Yawezekana Mbowe anachanganya kwa pamoja madaraka ya KUB na Mwenyekiti wa Chadema na matokeo yake ni kutenda Uonezi!

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Kuna wakati Zitto akiwa Chadema aliwaeleza madhara ya kuweka kanuni inayomfanya mwenyekiti wa Chadema kuwa KUB iwapo ni mbunge na chama kimepata ridhaa ya kuunda kambi rasmi ya upinzani.

Madhara yake ndio haya tunayoyashuhudia sasa. Binafsi sikumbuki kama kuna kikao halali iwe halmashauri kuu au kamati kuu kilikaa na kuamua wabunge wa Chadema waende kwenye karantini wakati bunge likiendelea.

Lakini jana mh Mnyika amedai wabunge waliofukuzwa na wale waliotakiwa kujieleza walikiuka maagizo ya chama kuwataka wajitenge kwa siku 14.

Ikumbukwe kuwa KUB hatoi maagizo ya chama bali anatoa maagizo ya kambi rasmi ya upinzani bungeni.
Wabunge wanaoendelea kuhudhuria bungeni hawajakiuka maagizo yoyote ya chama bali wameshindwa kukubaliana na kiongozi wao wa kambi na wanapaswa kuchukuliwa hatua kwa mujibu wa taratibu za kambi ambazo zipo kwa mujibu wa kanuni za bunge iwapo kweli wamefanya makosa.

Ni vema Mbowe akafahamu ipo tofauti ya MSINGI kabisa kati ya yeye kuwa KUB na yeye huyo huyo kuwa Mwenyekiti wa Chadema.

Mungu awape wepesi makamanda.

Maendeleo hayana vyama!
 
I see your point. Pia, suala la mtu kujitenga ni mpaka awe suspected au aji suspect sasa kwa hawa wabunge CHADEMA sijui imekuwaje!

Kingine hawa wabunge walioamua kuendelea na vikao nao hawana adabu, ilikuwaje waanze kushambulia chama na kiongozi wake aliyewaagiza kujitenga ni KUB na walikuwa na nafasi ya kuwasilisha maini yao matokeo yake tukamuona huyu dogo Silinde akiongea mbovu akiwa lashikiwa mike na Lusinde
 
Nakubaliana na wewe hao wabunge hawakupaswa kukishambulia chama chao ndani ya bunge lililojaa wabunge wa CCM.

Nadhani wamemuiga Rostam Aziz walichosahau ni kwamba Rostam na ubunge wenyewe aliachana nao!
 
Kuna wakati Zitto akiwa Chadema aliwaeleza madhara ya kuweka kanuni inayomfanya mwenyekiti wa Chadema kuwa KUB iwapo ni mbunge na chama kimepata ridhaa ya kuunda kambi rasmi ya upinzani.

Madhara yake ndio haya tunayoyashuhudia sasa. Binafsi sikumbuki kama kuna kikao halali iwe halmashauri kuu au kamati kuu kilikaa na kuamua wabunge wa Chadema waende kwenye karantini wakati bunge likiendelea.

Lakini jana mh Mnyika amedai wabunge waliofukuzwa na wale waliotakiwa kujieleza walikiuka maagizo ya chama kuwataka wajitenge kwa siku 14.

Ikumbukwe kuwa KUB hatoi maagizo ya chama bali anatoa maagizo ya kambi rasmi ya upinzani bungeni.
Wabunge wanaoendelea kuhudhuria bungeni hawajakiuka maagizo yoyote ya chama bali wameshindwa kukubaliana na kiongozi wao wa kambi na wanapaswa kuchukuliwa hatua kwa mujibu wa taratibu za kambi ambazo zipo kwa mujibu wa kanuni za bunge iwapo kweli wamefanya makosa.

Ni vema Mbowe akafahamu ipo tofauti ya MSINGI kabisa kati ya yeye kuwa KUB na yeye huyo huyo kuwa Mwenyekiti wa Chadema.

Mungu awape wepesi makamanda.

Maendeleo hayana vyama!
Mbowe hajafukuza mbunge, ni CHADEMA ndio wamechukua hatua stahiki kabisa za kinidhamu. Hata mimi kwenye jimbo langu nafurahi kwamba sasa tunamtafuta mbunge mpya sio aliyekuwepo.
 
Wamefuata utaratibu wa kufukuza?!
 
Wamefuata utaratibu wa kufukuza?!
Una taka wafuate utaratibu gani? Selasini na Komu walishasema ubunge ukikoma wanaenda NCCR chadema wakaheshimu maamuzi yao. Sasa je nisahihi kuendelea kukishambulia chama ambacho kilipa lidhaa ya kugombea na kupata nafasi za ubunge?

Rwakatare kasema anastafuu kwahiyo atakuwa benchi chama kikasema ok. Anakujaja na Selasini za Mapinduzi kumpindua KUB je nisawa?

Silinde binafsi naona kama hajielewi na ama anatumika maana kitendotu cha kulihama jimbo la Momba na kumfuata mwenzie Aonga Tunduma wenye akili ndefu alishajua ninikitafuata. Kwahuyu Mimi nasema muda utaongea maana dogo amepewa Platform kashajiona nayeye kidume lakini sawa nikidume.

Wengine wameambiwa wajieleze kwania njema kabisa.
Hebu sasa tueleze kwa hoja hizo halo Fanya wewe ndiye mwenyekiti ungefanyaje?

Siasa za nnchi hii kwasasa zimekuwa kama uadui especially kwa watu kama wewe amabo naweza sema hata hamueleweki mnataka nini. Siku hawa walioko madarakani wakiondoka nyinyi ndiyo mtakuwa wanangaji wao wakubwa.
Jamani tulisaidieni hili Taifa tunapotea sana tena sana kama Taifa.
 
Hujui bungeni kuna vikao vya kivyama ambavyo huwa na msimamo mmoja katika shughuli zote za bunge hasa panapokuwa na issue kubwa? Au ulitaka wakuonyeshe ili ujue?

Hata CCM kubaki kwako ni kwa sababu ya mahitaji ya chama ila kuna wengi walihitaji quarantine ya siku 14 ila chama kikaopt wabaki.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom