Father of All
JF-Expert Member
- Feb 26, 2012
- 7,672
- 9,039
Kwa waliosoma na kuelewa habari za Yesu watakubaliana nami yafuatayo:
Mosi, alikuwa maskini au lofa wa kawaida mwana wa seremala ambaye kama angerudi leo na kukuta wanaomhubiri na utajiri wao haramu, angezimia mbali na kuwakaripia hata kuwachapa.
Pili, hakuwahi kuwa na wala kuingia kanisani.
Tatu, aliingia kwenye masinagogi na kuhubiri humo.
Nne, aliacha wanafunzi na si wakristo.
Tano, hadi anaondoka, hakuwahi kusikia neno ukristo.
Sita, hakujitangaza kuwa alikuwa akitenda miujiza kama hawa majizi wa sasa wanaomtumia na kumsingizia.
Saba, alisema wazi kuwa alikuja kwa ajili ya kabila 12 za Israel ingawa tapeli Sauli baadaye Paulo alikuja na kugeuza kila kitu kiasi cha kuunda dhehebu ndani ya dhehebu.
Nane, hakupenda sifa wala ujiko kama haya majizi ya sasa yanayotumia runinga kuwaibia mazwazwa.
Tisa, hakuwahi kushirikiana na serikali kwa vile alijua uhovyo na uovu wake.
Kumi, hakuacha uislam ambao nao ulimdandia kujifanya unamtambua ili kuwanasa wakristo.
Kumi na moja, alipenda kukaa na watu wa tabaka la chini na siyo wakwasi na wenye madaraka.
Kumi na mbili, hauandika wala kuacha biblia.
Je wewe unasemaje?