Afisa mwandamizi wa Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Ansarullah ya Yemen amesema vikosi vya jeshi la nchi hiyo vipo tayari kuingia katika makabiliano ya kijeshi na Marekani iwapo hali ya taharuki itashtadi katika Bahari Nyekundu.
Mohammad al-Bakhiti, mwanachama wa ngazi ya juu wa Ofisi ya Kisiasa ya Ansarullah alisema hayo jana usiku na kuongeza kuwa, "Ujumbe wetu kwa maadui ni kwamba, vikosi vya ulinzi vya Yemen vina hamu ya kupambana hasa na adui mkuu, Marekani."
Ameeleza bayana kuwa, kama ambavyo Yemen iliibuka mshindi katika 'vita vya kimaadili' dhidi ya muungano vamizi wa Marekani, ndivyo itakavyoshinda makabaliano yoyote ya kijeshi iwapo itashambuliwa.
Afisa huyo mwandamizi wa Ansarullah ya Yemen amebainisha kuwa: Iwapo manowari za Marekani zitaishambulia Yemen, (Wamarekani) watalengwa moja kwa moja, na wenyewe wanafahamu uzito wa uamuzi huo.
Vikosi vya ulinzi vya Yemen vimeapa kuendeleza mashambulizi yao hadi pale utawala katili wa Israel utakaposimamisha vita na kuondoa mzingiro ambao umeuwekea Ukanda wa Gaza kwa takriban miaka 17 sasa.