Jagina
JF-Expert Member
- Jan 29, 2019
- 8,428
- 4,022
Narudia Tena YESU Aliposema Yeye ni MUNGU!
๐๐
John 14:8-9
[8]Filipo akamwambia, Bwana, utuonyeshe Baba, yatutosha.
[9]Yesu akamwambia, Mimi nimekuwapo pamoja nanyi siku hizi zote, wewe usinijue, Filipo? Aliyeniona mimi amemwona Baba; basi wewe wasemaje, Utuonyeshe Baba?
muham mad aka allah naye anakubali YESU ni NENO NA ROHO YA MWENYEZI MUNGU!
Sasa nitajie Mtume au Nabii Aliyetambulishwa Kwa Watu Kuwa yeye ni NENO NA ROHO YA MWENYEZI MUNGU ๐ค
๐๐
: ุฅูุฐู ููุงููุชู ุงููู ูููุงุฆูููุฉู ููุง ู ูุฑูููู ู ุฅูููู ุงูููููู ููุจูุดููุฑููู ุจูููููู ูุฉู ู ูููููู ุงุณูู ููู ุงููู ูุณููุญู ุนููุณูู ุงุจููู ู ูุฑูููู ู ููุฌููููุง ููู ุงูุฏููููููุง ููุงููุขุฎูุฑูุฉู ููู ููู ุงููู ูููุฑููุจูููู
(AL I'MRAN - 45)
Na pale Malaika walipo sema: Ewe Maryamu! Hakika Mwenyezi Mungu anakubashiria. kwa neno litokalo kwake. Jina lake ni Masihi Isa mwana wa Maryamu, mwenye hishima katika dunia na Akhera, na miongoni mwa walio karibishwa.
"Aliyeniona mimi amemwona baba."
Wacha tuangalie muktadha: ( context ).
โFilipo akamwambia, Bwana, tuonyeshe Baba, nasi yatutosha. Baba; nawe wasemaje basi, Utuonyeshe Baba?
Yohana 14:8-9
Filipo alitaka kumwona Mungu kwa macho yake mwenyewe, lakini hii haiwezekani kwa kuwa hakuna mtu anayeweza kufanya hivyo. Biblia inasema:
"Hakuna mtu aliyemwona Mungu wakati wowote,"
Yohana 1:18
"Hakuna mtu aliyemwona Mungu wakati wowote,"
1 Yohana 4:12
"Na Baba mwenyewe aliyenipeleka amenishuhudia. Sauti yake hamkuisikia wakati wo wote, wala sura yake hamjaiona."
Yohana 5:37
Lakini walikuwa wakisikiliza sauti ya Yesu na kumtazama akiwa amesimama mbele yao! Yesu alikuwa anatuambia tu kwamba matendo yake mwenyewe na miujiza inapaswa kuwa uthibitisho wa kutosha wa kuwepo kwa Mungu bila Mungu kushuka kimwili na kujiruhusu kuonekana . Hii ni sawa na kwa mfano:
1)Yohana 8:19: "Wakamwambia, Baba yako yuko wapi? Yesu akajibu, Ninyi hamnijui mimi wala Baba yangu; kama mngalinijua mimi, mngalimjua na Baba yangu."
2)Yohana 12:44 "Yesu akapaza sauti, akasema, Yeye aniaminiye mimi, haniamini mimi, bali yeye aliyenipeleka."
3)Yohana 15:23 "Yeye anichukiaye mimi anamchukia na Baba yangu."
4)Mathayo 10:40-41 "Awapokeaye ninyi, anipokea mimi (Yesu), naye anipokeaye mimi, ampokea yeye aliyenituma. Ampokeaye nabii kwa kuwa ni nabii, atapata thawabu ya nabii; ampokeaye mwenye haki kwa kuwa ni mwenye haki, atapata thawabu ya mwenye haki."