Yesu na Jobless: Dhana ya janga la ukosefu wa ajira; kuwahi sio kufanikiwa

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
28,297
Reaction score
68,017
Yesu na Jobless: Dhana ya Janga la Ukosefu wa Ajira; Kuwahi sio Kufanikiwa

Anaandika, Robert Heriel.
Mwanafalsafa.

Kuwahi kupata ajira au kazi haimaanishi utawahi kufanikiwa, maisha hayapo hivyo. Na kuchelewa kupata kazi au ajira haimaanishi ndio utachelewa kupata mafanikio au hautafanikiwa kabisa.

Mafanikio ya mtu siku zote hupimwa mwishoni na sio mwanzoni. Hilo likae kwenye akili yako. Kama uliwahi sikia msemo, fainali uzeeni. Basi ndivyo maisha yalivyo. Niccolò Machiavelli aliwasema, "the end justifies the means" ingawaje falsafa hii ilikuwa ya kisiasa kwa wakati huo. Lakini pia inahusu maisha ya mwanadamu katika nyanja karibu zote za maisha. Mshindi anapatikana mwishoni na wala sio mwanzoni.

Yesu aliwahi kusema, "atakayevumilia mpaka mwisho ndiye atakayeokoka/atakayeshinda." Sisemi kumtia mtu moyo isipokuwa nazungumzia uhalisia wala sisemi kumfanya mtu abweteke asifanye wajibu wake, la hasha! Isipokuwa najaribu kueleza jambo muhimu katika maisha la kila mtu kujidhatiti ili kupata mwisho uliomwema.

Taikon nimeandika andiko hili ili kuwafanya wale wasio na kazi wasione wivu pale wanapoona wenzao wapo kazini wakichanja mbuga katika mafanikio. Pia wale wenye ajira au kazi wasiwadharau wale wasio na ajira au kazi kwa maana maisha hayapo hivyo.

Maisha unaweza ukawahi kupata kazi na ukafanya miaka 10 alafu ukashangaa yule ambaye hakuwa na kazi akapata dili ambalo ndani ya mwaka mmoja amekupiga gap la kukuacha mdomo wazi.

Embu tusome kisa hiki Kwanza: Yesu na Jobless
Mathayo 20:4
Akatoka mnamo saa tatu, akaona wengine wamesimama sokoni wasiokuwa na kazi
Mathayo 20:6
Hata kama saa kumi na moja akatoka, akakuta wengine wamesimama, akawaambia, mbona mmesimama hapa mchana kutwa bila kazi?
Mathayo 20:7
Wakamwambia, kwa sababu hakuna mtu aliyetuajiri. Akawaambia, enendeni nanyi katika shamba la mizabibu.
😀😀😀
Aya hizi nikizisoma huwaga nachekaga sana.

Aya hizi zinatufunulia mambo Yafuatayo:

i. Tatizo la ajira lilikuwepo tangu zamani enzi za Yesu. Hii ni kutokana na kukua kwa miji.
ii. Suala la vijana kuzurura pasipo na kazi halikuanza leo
iii. Vijana ili wapate kazi itawapasa watoke kuzurura au kukaa vijiweni kuliko kushinda ndani kama wali. Kazi hazikufuati nyumbani kwenu. Tunaona vijana wa barabarani na sokoni ndio waliopata kazi.
iv. Tangu zamani kama huna connection ilikuwa ngumu kupata kazi. Aya inaonyesha majibu ya jobless kuwa hakuna mtu wa kuwapa kazi.

Tusome kisa kizima tumalize Kabisa;
Mathayo 20:1
Kwa maana ufalme wa mbinguni umefanana na mtu mwenye nyumba aliyetoka alfajiri kwenda kuajiri wakulima awapeleke katika shamba lake la mizabibu.

Mathayo 20:2
Naye alipokwisha kupatana na wakulima kuwapa kutwa dinari, aliwapeleka katika shamba lake la mizabibu.

Mathayo 20:3
Akatoka mnamo saa tatu, akaona wengine wamesimama sokoni wasiokuwa na kazi;

Mathayo 20:4
na hao nao akawaambia, Enendeni nanyi katika shamba langu la mizabibu, na iliyo haki nitawapa. Wakaenda.

Mathayo 20:5
Akatoka tena mnamo saa sita na saa kenda, akafanya vile vile.

Mathayo 20:6
Hata kama saa kumi na moja akatoka, akakuta wengine wamesimama, akawaambia, Mbona mmesimama hapa mchana kutwa bila kazi?

Mathayo 20:7
Wakamwambia, Kwa sababu hakuna mtu aliyetuajiri. Akawaambia, enendeni nanyi katika shamba la mizabibu.

Mathayo 20:8
Kulipokuchwa, yule bwana wa shamba akamwambia msimamizi wake, Waite wakulima, uwalipe ujira wao, ukianzia wa mwisho hata wa kwanza.

Mathayo 20:9
Na walipokuja wale wa saa kumi na moja, walipokea kila mtu dinari.

Mathayo 20:10
Na wale wa kwanza walipokuja, walidhani kwamba watapokea zaidi; na hao pia wakapokea kila mtu dinari.

Mathayo 20:11
Basi wakiisha kuipokea, wakamnung’unikia mwenye nyumba,

Mathayo 20:12
wakisema, Hao wa mwisho wametenda kazi saa moja tu, nawe umewasawazisha na sisi tuliostahimili taabu na hari za mchana kutwa.

Mathayo 20:13
Naye akamjibu mmoja wao, akamwambia, Rafiki, sikudhulumu; hukupatana nami kwa dinari?

Mathayo 20:14
Chukua iliyo yako, uende zako; napenda kumpa huyu wa mwisho sawa na wewe.

Mathayo 20:15
Si halali yangu kutumia vilivyo vyangu kama nipendavyo? Au jicho lako limekuwa ovu kwa sababu ya mimi kuwa mwema?

Mathayo 20:16
Vivyo hivyo wa mwisho watakuwa wa kwanza, na wa kwanza watakuwa wa mwisho.

Hapa kuna makundi mawili

1. waliowahi kupata kazi/ajira
2. waliochelewa kupata kazi/ajira.

Makundi haya yapo hàta hivi leo, wapo wanaowahi kupata kazi soon wanapohitimu Mafunzo au Ujuzi Fulani, na wapo wanaosota mpaka miaka kumi Kama sio ishirini kabisa. Yaani wanapata kazi jioni Kabisa.

Waliowahi kupata kazi mapema kikawaida lazima wategemee malipo na mafanikio zaidi kuliko waliochelewa kupata kazi. Lakini matokeo yake mtoaji/mwajiri ambaye ni Mungu anafanya vile apendavyo, anaweza mwishoni kumpa mafanikio yule aliyechelewa huku wewe uliyefanya kazi Kwa miaka nenda rudi ukiachwa solemba au kupewa mafanikio kidunchu.

Kutangulia sio kufika. Na kufika sio kukaa. Hizo sio kauli za kufarijiana isipokuwa zinabeba uhalisia wa maisha kwa kiasi kikubwa.

Sio ajabu kijana wa miaka 80's akapitwa kimaisha na kijana wa miaka 2000's. Jambo kama hilo ni jambo la kawaida wala lisikuumize kichwa.

Yesu na kisa cha majobless kinawapa imani vijana wa zama za leo kuwa na subira na kuridhika kwa yote waliyonayo katika maisha yao.

Kisa hiki kinawatahadharisha pia vijana kuwa kuhangaika sana hakukufanyi ufanikiwe😂😂 upo msemo usemao; "Jitihada hazizidi Kudura"

Wakati nasoma wapo vijana waliokuwa mahiri sana kwenye masomo, waliokuwa wakijitahidi kusoma na kujishughulisha na mambo ya kishule, na matokeo mazuri ya kishule walikuwa wakiyapata hali iliyotoa matumaini na Imani kuwa watafanya vizuri katika mitihani ya mwisho, lakini haikuwa hivyo. Baadhi yao hawakufaulu walishindwa huku wakiinuka baadhi ya ambao walikuwa hawajatarajiwa kufaulu😀😀. Hivyo ndivyo maisha yalivyo.

Kwenye maisha, ridhika na kile Mungu amekupatia. Mwenzako akibarikiwa usipate kinyongo wala usitamani mali ya jirani yako.
Na wewe upataye usidharau wala usiwe na kiburi na kujiona bora au unaakili kuliko waliokosa.

Taikon mara nyingi hapendi watu wenye kiburi na kujiona wao ni bora kuliko wengine. Lakini pia hapendi watu wanaojidharau na kujiona duni.

Siku zote wenye ehkima huangalia zaidi mwisho wao kwani ndipo matokeo yatakapotangazwa kuliko mwanzo au katikati yao.
Wapumbavu huingalia leo yao tuu.
Wenye hekima na akili hujivuna na kujitamba mwanzoni au katikati ya pambano mwishowe huingia katika fedheha.

Kijana, usikae ndani kama mwari tafuta kazi. Jishughulishe, jitahidi kadri ya uwezo wako usiwe mzigo ndani ya jamii. Mwanaume unapaswa kutegemewa sio kutegemea. Mwanamke ni halali na haki yake hata akiwa mtegemezi. Hiyo ni haki yake. Kutafuta pesa Kwa mwanamke ni hisani tuu na wala sio wajibu wake.

Taikon amemaliza,

Ijumaa Kareem.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi,
Kwa sasa Dar es salaam.
 
Hivi hadithi kwenye biblia inanifirisha sana lakini walao ndugu ROBERT HERIEL umeweza kuitafsiri kwa nyakati zetu hizi ambazo maisha ni magumu kwa kiasi chake.

Binafsi nimeanza kujishughulisha na utafutaji wa hela nikiwa mdogo sana tokea miaka 99 na hata sasa siwezi kusema ni aheri .

lakini kuna wenzangu wameanza kutafuta hela miaka ya juzi juzi ya 2018 leo hii wana mafanikio ya moja kwa moja.
Hii kuna wakati ilinipekekea kukata tamaa kwa kiasi kikubwa lakini hivi karibuni nimejipa moyo kwamba maisha ni kuishi kwa amani hata kama hauna kile wala hiki.

Kikubwa kufanya wajibu kwa bidii bila ya kuweka matarajio makubwa huku ukimtanguliza mungu katika kila hali bila ya kukata tamaa .

Uliwahi kutolewa mfano wa mtu alie kua akipasua jiwe kwa nyundo, aliweza kupiga nyundo 99 bila ya jiwe kupasuka akakata tamaa na kuachana na hio kazi.

Alitokea mtu mmoja akiwa na nyundo yeye alipiga nyundo moja tu na jiwe kupasuka.

Kumbe yule wa awali alihitaji kupiga nyundo moja ya mwisho kabla ya kuta tamaa, lakini alikata tamaa na mwishowe alishindwa moja kwa moja.

Tusikate tamaa kama vijana katika lolote lile tufanyalo hata kama litachukua muda kiasi gani ilimradi tu tunajaliwa uhai na uzima.
 
Kuna braza alifungwa akiwa na miaka 19 alikuja kutoka akiwa na 47.

Katoka hakuna hata ndugu aliyemshobokea, akapambana na kwa mbinu anazozijua yeye , Leo ana familia na maisha ya kutambia mjini.

Kawapita hata aliowaacha mtaani.

Kutangulia sio kufika.
 
Imekaa vizuri kwenye kuwatia moyo vijana kuliko zile nyuzi za kukatishana tamaa. Maisha ni safari yenye vita vikali ambavyo kila anayekuzunguka anaweza kuwa kikwazo cha kufanikiwa kwako.

Ni kweli kuna watu wana watu wa kuwasaidia lakini walio wengi hawana watu wa kuwasaidia.
Lakini katika yote " Hakuna marefu yasiyokuwa na ncha " au " Kila jambo lina mwisho wake "
 
Yesu na Jobless: Dhana ya Janga la Ukosefu wa Ajira; Kuwahi sio Kufanikiwa

Anaandika, Robert Heriel.
Mwanafalsafa.

Kuwahi kupata ajira au kazi haimaanishi utawahi kufanikiwa, maisha hayapo hivyo. Na kuchelewa kupata kazi au ajira haimaanishi ndio utachelewa kupata mafanikio au hautafanikiwa kabisa.

Mafanikio ya mtu siku zote hupimwa mwishoni na sio mwanzoni. Hilo likae kwenye akili yako. Kama uliwahi sikia msemo, fainali uzeeni. Basi ndivyo maisha yalivyo. Niccolò Machiavelli aliwasema, "the end justifies the means" ingawaje falsafa hii ilikuwa ya kisiasa kwa wakati huo. Lakini pia inahusu maisha ya mwanadamu katika nyanja karibu zote za maisha. Mshindi anapatikana mwishoni na wala sio mwanzoni.

Yesu aliwahi kusema, "atakayevumilia mpaka mwisho ndiye atakayeokoka/atakayeshinda." Sisemi kumtia mtu moyo isipokuwa nazungumzia uhalisia wala sisemi kumfanya mtu abweteke asifanye wajibu wake, la hasha! Isipokuwa najaribu kueleza jambo muhimu katika maisha la kila mtu kujidhatiti ili kupata mwisho uliomwema.

Taikon nimeandika andiko hili ili kuwafanya wale wasio na kazi wasione wivu pale wanapoona wenzao wapo kazini wakichanja mbuga katika mafanikio. Pia wale wenye ajira au kazi wasiwadharau wale wasio na ajira au kazi kwa maana maisha hayapo hivyo.

Maisha unaweza ukawahi kupata kazi na ukafanya miaka 10 alafu ukashangaa yule ambaye hakuwa na kazi akapata dili ambalo ndani ya mwaka mmoja amekupiga gap la kukuacha mdomo wazi.

Embu tusome kisa hiki Kwanza: Yesu na Jobless
Mathayo 20:4
Akatoka mnamo saa tatu, akaona wengine wamesimama sokoni wasiokuwa na kazi
Mathayo 20:6
Hata kama saa kumi na moja akatoka, akakuta wengine wamesimama, akawaambia, mbona mmesimama hapa mchana kutwa bila kazi?
Mathayo 20:7
Wakamwambia, kwa sababu hakuna mtu aliyetuajiri. Akawaambia, enendeni nanyi katika shamba la mizabibu.
😀😀😀
Aya hizi nikizisoma huwaga nachekaga sana.

Aya hizi zinatufunulia mambo Yafuatayo;
i. Tatizo la ajira lilikuwepo tangu zamani enzi za Yesu. Hii ni kutokana na kukua kwa miji.
ii. Suala la vijana kuzurura pasipo na kazi halikuanza leo
iii. Vijana ili wapate kazi itawapasa watoke kuzurura au kukaa vijiweni kuliko kushinda ndani kama wali. Kazi hazikufuati nyumbani kwenu. Tunaona vijana wa barabarani na sokoni ndio waliopata kazi.
iv. Tangu zamani kama huna connection ilikuwa ngumu kupata kazi. Aya inaonyesha majibu ya jobless kuwa hakuna mtu wa kuwapa kazi.

Tusome kisa kizima tumalize Kabisa;
Mathayo 20:1
Kwa maana ufalme wa mbinguni umefanana na mtu mwenye nyumba aliyetoka alfajiri kwenda kuajiri wakulima awapeleke katika shamba lake la mizabibu.

Mathayo 20:2
Naye alipokwisha kupatana na wakulima kuwapa kutwa dinari, aliwapeleka katika shamba lake la mizabibu.

Mathayo 20:3
Akatoka mnamo saa tatu, akaona wengine wamesimama sokoni wasiokuwa na kazi;

Mathayo 20:4
na hao nao akawaambia, Enendeni nanyi katika shamba langu la mizabibu, na iliyo haki nitawapa. Wakaenda.

Mathayo 20:5
Akatoka tena mnamo saa sita na saa kenda, akafanya vile vile.

Mathayo 20:6
Hata kama saa kumi na moja akatoka, akakuta wengine wamesimama, akawaambia, Mbona mmesimama hapa mchana kutwa bila kazi?

Mathayo 20:7
Wakamwambia, Kwa sababu hakuna mtu aliyetuajiri. Akawaambia, enendeni nanyi katika shamba la mizabibu.

Mathayo 20:8
Kulipokuchwa, yule bwana wa shamba akamwambia msimamizi wake, Waite wakulima, uwalipe ujira wao, ukianzia wa mwisho hata wa kwanza.

Mathayo 20:9
Na walipokuja wale wa saa kumi na moja, walipokea kila mtu dinari.

Mathayo 20:10
Na wale wa kwanza walipokuja, walidhani kwamba watapokea zaidi; na hao pia wakapokea kila mtu dinari.

Mathayo 20:11
Basi wakiisha kuipokea, wakamnung’unikia mwenye nyumba,

Mathayo 20:12
wakisema, Hao wa mwisho wametenda kazi saa moja tu, nawe umewasawazisha na sisi tuliostahimili taabu na hari za mchana kutwa.

Mathayo 20:13
Naye akamjibu mmoja wao, akamwambia, Rafiki, sikudhulumu; hukupatana nami kwa dinari?

Mathayo 20:14
Chukua iliyo yako, uende zako; napenda kumpa huyu wa mwisho sawa na wewe.

Mathayo 20:15
Si halali yangu kutumia vilivyo vyangu kama nipendavyo? Au jicho lako limekuwa ovu kwa sababu ya mimi kuwa mwema?

Mathayo 20:16
Vivyo hivyo wa mwisho watakuwa wa kwanza, na wa kwanza watakuwa wa mwisho.

Hapa kuna makundi mawili

1. waliowahi kupata kazi/ajira
2. waliochelewa kupata kazi/ajira.

Makundi haya yapo hàta hivi leo, wapo wanaowahi kupata kazi soon wanapohitimu Mafunzo au Ujuzi Fulani, na wapo wanaosota mpaka miaka kumi Kama sio ishirini kabisa. Yaani wanapata kazi jioni Kabisa.

Waliowahi kupata kazi mapema kikawaida lazima wategemee malipo na mafanikio zaidi kuliko waliochelewa kupata kazi. Lakini matokeo yake mtoaji/mwajiri ambaye ni Mungu anafanya vile apendavyo, anaweza mwishoni kumpa mafanikio yule aliyechelewa huku wewe uliyefanya kazi Kwa miaka nenda rudi ukiachwa solemba au kupewa mafanikio kidunchu.

Kutangulia sio kufika. Na kufika sio kukaa. Hizo sio kauli za kufarijiana isipokuwa zinabeba uhalisia wa maisha kwa kiasi kikubwa.

Sio ajabu kijana wa miaka 80's akapitwa kimaisha na kijana wa miaka 2000's. Jambo kama hilo ni jambo la kawaida wala lisikuumize kichwa.

Yesu na kisa cha majobless kinawapa imani vijana wa zama za leo kuwa na subira na kuridhika kwa yote waliyonayo katika maisha yao.

Kisa hiki kinawatahadharisha pia vijana kuwa kuhangaika sana hakukufanyi ufanikiwe😂😂 upo msemo usemao; "Jitihada hazizidi Kudura"

Wakati nasoma wapo vijana waliokuwa mahiri sana kwenye masomo, waliokuwa wakijitahidi kusoma na kujishughulisha na mambo ya kishule, na matokeo mazuri ya kishule walikuwa wakiyapata hali iliyotoa matumaini na Imani kuwa watafanya vizuri katika mitihani ya mwisho, lakini haikuwa hivyo. Baadhi yao hawakufaulu walishindwa huku wakiinuka baadhi ya ambao walikuwa hawajatarajiwa kufaulu😀😀. Hivyo ndivyo maisha yalivyo.

Kwenye maisha, ridhika na kile Mungu amekupatia. Mwenzako akibarikiwa usipate kinyongo wala usitamani mali ya jirani yako.
Na wewe upataye usidharau wala usiwe na kiburi na kujiona bora au unaakili kuliko waliokosa.

Taikon mara nyingi hapendi watu wenye kiburi na kujiona wao ni bora kuliko wengine. Lakini pia hapendi watu wanaojidharau na kujiona duni.

Siku zote wenye ehkima huangalia zaidi mwisho wao kwani ndipo matokeo yatakapotangazwa kuliko mwanzo au katikati yao.
Wapumbavu huingalia leo yao tuu.
Wenye hekima na akili hujivuna na kujitamba mwanzoni au katikati ya pambano mwishowe huingia katika fedheha.

Kijana, usikae ndani kama mwari tafuta kazi. Jishughulishe, jitahidi kadri ya uwezo wako usiwe mzigo ndani ya jamii. Mwanaume unapaswa kutegemewa sio kutegemea. Mwanamke ni halali na haki yake hata akiwa mtegemezi. Hiyo ni haki yake. Kutafuta pesa Kwa mwanamke ni hisani tuu na wala sio wajibu wake.

Taikon amemaliza,

Ijumaa Kareem.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi,
Kwa sasa Dar es salaam.
Wajingawajinga Kama wewe ndo hujaga na fungu vya biblia kama hivyo.....
 
Imekaa vizuri kwenye kuwatia moyo vijana kuliko zile nyuzi za kukatishana tamaa . Maisha ni safari yenye vita vikali ambavyo kila anayekuzunguka anaweza kuwa kikwazo cha kufanikiwa kwako .

Ni kweli kuna watu wana watu wa kuwasaidia lakini walio wengi hawana watu wa kuwasaidia .
Lakini katika yote " Hakuna marefu yasiyokuwa na ncha " au " Kila jambo lina mwisho wake "

Naam Mkuu
 
Kuna braza alifungwa akiwa na miaka 19 alikuja kutoka akiwa na 47.

Katoka hakuna hata ndugu aliyemshobokea, akapambana na kwa mbinu anazozijua yeye , Leo ana familia na maisha ya kutambia mjini.

Kawapita hata aliowaacha mtaani.

Kutangulia sio kufika.

Hiyo Noma Sana. Duuh
 
Hivi hadithi kwenye biblia inanifirisha sana lakini walao ndugu ROBERT HERIEL umeweza kuitafsiri kwa nyakati zetu hizi ambazo maisha ni magumu kwa kiasi chake.

Binafsi nimeanza kujishughulisha na utafutaji wa hela nikiwa mdogo sana tokea miaka 99 na hata sasa siwezi kusema ni aheri .

lakini kuna wenzangu wameanza kutafuta hela miaka ya juzi juzi ya 2018 leo hii wana mafanikio ya moja kwa moja.

Hii kuna wakati ilinipekekea kukata tamaa kwa kiasi kikubwa lakini hivi karibuni nimejipa moyo kwamba maisha ni kuishi kwa amani hata kama hauna kile wala hiki.

Kikubwa kufanya wajibu kwa bidii bila ya kuweka matarajio makubwa huku ukimtanguliza mungu katika kila hali bila ya kukata tamaa.

Uliwahi kutolewa mfano wa mtu alie kua akipasua jiwe kwa nyundo, aliweza kupiga nyundo 99 bila ya jiwe kupasuka akakata tamaa na kuachana na hio kazi.

Alitokea mtu mmoja akiwa na nyundo yeye alipiga nyundo moja tu na jiwe kupasuka.

Kumbe yule wa awali alihitaji kupiga nyundo moja ya mwisho kabla ya kuta tamaa, lakini alikata tamaa na mwishowe alishindwa moja kwa moja.

Tusikate tamaa kama vijana katika lolote lile tufanyalo hata kama litachukua muda kiasi gani ilimradi tu tunajaliwa uhai na uzima.

Yes ni Kweli.
Maisha ni kufurahia Yale uliyojaliwa. Hivyo ndivyo namna ya kuwa na Amani
 
Wewe kuwa na amani na ulichojaliwa ridhika nacho tu hicho wenzio hawajaridhika bado wanasaka pesa...si kwa sababu Yesu anafundisha watu wawe masikini
 
Back
Top Bottom