Yatakayojiri baada ya Yanga kutolewa na Al Hilal kesho huko Sudan

Mwishokambi

JF-Expert Member
Joined
Nov 23, 2020
Posts
390
Reaction score
1,425
1. Mchezo ulikuwa wetu kabisa ule, sema wachezaji wetu wazembe sana.

2. Kocha naye kazingua sana, amechelewa sana kufanya sub.

3. Morrison naye utoto amezidi, sasa pale baada ya kufunga analeta ubishoo.

4. Kisinda angebakia kule kule Berkane, kazi yake kukimbia tu kama swala.

5. Bangala kwanini achezeshwe namba 5 wakati akicheza sita ndio ananoga?

6. Mwamnyeto siyo mchezaji wa kuchezea Yanga.

7. Aziz Ki hamna mtu mle, tumepigwa.

8. Fei Toto anasumbua bongo tu, ugenini kawa ulojo.

9. Hasira zetu sasa tuzimalizie kwa Simba tarehe 23.

10. Nabi atuachie timu yetu.

Sent from my SM-F916B using JamiiForums mobile app
 
umekunywa mbege lita ngapi wewe?
 
Watavurugana sana kesho bila sababu wakati timu yao ni ndogo kimataifa
 
Nimecheka haswaa.

Nimesikiliza videos instagram, kwa hakika ndicho wanachokisema.

Ahsante sana Mkuu.
 
Naona umebakia tu na aibu! Maana hali ya hewa iko shwari kabisa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…