Na mtindo maarufu wa nywele kwa vijana ulikuwa ni Punk! Umenifanya nianze kupekua makabrasha ya picha zangu za enzi hizo. Niliweka punk kama ile ya Shabba Ranks na nilijulikana kwa jina hilo kunako maeneo yangu... Weweeee!! Acha hiyo maneno. Nilikuwa natoka kijijini naenda mjini (wilayani)mwendo wa miguu takriban 30km! kulikuwa na fundi mmoja matata alikuwa anaweza kunyoa hiyo kitu kama ya Shabba Ranks tena kwa mkasi na wembe Topaz! Ukimwi ulikuwa ndo kwanza unaingia mijini. Vijijini habari hatuna, tunakula maini kiulaiiini...!