Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 28,297
- 68,017
YESU ALIKUNYWA NA KULA NA WALEVI NA WAHUNI; JE Rais SAMIA ANATUMIA FALSAFA HII?
Kwa Mkono wa Robert Heriel.
Nikiuangalia utawala wa Mama Samia Suluhu ninajikuta nikikumbuka Kisa cha Yesu wa Nazareth.
Yesu wa Nazareth moja ya falsafa yake ni kuchangamana na Wale wanaotofautiana naye kiitikadi, kiimani, kimitindo ya maisha, wakosoaji wake, na Wale ambao walionekana ni hatari kubwa.
Kwa mujibu wa maandiko Yesu Hakuwa na dhambi.
Hakuwa mlevi Ila alikaa na walevi,
Hakuwa Mhuni lakini alipenda kukaa na wahuni.
Hakuwa mlafi lakini alipenda kukaa wa walafi.
Hakuwa na dhambi lakini alipenda kukaa na wenye dhambi.
Hakuwa mnyonge lakini alipenda kukaa na wanyonge.
Hakuwa mchafu lakini alipenda kukaa na wachafu.
Ndio maana moja ya kashfa zake alizokuwa akipewa na Mafarisayo ni Kukaa vijiweni na wahuni, wenye dhambi.
Watakatifu alikuwa akikutana nao huenda Kwa wiki mara moja tena akipenda Hekaluni au Kwenye visinagogi kusali.
Hata hivyo ukimuuliza sababu; Majibu yake alisema Hakuja Kwa sababu ya watakatifu isipokuwa wenye dhambi. Kusema; wenye Afya hawahitaji Tabibu. Hiyo ndio sababu kuu.
Mama Samia utawala wake kidogo unafanana na Utawala wa Kikwete ambao unatumia Falsafa hiyo ya Kukaa na wenye mtizamo tofauti na wewe.
Sio ajabu Mama Samia akihamasisha watu wamkosoe ukilinganisha na viongozi wenye mfumo wa Kifarisayo Kama JPM ambaye hataki kukaa meza moja na watu wenye mtazamo tofauti na yeye.
Mama Samia anajua wazi kabisa Kama ilivyo Kwa watu wote wanaotumia Kanuni hiyo ya Yesu kuwa Adui yako muweke Karibu,
Anajua kuwa wenye mtizamo tofauti kikawaida wanakuwa na akili ya ziada ukilinganisha na Wale mnaofanana Fikra.
Hata kwenye jamii watu wahuni, walevi, wajanja wajanja akili zao huwezi kuzilinganisha na watu wasio wahuni.
Falsafa ya Adui yako muweke Karibu, inamanufaa zaidi kuliko ya Mafarisayo ambayo hujitenga na kumuweka mbali Adui.
Kikawaida mtu yeyote anayekosoa sharti awe na akili inayochambua mambo, na kuona katika muono tofauti. Huwezi kuwa mkosoaji pasipo kuwa na Akili.
Yesu alikaa na waovu Kwa sababu wao ndio wangemfanya kuwa Masihi.
Yesu alikaa na Malaya Kwa sababu wao ndio wangemhudumia pale apatwapo na madhila, sio ajabu hata alivyosulubishwa walioenda Kusafisha mwili wake na kuupaka mafuta walikuwa ni Malaya ndiye Mariam Magdalena Yule Kahaba Mkuu; Wakati mafarisayo wakishangilia kifo cha Yesu,
Changamoto kubwa ya kumuweka Adui karibu ni kujua kufanya timing kwani ukizubaa unaweza kupigwa.
Mama Samia kuwa karibu na wapinzani ambao wanamtizamo tofauti na yeye, Kuwa karibu na Wafanyabiashara ambao kikawaida wengi hawapendi kulipa Kodi, kuwa karibu na Wafanyakazi Kwa kuwaongezea mishahara na kuwapandishia madaraja ni Jambo zuri Ila linalohitaji umakini mno.
Ukikaa na wahuni kijiweni sharti uwe smart usijevutishwa Sigara Kali au kusombwa na Askari wakija kukamata Wavuta bangi.
Ukikaa na wahuni lazima uwe makini wasije wakakugeuka na kuvamia nyumba yako wakakuibia.
Ila Jambo moja ambalo wahuni wengi wanalo ni kupendana. Na wengi wanajua kusaidiana.
Mama Samia kukaa karibu na watu wenye mtazamo tofauti na yeye ni Jambo zuri lakini linalohitaji umakini na tahadhari ya hali ya juu Sana.
Shida ya wahuni ukiona wanakusifia Sana, Anza kushtuka, maana hawachelewi kugongea Sigara au kuomba kete Kama sio kuomba uwazungushie Bia
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
0693322300
Mvomero