Yapi ni matukio yako makubwa kimichezo 2024?

Yapi ni matukio yako makubwa kimichezo 2024?

MwananchiOG

JF-Expert Member
Joined
Apr 4, 2023
Posts
1,970
Reaction score
4,037
Je, Matukio gani makubwa utayakumbuka katika ulimwengu wa kimichezo kwa mwaka 2024?

Kwa upande wangu, ni mengi yametokea, Ila haya nadhani yamechukua nafasi kubwa

1.Yanga kutwaa ubingwa wa Ligi kuu mara ya 30 na mara ya tatu mfululizo

2.Yanga kufuzu robo fainali CAFCL

3.Goli la Aziz ki lililokataliwa Vs Mamelodi sundowns SA

4.Tanzania kufuzu AFCON kibishi sana baada ya kukatiwa tamaa na hatimaye kumfunga Guinea. Hii imenifanya kumuona kocha Moloko si mtu wa kawaida, kwani pamoja na kufungwa michezo ya nyumbani ikiwemo Congo DRC na kupoteza matumaini, ila huyu mtu aliapa na kusema kufuzu ni lazima, na kweli ikawa hivyo bhana!

5. Yanga kumfunga Kaizer chiefs kiulaini kabisa na kutwaa kombe la Toyota SA
 
hayo ni matukio makubwa duniani? Africa, Tanzania au katika klabu ya Yanga?
 
hayo ni matukio makubwa duniani? Africa, Tanzania au katika klabu ya Yanga?
Hayo ni matukio makubwa kwangu, kama shabiki wa Yanga na Taifa stars, Je, kwa upande wako na kulingana na club unayoshabikia yapi yalikuwa matukio yaliyokugusa?
 
Kwangu mimi tukio ni moja tu katika mwaka huu wa 2024. Simba kufungwa ×3 mfululizo kwa mwaka mmoja, yaani kapigwa Ktk NBC PL msimu 2023/24 bao mbili moja, kapigwa ngao ya jamii moja bila,kapigwa tena nbc pl 2024/25 moja bila. hiuyo akakamilisha hesabu ya vipigo vinne vitakatifu mfululizo. ahsanteni.
 
Back
Top Bottom