YES Tunahitaji Apartments Tanzania Lakini si kila Mkoa

WhAt about social services??

Social services like schools, hospitals, police, shops, roads, electricity, water, sewage systems, disabled accessibility ....
determines the feasibility of building an apartment complex. Ni bora ujenge Mbeya mjini au rent Mbeya mjini kuliko kuwa na nyumba yako Chunya... People rent to have access to these type of things.

Tutabadilika tu kimawazo, nyumba si kihivyo sana kama mnavyofikiria.
 
Hoja yako ni nzuri mkuu, tatizo ni wangapi wenye uwezo wa kulipa laki 8 kwa mwezi?

Niamini mkuu,

wapo....

Hata hivyo mkiwa mke na mume mnaishi Tegeta Kibaoni, mnafanya kazi posta na mnaendesha Toyota Harrier, engine 3000cc,,mafuta mnayotumia kwa mwezi kwenda na kurudi posta tu ni around TZS 600,000 kwa mwezi..Na hapo ukute mmepanga nyumba nzima na mnalipa laki 3 kwa mwezi...kwa hivyo jumla inawatoka TZS 900,000 kwa mwezi.

Wahindi wanapanga hizo appartment mjini, hawapotezi muda kwenye foleni na wanatembea kwenda ofisini..kupanga mjini kungekuwa economically unprofitable wahindi wasingekaa mjini, I swear...nawajua hawa watu, hakuna watu bahili duniani kama wahindi.
 
Kipi sio kweli sasa ndugu yangu,
Embu jibu ki-jf nikupe ufafanuzi.

Sasa mkuu mimi ninakaa Salasala na ninafanya kazi IPTL nina nyumba vyumba viwili na sebule, ninatumia miguu yangu kwenda kazini na watoto wangu wanasoma Wazo shule ya msingi ni gharama kuliko wewe unaekaa apartment ya huko posta na unafanya kazi Shelys pharmaceuticals Mwenge? Na watoto wako wanasoma Mwenge au Makini primary kule Africana?
 
Niamini mkuu,

wapo....

Hata hivyo mkiwa mke na mume mnaishi Tegeta Kibaoni, mnafanya kazi posta na mnaendesha Toyota Harrier, engine 3000cc,,mafuta mnayotumia kwa mwezi kwenda na kurudi posta tu ni around TZS 600,000 kwa mwezi..Na hapo ukute mmepanga nyumba nzima na mnalipa laki 3 kwa mwezi...kwa hivyo jumla inawatoka TZS 900,000 kwa mwezi.

Wahindi wanapanga hizo appartment mjini, hawapotezi muda kwenye foleni na wanatembea kwenda ofisini..kupanga mjini kungekuwa economically unprofitable wahindi wasingekaa mjini, I swear...nawajua hawa watu, hakuna watu bahili duniani kama wahindi.

Nimeshakupata mkuu, ila bado narudi pale pale, hilo kundi lahao watu lipo lakini ni dogo sana.
 
Hapo ndipo unapokosea.

Unadhani mtu anaponunua nyumba na kuipangisha engo lake ni pesa irudi. unfortunately kwa nyumba hali halisi ni tofauti. Mtu anayetaka biashara ya kuona pesa yake inarudi hawezi kufanya biashara ya kupangisha nyumba na kukusanya kodi za mwezi.

Watu wanaofanya biashara ya nyumba za kupangisha wengi ni watu wanaotaka regular source of income ambayo haina head ache. At the same thamani ya nyumba mara nyingi hupanda na hivyo kumfanya mwenye nyumba kuwa na faida kwa kuimiliki tu ile nyumba.

Mara nyingi utasikia mzee anasema "hii nyumba italipia ada za watoto". The same applies to appartments, mtu akinunua appartmen kwa sh. mil 50 akaipangisha kwa sh. laki moja na nusu haimaanishi kwamba anataka baadae ile mil. 50 yake irudi noooooo. Anachotaka yeye ni kuihifadhi ile mil. 50 katika mazingira salama zaidi kuliko kuiweka bank in terms of cash with limited interest.

Ardhi siku hizi hata mikoani bei ghali. tembelea jukwaa la matangazo madogo utaona watu wanatangaza viwanja Dodoma na kwingineko kwa bei gani.

Ni forces za demand and supply, wacha investors wajenge halafu wanunuzi waonyeshe kama nyumba hizo zinahitajika au hazihitajiki. General knowledge ni kwamba katika mji wowote ule hakuna aina nyumba isiyohitajika.

Na wewe Great Thinker unasupport hiyo hali ya kununua tu bila kuangalia return on investment? Hapa ndio inabidi tubadilike Watanzania? Unatambua kwa,ba nyumba ni investment? Tuachane na hiyo traditional behaviour eti nyumba itanisaidia kulipa ada ya watoto! Tuachane na tabia za kuzika pesa zetu kwa kununua tu nyumba bila malengo ya maendeleo! Hali hii inatufanya wengi tuendelee kuwa masikini baada ya kufikiria kijasiriamali zaidi, we just sink the money!
 
WhAt about social services??

Social services like schools, hospitals, police, shops, roads, electricity, water, sewage systems, disabled accessibility ....
determines the feasibility of building an apartment complex. Ni bora ujenge Mbeya mjini au rent Mbeya mjini kuliko kuwa na nyumba yako Chunya... People rent to have access to these type of things.

Tutabadilika tu kimawazo, nyumba si kihivyo sana kama mnavyofikiria.

You argument holds water but too academic! WHY? Ndio maana hata heading yangu nikasema, yes we need apartments but not in every region! Need analysis ni muhimu mkuu! Haya maisha ya kuishi kwenye gated community yanahitaji gradual changes, taking into account the cultural trend
 
  • Thanks
Reactions: dig
Sasa mkuu mimi ninakaa Salasala na ninafanya kazi IPTL nina nyumba vyumba viwili na sebule, ninatumia miguu yangu kwenda kazini na watoto wangu wanasoma Wazo shule ya msingi ni gharama kuliko wewe unaekaa apartment ya huko posta na unafanya kazi Shelys pharmaceuticals Mwenge? Na watoto wako wanasoma Mwenge au Makini primary kule Africana?

Haya sasa, ona tumepishania Moroco wewe unaenda Posta mie naenda Mwenge....halafu unadhani tuko pamoja.

Nilikuwa nazungumzia idea zaidi....kuwa kwa yeyote anayefanya kazi mjini, ni faida zaidi ki-economiki na hata ki-biologia kwa yeye kukaa mjini.,.kuliko huko 'nje kidogo' ya Jiji la Daslam...upo?!?

Twende kazi.
 
Nimeshakupata mkuu, ila bado narudi pale pale, hilo kundi lahao watu lipo lakini ni dogo sana.

lol..
Siku hizi private sector milioni 3 mshahara ni kima cha chini unajua....
Halafu kama laki 8 inaonekana kubwa basi tuifikirie kama 400,000 ya mke na 400,000 ya mume.
At the end of the day kama mnatumia gari..lazima mtakuwa mnakaribia huko huko tu., kibaya zaidi mnachokea kwenye mafoleni.
 
Haya sasa, ona tumepishania Moroco wewe unaenda Posta mie naenda Mwenge....halafu unadhani tuko pamoja.

Nilikuwa nazungumzia idea zaidi....kuwa kwa yeyote anayefanya kazi mjini, ni faida zaidi ki-economiki na hata ki-biologia kwa yeye kukaa mjini.,.kuliko huko 'nje kidogo' ya Jiji la Daslam...upo?!?

Twende kazi.
Hukuweka assumptions yoyote mkuu na ndio maana nikakwambia Si kweli!, Hayo ya kila mtu kufanya kazi mjini umeyasema sasa hivi tu
 
Usiwe na hasira mkuu,
Embu nieleweshe ni kipi sikuelewa. Manake kiingereza sio lugha ya mama wajua.

Samahani mkuu Prisoner 46664 kama maelezo yangu yamekaa kihasira!
Tukirudi kwenye hoja, heading ya thready yangy tu yenyewe inasema [h=2]"YES Tunahitaji Apartments Tanzania Lakini si kila Mkoa"[/h]Kwa hiyo mimi sijapinga apartment zisijengwe, na ndio maana ninaomba urudie kuisoma vizuri kwani hoja yako imejikita katika muktadha wa kusema apartment zinalipa hasa DSM, yes, kama zinalipa DSM, na kIgoma zinalipa the same?
 
Hukuweka assumptions yoyote mkuu na ndio maana nikakwambia Si kweli!, Hayo ya kila mtu kufanya kazi mjini umeyasema sasa hivi tu

Haya basi,tufanye nimeweka hiyo assumption..argument yangu ni kweli au si kweli?
 
You argument holds water but too academic! WHY? Ndio maana hata heading yangu nikasema, yes we need apartments but not in every region! Need analysis ni muhimu mkuu! Haya maisha ya kuishi kwenye gated community yanahitaji gradual changes, taking into account the cultural trend
Kwenye market economy, cultural trend is determined by the seller, not the buyer.

I'm short-changed and the banks in Tanzania got some crazy rates!, otherwise, ningependa sana niwe na condo bongo. Nyumba zetu za uswazi hazilipi kabisa!! ... majalala na vibaka, hata ukitaka kukodisha ni milioni moja kwa mwaka. Yaani mtu anaweza akakupa milioni 50, akaishi mpaka kifo chake. ... What a joke!!
 
Ni katika hiyo hiyo market economy ambapo kuna survival for the fittest! Ni katika hiyo hiyo market economy ambapo kuna classes, low income, middle class and upper! Sasa unapongelea habari za uswazi una refer group ipi na je ni nani unahisi wateja wa hizo apartment? Hata hivyo mimi bado sina pingamizi na investment ya apartments kwa jiji kama DSM kama uliielewa vizuri thread yangu
 
Samahani mkuu Prisoner 46664 kama maelezo yangu yamekaa kihasira!
Tukirudi kwenye hoja, heading ya thready yangy tu yenyewe inasema "YES Tunahitaji Apartments Tanzania Lakini si kila Mkoa"

Kwa hiyo mimi sijapinga apartment zisijengwe, na ndio maana ninaomba urudie kuisoma vizuri kwani hoja yako imejikita katika muktadha wa kusema apartment zinalipa hasa DSM, yes, kama zinalipa DSM, na kIgoma zinalipa the same?

Bila shaka ExpertBroker...
Kama ishu ni apartment kulipa mikoa mingine kama zinavyolipa hapa Dar,..mimi nadhani hilo ni suala la Demand and supply tu..at any point in time, Demand ikiwa imezidi supply, lazima apartments zitakuwa zinalipa sana kwa wamiliki wake kwa sababu wataweza kujichagulia rents watakazo.

Lazima tukubali kuwa pamoja na culture yetu kuwa ya kupenda kukaa kwenye nyumba zetu wenyewe, kuna watu wachache kati yetu ambao wanapenda kukaa kwenye apartments (sio wengi)..kwa hivyo at any point in time, mji wowote unaokua kiuchumi, kutakuwa na mahitaji ya apartments.

Kitu cha msingi ni kwa yeyote mwenye lengo la kujenga apartment at a given point in time (hii ina-apply hata hapa Dar es Salaam) kufanya assessment ya Demand na Supply ili kujua kama kuna faida..lakini sidhani kama ni sahihi kwa sisi kutengeneza general rule.

Halafu pia kuna suala la miji kukua...mji kama Arusha, mwaka 2005 kitu kinachoitwa foleni ilikuwa ni hadithi kabisa. Sasa hivi foleni za magari barabarani zimeanza kuwa tatizo almost kama Dar..kwa hivyo kwa assumption yangu ya kuwa watu (especially elites) watachagua kupanga kwenye apartments kuliko kujenga nje ya mji..itazidi kuwa viable.

Anyways...Demand vs Supply.
 
Last edited by a moderator:
Ni katika hiyo hiyo market economy ambapo kuna survival for the fittest! Ni katika hiyo hiyo market economy ambapo kuna classes, low income, middle class and upper! Sasa unapongelea habari za uswazi una refer group ipi na je ni nani unahisi wateja wa hizo apartment? Hata hivyo mimi bado sina pingamizi na investment ya apartments kwa jiji kama DSM kama uliielewa vizuri thread yangu
Nimeielewa vizuri hoja yako, ila wewe hujaielewa yangu.

Kwa kifupi, apartments are marketable in TZ nowadays, hata mikoani.... Huwezi mfananisha mwenye condo Arusha mjini na mwenye nyumba ya vyumba sita yombo.
 
Na wewe Great Thinker unasupport hiyo hali ya kununua tu bila kuangalia return on investment? Hapa ndio inabidi tubadilike Watanzania? Unatambua kwa,ba nyumba ni investment? Tuachane na hiyo traditional behaviour eti nyumba itanisaidia kulipa ada ya watoto! Tuachane na tabia za kuzika pesa zetu kwa kununua tu nyumba bila malengo ya maendeleo! Hali hii inatufanya wengi tuendelee kuwa masikini baada ya kufikiria kijasiriamali zaidi, we just sink the money!

Sasa hapo unakuwa unawafundisha watu nini wanahitaji. Kwenye jamii kuna aina zote za watu. Huwezi kutaka kila mtu awe mfanyabiashara. hakuna jamii ya namna hiyo duniani. Pesa kila mtu anaipa nafasi anayoona yeye kwenye maisha yake.

Si sahihi kusema kwa sababu unataka kila mtu awe anafikria kurudisha pesa yake tu basi nyumba za namna fulani hazifai kujengwa mijini. Thats not right!

Kuna mtu unakuta ana akiba bank sh. mil. 250. Hivi mtu huyu akichukua mil. 50 akanunua appartment mjini ili kudiversify jinsi anavyotunza pesa zake kuna ubaya gani? Hivi hujui kuwa kuna watu wananunua dhahabu na kutunza kama njia ya kuhifadhi pesa? Kwani dhahabu inawarudishia nini? Its just a way of making sure that your money retains the same value over time. Hivyohivyo kununua appartment, pesa inakuwa na value inayoongezeka mwaka mpaka mwaka and at the same time inakuletea kipato kidogokidogo in terms of kodi.

Mwingine anaweza kuwa anakaa ughaibuni na anataka kuweka kitu nyumbani ambacho hakitahitaji usimamizi mkubwa na kiweze kumfaa siku akirudi Bongo. Kununua appartment kwake ni more convinient kwa sababu hana haja ya kuingia gharama za ulinzi etc.

Katika kiwanja cha sq. m 1000 mtu anaweza kujenga appartments zaidi ya 30. lakini ukimwambia ajenge nyumba 30 solitary atahitaji angalau sq. m 12000. That is 12 times more investment on land space alone! Ukichukulia na the fact kwamba appartments zinashare kuta utagundua kuinvest kwenye nyumba solitary ni gharama kubwa zaidi kuliko kujenga appartments hasahasa ukiongeza gharama za usimamizi, installation ya umeme, maji, kuweka pavements, ulinzi etc.
 
Bila shaka ExpertBroker...
Kama ishu ni apartment kulipa mikoa mingine kama zinavyolipa hapa Dar,..mimi nadhani hilo ni suala la Demand and supply tu..at any point in time, Demand ikiwa imezidi supply, lazima apartments zitakuwa zinalipa sana kwa wamiliki wake kwa sababu wataweza kujichagulia rents watakazo.

Lazima tukubali kuwa pamoja na culture yetu kuwa ya kupenda kukaa kwenye nyumba zetu wenyewe, kuna watu wachache kati yetu ambao wanapenda kukaa kwenye apartments (sio wengi)..kwa hivyo at any point in time, mji wowote unaokua kiuchumi, kutakuwa na mahitaji ya apartments.

Kitu cha msingi ni kwa yeyote mwenye lengo la kujenga apartment at a given point in time (hii ina-apply hata hapa Dar es Salaam) kufanya assessment ya Demand na Supply ili kujua kama kuna faida..lakini sidhani kama ni sahihi kwa sisi kutengeneza general rule.

Halafu pia kuna suala la miji kukua...mji kama Arusha, mwaka 2005 kitu kinachoitwa foleni ilikuwa ni hadithi kabisa. Sasa hivi foleni za magari barabarani zimeanza kuwa tatizo almost kama Dar..kwa hivyo kwa assumption yangu ya kuwa watu (especially elites) watachagua kupanga kwenye apartments kuliko kujenga nje ya mji..itazidi kuwa viable.

Anyways...Demand vs Supply.

Mimi nafikiri mkuu Prisoner 46664, tunaongelea kitu kilekile ila katika mlengo tofauti! Ieleweke kwamba mimi sipingi investment katika apartment blocks!
 
Nimeielewa vizuri hoja yako, ila wewe hujaielewa yangu.

Kwa kifupi, apartments are marketable in TZ nowadays, hata mikoani.... Huwezi mfananisha mwenye condo Arusha mjini na mwenye nyumba ya vyumba sita yombo.

Mkuu, nilijitahidi kuifupisha sama hoja yangu nikifikiri itaeleweka! Anyway, suala la property market value kote duniani linategemea vitu vitatu, LOCATION, LOCATION and LOCATION! Hivyo sidhani katika hoja yangu nilijaribu kulinganisha eti condominium property ya Arusha(japo hujasema Arusha location ipi, maana si kila sehemu ni prime Arusha) ni sawa na nyumba ya vyumba sita Yombo!
 
Na wewe Great Thinker unasupport hiyo hali ya kununua tu bila kuangalia return on investment? Hapa ndio inabidi tubadilike Watanzania? Unatambua kwa,ba nyumba ni investment? Tuachane na hiyo traditional behaviour eti nyumba itanisaidia kulipa ada ya watoto! Tuachane na tabia za kuzika pesa zetu kwa kununua tu nyumba bila malengo ya maendeleo! Hali hii inatufanya wengi tuendelee kuwa masikini baada ya kufikiria kijasiriamali zaidi, we just sink the money!

Vile vile suala la uhaba wa ardhi ,maeneo ya mikoani isiwe kigezo cha kuacha kufikiria njia bora zaidi za namna ya kutumia ardhi kwa ajili ya shughuli za kiuchumi.

Huko tunapopaita mikoani ni kweli maeneo yapo na yanazidi kupanda bei, achilia mahekar yaliyoshikiliwa na wakubwa, kwa upande mwingine naona kama pangekua na sera nzuri, tungeweza kuhimiza apartments kwa lengo la kupata ardhi zaidi kwa ajili ya kukuuza uchumi.

Mfano mdogo ni Zanzibar, kama sio yale maghorofa ya mzee Karume, unafikiri ni eneo kiasi gani lingechukua idadi ya watu wanaoishi kwenye hayo maghorofa?

Cha msingi sio kuiga kila kitu, tuangalie mahitaji, mazingira, na zaidi kama kuna tija kwa tunachotaka kukifanya. Hakuna suluhu moja iliyo sahihi kwa matatizo yote.
 
Sasa hapo unakuwa unawafundisha watu nini wanahitaji. Kwenye jamii kuna aina zote za watu. Huwezi kutaka kila mtu awe mfanyabiashara. hakuna jamii ya namna hiyo duniani. Pesa kila mtu anaipa nafasi anayoona yeye kwenye maisha yake.

Si sahihi kusema kwa sababu unataka kila mtu awe anafikria kurudisha pesa yake tu basi nyumba za namna fulani hazifai kujengwa mijini. Thats not right!

Kuna mtu unakuta ana akiba bank sh. mil. 250. Hivi mtu huyu akichukua mil. 50 akanunua appartment mjini ili kudiversify jinsi anavyotunza pesa zake kuna ubaya gani? Hivi hujui kuwa kuna watu wananunua dhahabu na kutunza kama njia ya kuhifadhi pesa? Kwani dhahabu inawarudishia nini? Its just a way of making sure that your money retains the same value over time. Hivyohivyo kununua appartment, pesa inakuwa na value inayoongezeka mwaka mpaka mwaka and at the same time inakuletea kipato kidogokidogo in terms of kodi.

Mwingine anaweza kuwa anakaa ughaibuni na anataka kuweka kitu nyumbani ambacho hakitahitaji usimamizi mkubwa na kiweze kumfaa siku akirudi Bongo. Kununua appartment kwake ni more convinient kwa sababu hana haja ya kuingia gharama za ulinzi etc.

Katika kiwanja cha sq. m 1000 mtu anaweza kujenga appartments zaidi ya 30. lakini ukimwambia ajenge nyumba 30 solitary atahitaji angalau sq. m 12000. That is 12 times more investment on land space alone! Ukichukulia na the fact kwamba appartments zinashare kuta utagundua kuinvest kwenye nyumba solitary ni gharama kubwa zaidi kuliko kujenga appartments hasahasa ukiongeza gharama za usimamizi, installation ya umeme, maji, kuweka pavements, ulinzi etc.

Nafikiri hutujaelewana ZeMarcopolo, labda kama unataka kila post nitoe ufafanuzi kwa kina! Unaongelea asilimia ngapi ya watanzania katika hoja yako! Katika research mara nyingi huwa tunafikia hitimisho pale ambapo zaidi ya asilimia 50 imelenga kwenye hoja/kitu husika! First home buyers wengi wanajinyima na kuishi maisha duni ati alimradi ajenge nyumba! Unaweza hata somesha wanao best school kuliko kuchukua pesa na kuzika eti kisa unamiliki nyumba ambapo utakuta nyumba yenye haina hata hati, limited appreciation na not mortgageable! Usisahau zaidi ya asilimia 75 kwa jiji la DSM bado ni unplanned! Na ieleweke kwamba si vibaya kujenga nyumba but how right is the decision to put up(invest) a house is right? Unaweza usiite biashara kwa sababu ya uhaba wa maneno katika kiswahili lakini building a home is an investment!
 
Back
Top Bottom