Ee Mwenyezi Mungu mapenzi yako yatimizwe katika kila kitu.
Nakemea kila nia ovu juu ya mchezo huo.
Ashinde yeyote uliyempa kibali mbele zako.
Acha baraka zako zimiminike ee Bwana, Acha ukuu wako uonekane ee Bwana. Jidhihirishe katika kazi za watu wako wenye nia nyofu mbele zako Bwana.
Ukadhihirike ,ukaonekane kati watu wako Bwana.Tazama mchezo huo ni ajira kwa watu wako Bwana.
Nakemea roho za shirki, imani potofu nakila kitu kilicho kinyume na mapenzi yako Bwana.
Mungu wa Ibrahim Mungu wa Isaka Mungu aa Yakobo jina lako litukuzwe katika watu wote.
Nanaomba hayo kwa njia ya Yesu Kristo Bwana na mwokozi wa maisha yangu.
Amina.