Yawezekana hizi Tozo Umiza za Kuwaona hawa Manabii Matapeli waliopo Tanzania ndizo zinawafanya Watu waendelee kwenda na kuwaamini Waganga wa Kienyeji

Yawezekana hizi Tozo Umiza za Kuwaona hawa Manabii Matapeli waliopo Tanzania ndizo zinawafanya Watu waendelee kwenda na kuwaamini Waganga wa Kienyeji

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
60,660
Reaction score
121,325
Haiingii Akilini unaenda kupata Tiba ya Kiroho kwa Mtumishi wa Mungu halafu Yeye badala ya Kukuonea Huruma kama alivyokuwa Yesu Kristo anaanza Kukuambia kuwa ili Akuombee na Upone tatizo lako ulilonalo Kwanza utoe Shilingi Laki Tano au Milioni Mbili.

Kwanini GENTAMYCINE nisiendelee kwenda kwa Mganga wangu Hatari aliyeko nyuma ya Milima ya Uluguru (Matomboni) Mkoani Morogoro ambaye Yeye ukienda tu na tatizo lako anakutibia na anakuambia umpe tu Shilingi Mia Mbili ya Sarafu ya Kitanzania au Shilingi Mia Tano na uende na Mafanikio unaanza kuyaona pale pale tu?

Na ni Mganga huyu huyu nilimwomba asababishe Maafa Jangwani na Mtu akafa mara mbili mfululizo na Kuchanganyikiwa.
 
Inahitaji uwe na upungufu wa akili kichwani ili uweze kulipa pesa kumuona mpiga ramli anayejiita nabii, kama mungu hawezi kuzungumza na mimi moja kwa moja hadi apitie kwa manabii na mitume basi huyo ni mbabaishaji tu. Ukitaka kujua dini ni utapeli litazame bara la Africa
 
Kulipa pesa kumuona nabii ni upungufu wa akili!
Lakini kulipa pesa kumuona mchawi ni wingi wa akili!
Hapo sijui punguani ni yupi.
 
Back
Top Bottom