Yas yazindua mnara wa mawasiliano wa 5g Kinyerezi

Yas yazindua mnara wa mawasiliano wa 5g Kinyerezi

News TZ

Senior Member
Joined
Jun 17, 2015
Posts
169
Reaction score
88
IMG_9894.jpg

Kampuni ya mawasiliano ya YAS imezindua rasmi mnara wa mawasiliano wa teknolojia ya 5G katika eneo la Kinyerezi – Zimbili, Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam, katika hafla iliyofanyika tarehe 28 Aprili 2025 na kuhudhuriwa na viongozi wa Serikali na wakazi wa maeneo ya jirani.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Mkurugenzi wa YAS Kanda ya Kusini, Bw. Robert Kasulwa, alisema mnara huo ni sehemu ya mkakati wa Kampuni hiyo wa kusambaza teknolojia ya mawasiliano ya kisasa katika maeneo mbalimbali nchini, ikiwa ni utekelezaji wa ahadi iliyotolewa tangu mwaka 2022 ya kuboresha miundombinu ya mawasiliano.

“ Zaidi ya minara 300 ya 5G imeshajengwa jijini Dar es Salaam pekee, na hii inaonesha dhamira ya dhati ya YAS katika kuhakikisha kila Mtanzania anapata huduma bora za mawasiliano,” alisema Bw. Kasulwa.

Aliongeza kuwa uwepo wa teknolojia hiyo ya 5G katika maeneo ya pembezoni kama Kinyerezi – Zimbili unalenga kuongeza ufanisi katika sekta mbalimbali zikiwemo biashara ndogondogo, elimu, afya na upatikanaji wa taarifa mtandaoni, jambo litakalosaidia wananchi kuinua hali zao za maisha.

“Teknolojia ya 5G inatoa fursa ya huduma za uhakika, zenye kasi ya hali ya juu na zinazoweza kutegemewa, hivyo ni chachu ya maendeleo katika nyanja zote za kijamii na kiuchumi,” alisisitiza.

Uzinduzi huo pia umeelezwa kuwa unaendana na mpango wa kidigitali wa Serikali, unaolenga kuhakikisha teknolojia ya habari na mawasiliano (TEHAMA) inawafikia Watanzania wote ili waweze kushiriki kikamilifu kwenye maendeleo ya taifa.

Katika hotuba yake, Bw. Kasulwa alitumia nafasi hiyo kuishukuru serikali kwa ushirikiano wake na kuahidi kuwa YAS itaendelea kushirikiana kwa karibu na mamlaka mbalimbali katika kujenga taifa lenye mawasiliano ya kisasa na jumuishi.

Uzinduzi wa mnara huo wa 5G unatarajiwa kuleta mapinduzi ya kiteknolojia kwa wakazi wa Kinyerezi – Zimbili na maeneo jirani, huku ukifungua milango ya fursa mpya kwa vijana, wajasiriamali na sekta nyingine muhimu za uzalishaji.
IMG_9836.jpg
IMG_9999.jpg
 
Ni jambo Jema. Lakini Kwanini wasije na teknolojia ya kutumia hiyo hiyo minara ya 2,3&4G kuibadili kutumia 5G
 
Ni jambo Jema. Lakini Kwanini wasije na teknolojia ya kutumia hiyo hiyo minara ya 2,3&4G kuibadili kutumia 5G
Actualy tz minara mingi ndio inafanya kazi hivo. Wanachofanya ni kuongeza antenna za 5g , plus tanzania bado inatumia 2g,3g ,4g tech moaka leo duo to wananchi kutokuweza ku access na ku afford latest tech
 
Back
Top Bottom