Yesu Kubambikiwa alitakasa vyakula vyote ina maana alimkaidi Mungu alietuchagulia vya kula? Ni ruksa kula nzi, paka, mbwa, chura, kinyonga, nyoka?

NetMaster

JF-Expert Member
Joined
Sep 12, 2022
Posts
1,454
Reaction score
4,925
Mungu alishaweka sheria tule vyakula vifuatavyo

Wanyama - wawe wenye kwato + miguu ya kupasuka kati + mwenye kucheua

walioruhusiwa: Ng;ombe, mbuzi, kondoo, swala, nyati, n.k
wasioruhusiwa: Nguruwe, Kobe, punda, mbwa, nyau, panya, n.k.

Samaki - wawe na magamba + mapazi

walioruhusiwa: Kambale, dagaa, n.k.
Wasioruhusiwa: Pweza, Kasa, papa, kaa, chunusi, n.k.

Ndege:

Walioruhusiwa: kuku, bata mzinga, bata, njiwa, kanga, n.k.
wasioruhusiwa: Bundi, Popo, Kuguru, vulture, Mwewe, mbuni, n.k.

wadudu: wawe wana uwezo wa kuruka na wana miguu maalum kwajili ya kuruja

vilivyoruhusiwa: senene, nzige, senene, panzi n.k
visivyoruhusiwa: nzi, vipepeo, buibui, n.k.

Reptiles: hawa hawaruhusiwei kabisa kuliwa kuanzia kenge, chura, nyoka, konokono, n.k

Hata watu wanaokula baadhi ya visivyoruhusiwa huwa wanakula karibu vyote vilivyoruhusiwa kwa amani, iweje huko kwa ambavyo havijaruhusiwa wnachagua sana na vingi wanaona si sawa, mfanomtu anapenda nguruwe ila anaona nzi kwake si sawa ?

Kumbambikia Yesu kusafisha vyakula'

Yesu akiwa na wanafunzi wake waliokuwa na njaa walipopita sehemu ya mahindi walianza kuyachuma na kuyala bila kuosha mikono, kwa sheria za mafarisayo kula bila kunawa waliona kinachoingia kinamtia mtu unajisi, mafarisayo walipoanza kumbana Yesu ajieleze ndipo aliposema kwa mtu kufanya kinachonajisi ni kile kinachomtoka rohoni kinachomfanya atende dhambi na wala si kinachomuingia kwa kula bila kuosha mikono.

Kuna yale maneno ya kwenye mabano ya nyongeza kwamba kwa kusema hivi Yesu alivitakasa vyakula vyote, maneno yoyote ya kwenye mabano huwa ni mawazo binafsi ya watu wengine, hivyo Yesu hakuzungumzia lolote kuhusu kutakasa vyakula.

Tujiepushe na tukae mbali sana kwa vyakula ambavyo havikutakaswa, hivi wewe unaweza kula nzi, kupe, buibui, nyau, nk?
 
Kwa hakika lazima pawe na ukimya maana huko wanatafauta kila wawezacho lakini wanaona wazi kabisa si kila mnyama ni msafi.

Hivi kweli nzi asafishwe kuliwa, kenge asafishwe kuliwe, hadi nyau ?
 
Chura
Nyoka
Punda
Pig
Washawasha
Kumbilumbi
Panzi ndio senene

Wanlaiwa labda mazingira tu ndio tofauti Kuna watu wanakula hadi mbwa ndio ije kuwa nyau😀
 
Uandishi wa title za thread za aina hii umekithiri sana JF😀😀.Mtu anajiuliza swali ,anajibu mwenyewe,anatoa hoja mwenyewe alafu anataka watu wajibu kwenye direction anayotaka😂😂😂
 
Mtoa maada sio kila kitu kwaajili ya kila mtu
ni kweli, hata mapenzi ya jinsia tofauti si kwa kila mtu, mpo ambao mnaona ushoga ni sawa.

wacha wengne tuendelee kufuata maandiko takatifu
 
Hiyo biblia gani umeisoma?
Ndio tatizo la kukariri mistari hili bila kusoma kitabu kizima, utaskia mtu kakariri tu kamstari kale kwa kwenye kimuingiacho mtu hakitmtii unajisi bila hata kujua kilichopelekea mpaka kusema hivyo
 
Mungu alishaweka sheria tule vyakula vifuatavyo

Wanyama - wawe wenye kwato + miguu ya kupasuka kati + mwenye kucheua

walioruhusiwa: Ng;ombe, mbuzi, kondoo, swala, nyati, n.k
wasioruhusiwa: Nguruwe, Kobe, punda, mbwa, nyau, panya, n.k.

Samaki - wawe na magamba + mapazi

walioruhusiwa: Kambale, dagaa, n.k.
Wasioruhusiwa: Pweza, Kasa, papa, kaa, chunusi, n.k.

Ndege:

Walioruhusiwa: kuku, bata mzinga, bata, njiwa, kanga, n.k.
wasioruhusiwa: Bundi, Popo, Kuguru, vulture, Mwewe, mbuni, n.k.

wadudu: wawe wana uwezo wa kuruka na wana miguu maalum kwajili ya kuruja

vilivyoruhusiwa: senene, nzige, senene, panzi n.k
visivyoruhusiwa: nzi, vipepeo, buibui, n.k.

Reptiles: hawa hawaruhusiwei kabisa kuliwa kuanzia kenge, chura, nyoka, konokono, n.k

Hata watu wanaokula baadhi ya visivyoruhusiwa huwa wanakula karibu vyote vilivyoruhusiwa kwa amani, iweje huko kwa ambavyo havijaruhusiwa wnachagua sana na vingi wanaona si sawa, mfanomtu anapenda nguruwe ila anaona nzi kwake si sawa ?

Kumbambikia Yesu kusafisha vyakula'

Yesu akiwa na wanafunzi wake waliokuwa na njaa walipopita sehemu ya mahindi walianza kuyachuma na kuyala bila kuosha mikono, kwa sheria za mafarisayo kula bila kunawa waliona kinachoingia kinamtia mtu unajisi, mafarisayo walipoanza kumbana Yesu ajieleze ndipo aliposema kwa mtu kufanya kinachonajisi ni kile kinachomtoka rohoni kinachomfanya atende dhambi na wala si kinachomuingia kwa kula bila kuosha mikono.

Kuna yale maneno ya kwenye mabano ya nyongeza kwamba kwa kusema hivi Yesu alivitakasa vyakula vyote, maneno yoyote ya kwenye mabano huwa ni mawazo binafsi ya watu wengine, hivyo Yesu hakuzungumzia lolote kuhusu kutakasa vyakula.

Tujiepushe na tukae mbali sana kwa vyakula ambavyo havikutakaswa, hivi wewe unaweza kula nzi, kupe, buibui, nyau, nk?
Kambale ana magamba?? (Hapa umetoka Boko)

Tunakula hivi vyakula kwa kuwa ndio tamaduni zetu na ndivyo tulivyorithi toka vizazi na vizazi

Leo hii tungekua tunaishi china sisi tungekua tunakula kama wao Tu kila kitu chenye miguu kasoro meza na stuli tu
 
China ni waumini wa Budhism sio ukristo mkuu

anyway naona wewe mtaalam wa mambo ya samaki, nipe mifano ya samaki wenye magamba na mapezi nirekebishe au niongezee hapo
 
Kambale hana magamba wala mapezi,anaingia je kwenye list yako...
 
Kwani siku ya saba ya uumbaji Mungu alifanya nini?
 
China ni waumini wa Budhism sio ukristo mkuu

anyway naona wewe mtaalam wa mambo ya samaki, nipe mifano ya samaki wenye magamba na mapezi nirekebishe au niongezee hapo
Sio mtaalamu wa samaki lakini kambale nimeshakula sana. Ndio nimeshangaa uliposema Kambale ana Magamba

Sijagusa dini katika ufafanuzi wangu. Nimesema tunakula hivi kwa kuwa ndio timerithi hivyo. Hizi dini zimekuja zimetukuta na vyakula vyetu tayari.
 
There's an Adventist sign over here....
 
ni kweli, hata mapenzi ya jinsia tofauti si kwa kila mtu, mpo ambao mnaona ushoga ni sawa.

wacha wengne tuendelee kufuata maandiko takatifu
Hasa mkuu hapa ushoga unaingiaje!? Mkiambiwa mambo mengine mnayakuza wenyewe mnakuwa wabishi. Sawa wacha tukae kimya!
 
Yesu kristo mwana wa Mungu aliye hai, alikuja Ili watu wapate uhai na kuurithi ufalme wa Mungu, uhai wa kiroho
Dhambi ni ufu
Mwenye dhambi hatorithi ufalme wa Mungu, na hatofanyika kuwa mwana wa Mungu
Chakula chochote si dhambi
Chakula kibaya ni najisi, Kwa maana ya kuwa hakileti ladha njema, na usafi wa miili

Wayahudi walikazia fundisho LA chakula kana kwamba chakula kinamfanya mtu awe na dhambi

Yesu Kwa upendo wake, alitaka watu wake wapunguziwe mzigo wa Sheria zisizo na ulazima
Yesu alikazia matendo yenye kuleta usafi wa roho na si matendo ya usafi wa mwili

Yesu ni mwokozi wa ulimwengu
Usihofu Kwamba Yesu amekiuka taratibu iliyoasisiwa na Muumba, la hasha! Yote afanyayoYesu ni baada ya kupewa go ahead na Baba yake
Kumbuka Yesu alikuwa anaongea na Baba yake siku zote!
Je, hauwezi amini Yesu angeweza kumuomba Baba yake kutangua taratibu alizompangia mwanadamu?

Piga kitimoto Mzeebaba, utanishukuru!
 
Back
Top Bottom