Yawezekana serikali ikajitoa kwenye kesi ya Lissu kabla ya Mei 19

fazili

JF-Expert Member
Joined
Jun 10, 2011
Posts
17,994
Reaction score
24,902
Haitakuwa jambo la kushangaza kuona serkali ikisema haina nia ya kuendelea na kesi ya uhaini inayomkabili mwenyekiti wa Chadema Tundu Lissu.

Sababu ni kwamba inavyoonekana upande wa mashtaka unapata shida kuja na vielelezo vya kutosha kumshtaki Lissu kwa kosa la uhaini.

Lissu ni mbobevu wa sheria na ni vigumu kumshinda katika mazingira ya uwazi na haki.

Ukijumlisha na hofu itakayofuatiwa na aibu ya kushindwa na serkali kuonekana inafanya uonevu dhidi ya upinzani, kuna uwezekano mkubwa kabla ya siku iliyopangwa kusikilizwa kesi serkali ikaghairi nia yake ya kuendelea na kesi hiyo.
 
Ni bora wakamuachia tu maana mashinikizo kutoka nje nayo yanazidi kutokea
 
Ni aibu sana chama cha ccm kukosa mtu wa kumdhibiti Lissu kwa hoja 😁😁😁😁 ccm bure kabisa
 
Laana hiyo ya uonevu itakuwa juu yao na watoto wao, Mungu hadhihakiwi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…