Setfree
JF-Expert Member
- Dec 25, 2024
- 1,679
- 2,123
Kina nani hao? Amewaaibishaje? Ntakueleza, ngoja kidogo niwasaidie wale waliokimbia masomo ya sayansi, hasa hasa Fizikia. Ulimwengu wa kisayansi umejengwa juu ya sheria na kanuni zinazoelezea mienendo ya vitu. Miongoni mwa sheria/kanuni hizo ni:
Yesu alitembea juu ya maji – na kuvunja kanuni ya kuelea (Buoyancy)
Kulingana na kanuni hiyo ya Archimedes, ili mtu aweze kuelea, lazima nguvu ya msukumo iwe kubwa au sawa na uzito wake. Sasa kwa kuwa uzito wa mwanadamu ni mkubwa kuliko msukumo wa maji, haiwezekani mtu akatembea juu ya maji bila kuzama. Lakini Biblia inasema:
"...Saa nne usiku Yesu akawaendea, akitembea juu ya bahari." (Mathayo 14:25)
Kama tulivyoona, kisayansi mtu kutembea juu ya maji ni jambo lisilowezekana, lakini kwakuwa Yesu ni Mungu, hakuna linaloshindikana kwake.
Yesu alipaa mbinguni – na kuvunja Sheria ya Uvutano
Kulingana na Sheria ya Uvutano, Newton alieleza kwamba kitu chochote chenye uzito lazima kivutwe na mvuto wa dunia. Ndiyo maana mtu akiruka juu, lazima arudi chini.
Lakini Biblia inasema:
"Bwana Yesu, baada ya kusema nao, akachukuliwa juu mbinguni..." (Marko 16:19)
“Akiisha kusema hayo, wote wakiwa wanamtazama, akainuliwa, wingu likampokea kutoka machoni pao wasimwone tena.”(Matendo 1:9)
Yesu alipaa mbinguni bila kuvutwa na gravitational force! Tukio hili linathibitisha tena kuwa Yesu ni Mungu na yuko juu ya laws of nature. Wanasayansi wa kisasa wanahitaji makombora yenye nguvu nyingi kufanikisha safari za kwenda katika anga za juu, lakini Yesu alipaa kwa uwezo wake mwenyewe bila msaada wa makombora!
Kwa kuvunja sheria/kanuni hizi za kisayansi, Yesu anaonyesha kuwa Yeye hakuwa mwanadamu wa kawaida bali ni Mungu mwenye nguvu(Isaya 9:6).
Tumsifu Yesu Kristo. Milele Amina! 🙏🔥
- The Law of Universal Gravitation: Hii sheria inaelezwa na mwanasayansi mahiri Isaac Newton. Kwa maneno rahisi, sheria hii inasema kwamba kila kitu chenye uzito huvutwa kuelekea kwenye kitu kingine kwa nguvu ya uvutano.
- Archimedes' Principle: Kanuni hii inaelezwa na mwanasayansi Archimedes. Hii inasema kwamba kitu kinachoelea majini hupata msukumo unaolingana na uzito wa maji yaliyoachwa (displaced water).