimi kila ikifika zamu yangu kwenye foleni mtoa huduma ndio anaondoka

Superbug

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2018
Posts
13,864
Reaction score
35,079
Nachukizwa Sana na hili jambo sidhani Kama wewe lishawahi kukükuta kila nikiwa kwenye foleni ikifika zamu yangu Mtoa huduma ndio ana nyanyuka na kuondoka
Nimefanya risechi iwe ni

Hospital
Bank
Kanisani mikate inaisha

kila penye foleni nikifikiwa Mimi ndio Jamaa anasepa
Pengine bila hata sababu ya msingi
Wewe je?

Naumia Sana
 
Nachukizwa Sana na hili jambo sidhani Kama wewe lishawahi kukükuta kila nikiwa kwenye foleni ikifika zamu yangu Mtoa huduma ndio ana nyanyuka na kuondoka
Nimefanya risechi iwe ni

Hospital
Bank
Kanisani mikate inaisha

kila penye foleni nikifikiwa Mimi ndio Jamaa anasepa
Pengine bila hata sababu ya msingi
Wewe je?

Naumia Sana
Utakuwa na mapepo ya 3D (waswahili wanaita KIMAVI) , njoo PM tukupe ubani!!!
 
Inaweza kuwa ni coincidences tu na vile unawaza juu ya hilo ndio maana unahesabu au unakumbuka kila linapotokea.
 
teh..teh...teh...sijui nianzaje lakini wacha nichangie nipakapofikia ila usichukie ikiwa ukikutana na ukweli.
  1. kwanza anza kujikubali wewe mwenyewe na uelewe kuwa wewe si mtu wa kawaida umebwa tofauti na mwingine kama tunavyosema kwenye management kuwa kila binadamu yuko tofauti na katika kuliona hili usipende kuangalia udhaifu wako bali angalia uwezo wako na thamani yako.
  2. umejikataa na sasa inawezekana kabisa umeanza kujenga mazingira ya watu kukukataa ussikubali hali hii chochote kinachotokea kubali ni kwa bahati mbay zamu yako ipo na wewe ni wakupata sio kukosa.
  3. ipo hali ya malalamiko kwako pia ambayo inawezekana ilianza toka utoto wako na umekuwa nayo inawezekana ulikuwa mdogo hivyo wakubwa zako walikuwa wanakuonea au ulikuwa mkubwa na peke yako kwa muda mrefu mfano kupishana umri mkubwa na mdogo wako na anapokuja wazazi wanakata ghafla upendo kwako na kukubebesha maumivu ambayo unakuwa nayo.
  4. ipo changamoto pia wakati wa utoto kumtegemea mtu fulani inawezekana mzazi mmoja kwa kuwa yeye ndiye mtetezi wako na ikatokea akafariki na ukaona umekosa mtetezi na hata unapokuwa mtu mzima bado unakutana na changamoto ya kutojiamini.
zipo nyingi lakini muhimu jiamini na jikubali na mambo yatakwenda sawa.
 
UNA bahati sana wewe kijana ivo shetani anakukatisha tamaa, hao wote wanaopendelewa kwenye foleni wameshakufa au watakufa mapema kuliko wewe na wewe binafsi uko/utakuwa juuu sana. kiuchumi, kiroho, ki mwili na kiafya

unapigwa vita vya kiroho na ibilisi ili upoteee kwa kujidharau amini maneno yangu, au fanya hivi;

pima kati ya wao na wewe nani ana akili nyingi?

je ni nani anajua mambo mengi,

level yako kistandard ya maisha ikoje na wao ikoje fanya research lete mrejesho nikupe akili, usikose
 
duuuh kazi ipo ila jikubali tu ndugu

lakini hili lako sio tetesi kama unavyoelezea. bali ni hali inayokutokea.
 
Back
Top Bottom