Moja ya waombolezaji wakubwa wa msiba wa Ruge ni Konk master.Dudubaya yeye toka moyoni kashajitanabaisha kua hawapendi watu wa clouds media hasa Ruge na watangazaji wengine, anaona hana haja ya kudanganya kwa watu bora aseme ukweli wake ambao probably haukutaka kusikilizwa na watu wengine hasa kwa wakati huu mzito, ukweli wake yeye hampendi marehemu na anaamini marehemu alikua mtu mbaya kwake, hana haja ya kujibadilishia yeye mwenyewe mara tu baada ya mtu yule kufariki, na iko wazi hatukutegemea kama dudu asifurahie majonzi na mambo mabaya ya wana clouds.
1. Simjui ni kabila gani jama lakini tukumbuke kuna utani....
2. Kaombolezea nyumbani hadi kituo cha polisi
3. Anaomboleza kumkosa adui ambaye anadhani madhila yake yote ni sababu ya marehemu! hofu yake ni kesho yake atamsingizia nani? na kaipata kazi ya kutafuta adui mwingine ili maisha yaende.
Nini hasa tufanye ili tuwe jamii iliyostaarabika na kuheshimu kila hisia ya mtu kwa uvumilivu mkubwa ikiwezekana turekebishane pasipo chuki na kuumizana? DAB na wengine tumewanyoshea vidole kuwa ni wanafiki walimuumiza akiwa hai; na hili povu kwa konk latoka wapi?
Ukweli ni kwamba Ruge alikuwa kiongozi imara na bora sana.... watu wote wanalihisi pengo aliloacha kila mtu kwa namna yake.