Mwandishi wa vitabu na mwanasiasa nchini, Yericko Nyerere usiku wa kuamkia leo ameshinda tuzo mbili, ikiwemo ya mwandishi bora wa vitabu Afrika.
Yericko ameshinda tuzo hizo zinazojulikana kama Zikomo Awards katika vipengele vya mwandishi bora wa vitabu Afrika na kiongozi bora wa kijamii.
Tuzo hizo zimefanyika usiku wa Novemba 30, 2024 nchini Afrika Kusini.
Kwa mujibu wa tovuti ya tuzo hizo, ili uingie katika kinyang’anyiro cha mwandishi bora wa vitabu ni lazima uwe umechapisha vitabu vinavyojulikana kwa ubora wake wa kiufundi, maudhui yanayoelimisha au kuburudisha, na mchango wake katika jamii.
Mbali na hayo, waandishi wanapaswa kuwa na rekodi ya kazi zenye mchango kwa jamii kwa njia chanya.
Katika kipengele cha kiongozi bora wa jamii, sifa inayotazamwa ni mshiriki kuonyesha juhudi zake katika kuboresha maisha ya watu wengine, kwa mfano kupitia miradi ya elimu, afya, au ujasiriamali.
Pia, uongozi wake unapaswa kuwa na athari chanya kwa watu wa rika mbalimbali, na anapaswa kuwa mfano wa kuigwa katika jitihada za kuboresha maisha ya watu wake.
Chanzo Gazeti la Mwananchi
#mwananchiupdates
Pia, soma:
-https://www.jamiiforums.com/threads/yericko-nyerere-ashinda-tuzo-ya-mwandishi-bora-wa-vitabu-afrika-2024.2241965/
- Yericko Nyerere ashinda tuzo ya mwandishi bora wa vitabu Afrika 2024