Inasikitisha Sana....... Hapa madongo yote yanaelekea kwa single mother lakini so kweli,,
Asilimia kubwa ya wazazi Tanzania wako tayari kuzaa na so kulea!!!! Malezi ya watoto yanataka fedha, muda, hisia, kujali , kuthamini sasa tulio wengi tunaachia dada wa kazi , ndugu, majirani, jamaa na marafiki watutimizie majukumu yetu. Nashauri Kama hauko tayari kubeba jukumu la mzazi hakikisha mbegu zako unakaa nazo kiunoni mpka utakapokua tayari..... Uwe wa kiume au wa kike kaa tulia ukiwa tayari kuwa mzazi ndio uanze kuzaa. Sioni mantiki ya kuzalisha mtoto wa watu umuachie majukumu uanze kumuita single maza huku wewe single father ukitega ukila starehe na wanawake wengine.