ladyfurahia
JF-Expert Member
- May 10, 2011
- 14,753
- 9,575
Habarini marafiki
Leo nimeona niwafundishe WANAWAKE wa kileo mambo yasuhuyo WATOTO
na jinsi ya KUMNYONYESHA MTOTO ALIYE MCHANGA,
Msishangae kwaniini nimekuja na mada hii hapa kwani ilitokea hivi juzi kati
mtaani kwetu kuna Mama amejifungua mtoto na anashindwa namna ya
kumnyonyesha mtoto anabaki kuyakamua maziwa na kuweka kwenye chupa
kisingizio chake ni eti maziwa yataharibika shepu. Kwani ulivyoamua kuolewa
na kwenda kujenga NDOA yako ulifikiri mambo hayo hayatakuwepo kwako bidada?
Ngoja nisiende mbali niwape dondoo au vidokezo kidogo vya kuweza kumnyonyesha
mtoto wako mchanga pindi unapotoka kujifungua.
PATA HIZO DONDOO ZA UNYONYESHAJI MARA BAADA YA KUJIFUNGUA
Kumuanzishia mtoto kunyonya maziwa ya mama
0.1 Hatua za kumwanzishia mtoto kunyonya maziwa ya mama
♦ Mara tu baada ya kuzaliwa, muweke mtoto kifuani kwa mama ngozi zao zikiwa zinagusana ili
kumpa mtoto joto na kuhamasisha unyonyeshaji mapema
♦ Mtoto aanze kunyonyeshwa ndani ya saa moja mara baada ya kuzaliwa, hii husaidia maziwa ya
mama kutoka mapema na kwa wingi
♦ Mwache mtoto anyonye kwa uhuru bila vikwazo
♦ Hakikisha mtoto ananyonya maziwa ya mwanzo (danga)
Mnyosheshe mtoto mfululizo maziwa ya mama pekee kila anapohitaji; usiku na mchana bila
kumpa kitu chochote hata maji isipokuwa dawa iwapo ameandikiwa na mtaalamu.
0.2. Mnyonyeshe mtoto bila kuacha
♦ Mtoto anyonyeshwa kila anapohitaji, usiku na mchana bila kujipangia muda maalum wa
kunyonyesha
♦ Usiku, mweke mtoto karibu na mama ili kumrahisishia mtoto kunyonya kila atakapo hitaji
♦ Mnyonyeshe mtoto titi moja kwa muda kisha jingine ili mtoto apate maziwa ya mwisho ambayo
yana virutubisho vingi vinavyompa nguvu kuliko maziwa ya mwanzo
♦ Iwapo/mtoto amenyonya titi moja na anakataa kunyonya la pili, hakikisha kuwa atakapohitaji
tena kunyonya, anza kumnyonyesha titi la pili ili yote yanyonywe kwa uwiano sawia
0.3 Mambo muhimu ya kumshauri mama ayazingatie katika unyonyeshaji wa maziwa ya
mama pekee, mfululizo
♦ Mtoto anyonyeshwe mfululizo maziwa ya mama pekee kwa kipindi cha miezi sita ya mwanzo
na bila kupewa kitu chochote hata maji (Isipokuwa dawa pale anapoandikiwa na mtaalamu wa
huduma za afya
♦ Endelea kumnyonyesha mtoto hata kama mama au mtoto ni mgonjwa
♦ Mama aongeze kiasi cha chakula anachokula na maji ya kunywa (vinywaji)
♦ Mama aepuke kumlisha/nyonyesha mtoto kwa chupa, kikombe chenye mfuniko au chuchu
bandia.
0.4 Jinsi ya Kumsaidia mama kumweka mtoto vyema kwenye titi
♦ Mwache mama afanye kadiri anavyoweza mwenyewe, kama ni ikilazimu muonyeshe kwa
vitendo wewe mwenyewe jinsi gani ya kushikilia ziwa na kuendelea. Kama anahitaji msaada
weka mkono wako juu ya mkono wake kuliko kushika ziwa lake.
0.5 Vigezo vya kumweka vizuri kwenye titi
♦ Mama anakuwa amekaa vizuri na kutulia
♦ Kichwa na mwili wa mtoto viwe katika mkao wa kunyooka
♦ Mtoto apakatwe kwa ukaribu na kumuelekea mama
♦ Mwili mzima wa mtoto upakatwe
♦ Kichwa cha mtoto kielekee titi la mama na pua iwe mkabala na chuchu
♦ Kichwa kitazamane na titi
♦ Gusisha chuchu ya mama kwenye midomo ya mtoto
♦ Subiri mpaka mtoto aachame kama vile anapiga miayo
♦ Msogeze mtoto kwenye titi na siyo kumsogezea mtoto titi
♦ Sogeza mwili wote wa mtoto kuelekea kwenye titi na siyo kusogeza kichwa
cha mtoto pekee kwenye titi
ona picha hizi uone muonekano wa jinsi ya kuwanyonyesha watoto
wachanga

Hayo ni baadhi ya mambo ambayo nimewaandalia wanawake wa kisasa
wajue umuhimu na faida za unyonyeshaji wa watoto wao. Somo bado
linaendelea muendelezo wa hatua ingine inafuata. Hivyo mashostito kaeni
mkao wa kupokea na kujifunza hapa kwani ni darasa tosha kwenu na kizazi chote
cc: Mamndenyi, Passion Lady, Lady doctor, amu, charminglady, Smile, Preta, sweetlady, FirstLady, lady focus, Lady Unbreakable, Mama Ngina, Mama v, Heaven on earth, mwallu, mwaJ, measkron, @@Kongosho, gfsonwin, snowhite na
wanawake wote niliowasahau kuwataja hapa karibuni mabesti wangu kama kuna mapungufu
nanyi wekeni hapa
WARNING:
Wanaume wa jf msichakachue na kuharibu thread hii nanyi mjifunze
na kuwafundisha wake zenu namna ya kuwanyonyesha watoto kwani
watoto ni wetu sote. Nawapenda
Wasalaamu;
Ladyf

Attachments
Last edited by a moderator: