Yawezekana hayati Magufuli alikuwa anateua watendaji bila kuwahusisha VP na PM?

Yawezekana hayati Magufuli alikuwa anateua watendaji bila kuwahusisha VP na PM?

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Nauliza tu kwa wenye uzoefu na mambo ya teuzi

Naelewa kwamba kila zama na kitabu chake lakini naona kama mama anapata kazi ya ziada kuteua tena.

Kazi Iendelee!

Kesho ni Pentecoste.
 
Wizara ya mambo ya nje ni ya kufumuliwa yote kwa kweli.

Haikuwa wizara inayojua diplomasia, wao walijikita zaidi katika kutunishana misuli na majirani, matifa ya nje na taasisi za kimataifa
Kasikilize hotuba za Kabudi Bungeni na akiwa anaongea na Waandishi mambo ya Diplomasia ndio utajua kweli hakua mtu sahihi
 
Haijalishi.
Hayo ndiyo MAMLAKA, MADARAKA NA WAJIBU ya / wa Rais. Angeamua hata angeweza kuanza UPYA KABISA katika kila Teuzi bila kujali aliyekuwepo alishirikisha mtu au la!
 
Wizara ya mambo ya nje ni ya kufumuliwa yote kwa kweli
Haikuwa wizara inayojua diplomasia, wao walijikita zaidi katika kutunishana misuli na majirani, matifa ya nje na taasisi za kimataifa
Kasikilize hotuba za Kabudi Bungeni na akiwa anaongea na Waandishi mambo ya Diplomasia ndio utajua kweli hakua mtu sahihi
Aisee!
 
Wizara ya mambo ya nje ni ya kufumuliwa yote kwa kweli...
Diplomasia ni nini, ni kukubali matakwa yote ya wazungu au kusimamia mikakati ya watanzania.. Kama diplomasia ya Tanzania ilikua mbaya.

Ya Marekani inayovamia nchi za watu ipo kundi gani. Chuki zinawafanya mshindwe kufikiri. Hakuna hata balozi moja iliyofungwa halafu mnasema diplomasia ilikua mbaya
 
Diplomasia ni nini, ni kukubali matakwa yote ya wazungu au kusimamia mikakati ya watanzania.. Kama diplomasia ya Tanzania ilikua mbaya.. Ya Marekani inayovamia nchi za watu ipo kundi gani. Chuki zinawafanya mshindwe kufikiri. Hakuna hata balozi moja iliyofungwa halafu mnasema diplomasia ilikua mbaya
Mataga itawachukua muda Sana kuamini kuwa tupo awamu ya 6,
Lakini hamjachelewa, Chato nafasi bado ipo.
 
Nauliza tu kwa wenye uzoefu na mambo ya teuzi

Naelewa kwamba kila zama na kitabu chake lakini naona kama mama anapata kazi ya xiada kuteua tena.

Kazi Iendelee!

Kesho ni Pentecoste.
Nakataa tokana na hotuba zake

Kuna hotuba aliwakemea viongozi kutoleta majina watu furani wanaofanya vzr Kwa ajiri ya teuzi

Na akaagiza kuwa wawe wanaleta majina ya watu kama wale Kwa ajiri ya teuzi

Kingine nilichosikia jamaa mmoja mkubwa Tu office za serikali akilalama kuwa kosa alilofanya magufuri katika uteuzi wa Kwanza yeye hakusoma wala kifuatilia majina yeye alifuata tu mikoa iko 26 akaanza namba moja mpaka 26 wa mwanzo na kusema hawa wakuu wa mikoa namba furani mpaka namba furani wakuu wa mikoa .

Na ndiyo maana alikuw anaweza kuteua Leo na kesho yake akatumbua

[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Mataga itawachukua muda Sana kuamini kuwa tupo awamu ya 6,
Lakini hamjachelewa, Chato nafasi bado ipo.
Mimi sio mataga ila nakuona mshamba tuu.. Maana ungetuliza kichwa ungeelewa.. Hao unaowashabikia ndio walikuchukua utumwani sasa leo ndio wamegeuka malaika.. Ni mjinga tuu ndio anaweza jiaminisha hivyo
 
Naendelea kufuatilia huu mtanange huku nakula popcorn
 
Nadhani ndiyo tabia ya kila anayeshika dola anasafisha kila kitu ili kuweka watu wake naye wale keki ya taifa,ila bado kwa panga pangua hizi zote,hazina faida yoyote kwa taifa zaidi ya kuwanufaisha watu binafsi tu.

Katiba ikirekebishwa itasaidia sana kupata watu sahihi kwenye maeneo husika,ila kwa sasa ni panga pangua ileile tu kufurahishana na maandalizi ya neksti elekisheni
 
Naendelea kufuatilia huu mtanange huku nakula popcorn
All in all tukiacha chuki Mwendazake ametufanyia Mambo mengi yenye tija Kama Taifa...Tukubali hakua mwanasiasa mzuri kwaio nawashauri vijana wa bavicha muache chuki mzee wetu apumzike kwa amani.

Tunajua aliwabana Sana mnahasira nyingi poleni basi ,mrudi kwenye kazi yenu Sasa ya kukosoa,kuibua madudu ,tulijenge Taifa.sio huu ujinga mnaofanya Sasa ivi mmepewa nafasi Sasa itumieni.
 
Back
Top Bottom