Yapi Merkezi: Hakuna Mfanyakazi wa SGR atakayefutwa kazi bila kulipwa stahiki zake ikiwemo NSSF

Yapi Merkezi: Hakuna Mfanyakazi wa SGR atakayefutwa kazi bila kulipwa stahiki zake ikiwemo NSSF

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Baada ya Mwanachama wa JamiiForums.com aliyejitambulisha kuwa Mfanyakazi wa Mradi wa Ujenzi wa Reli ya SGR kulalamikia kuhusu Mkandarasi Mkuu wa Mradi, Yapi Merkezi, kuwa anawaondoa watu kazini kwa lazima kwa njia ya likizo na kuwa haingizi malipo ya NSSF, ufafanuzi umetolewa na Mkandarasi.

Kusoma hoja ya Mdau bofya hapa ~ Mkandarasi wa SGR (Yapi Merkezi) anawaondoa Wafanyakazi kwa gia ya kuwapa likizo ya lazima, pia hajaingiza malipo ya NSSF

Ufafanuzi wa YAPI MERKEZI...
YAPI MERKEZI'S RESPONSE_page-0001 (1).jpg

Tunapenda kutoa ufafanuzi wa kuhusu taarifa zilizochapishwa na Vyombo vya Habari kuhusu mabadiliko ya operesheni ndani ya Yapi Merkezi, baada ya mafanikio na kuanza kwa shughuli za treni kwa kutumia reli ya Kiwango cha Kimataifa (SGR) katika Lot-1 na Lot-2.

Ni muhimu kufafanua kwamba mabadiliko haya yamesababisha kupungua kwa idadi ya wafanyakazi, Ingawa tunajitahidi kusimamia kipindi hiki cha mpito kwa haki na kwa heshima kubwa kwa wanafanyakazi wetu wa mradi.

Zaidi ya hayo, tunapanga kwa umakini kuwapanga wafanyakazi hawa kwenye miradi mipya inavyoibuka, kuhakikisha kwamba ujuzi wao na uzoefu wanaendelea kuchangia katika mafanikio ya Kampuni Yapi Merkezi.

Tungependa pia kuweka wazi kwamba hakuna mfanyakazi atakayefutwa kazi bila kuhakikisha kuwa manufaa yote yanayostahili, ikiwa ni pamoja na michango ya Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), yamelipwa kwa ukamilifu na kuwa katika hali nzuri. Hii ni ahadi tunayoichukulia kwa umakini mkubwa kama sehemu ya wajibu welu kwa wafanyakazi wetu.

Tunathamini sana juhudi za Wafanyakazi wetu na tunaendelea kujitolea kuwasaidia katika kipindi hiki cha mpito.
 
Back
Top Bottom