Hapani Sio Kweli Masihi Mwana Wa Mariamu ni Mjumbe Tu Wa Allah Na Sio Mungu Na Hilo Atakuja Kulikataa Mwenyew Siku Ya Qiama Kama Alivyosema Allah Akatika Suurat Al Maaidah...
وَإِذْ قَالَ اللَّـهُ يَا عِيسَى ابْنَ مَرْيَمَ أَأَنتَ قُلْتَ لِلنَّاسِ اتَّخِذُونِي وَأُمِّيَ إِلَـٰهَيْنِ مِن دُونِ اللَّـهِ ۖ قَالَ سُبْحَانَكَ مَا يَكُونُ لِي أَنْ أَقُولَ مَا لَيْسَ لِي بِحَقٍّ ۚ إِن كُنتُ قُلْتُهُ فَقَدْ عَلِمْتَهُ ۚ تَعْلَمُ مَا فِي نَفْسِي وَلَا أَعْلَمُ مَا فِي نَفْسِكَ ۚ إِنَّكَ أَنتَ عَلَّامُ الْغُيُوبِ ﴿١١٦﴾
116. Na pindi Allaah Atakaposema: Ee ‘Iysaa mwana wa Maryam! Je, wewe uliwaambia watu: Nifanyeni mimi na mama yangu kuwa ni waabudiwa wawili badala ya Allaah? (‘Iysaa) atasema: Subhaanak! (Utakasifu ni Wako). Hainipasi mimi kusema yasiyo kuwa haki kwangu. Ikiwa nimesema hayo basi kwa yakini Ungeliyajua. (Kwani) Unayajua yale yote yaliyomo katika nafsi yangu, na wala mimi sijui yale yaliyomo katika Nafsi Yako, hakika Wewe Ni Mjuzi wa Ghaibu(Yaliyojificha).
مَا قُلْتُ لَهُمْ إِلَّا مَا أَمَرْتَنِي بِهِ أَنِ اعْبُدُوا اللَّـهَ رَبِّي وَرَبَّكُمْ ۚ وَكُنتُ عَلَيْهِمْ شَهِيدًا مَّا دُمْتُ فِيهِمْ ۖ فَلَمَّا تَوَفَّيْتَنِي كُنتَ أَنتَ الرَّقِيبَ عَلَيْهِمْ ۚ وَأَنتَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ شَهِيدٌ ﴿١١٧﴾
117. Sijawaambia (lolote) ila yale tu Uliyoniamrisha kwamba: Mwabuduni Allaah Rabb (Mola) wangu na Rabb wenu. Na nilikuwa juu yao shahidi wakati nilipokuwa nao. Uliponikamilishia muda Ukanichukua juu, Ulikuwa Wewe Ndiye Mwangalizi juu yao. Na Wewe Ni Mwenye Kushuhudia kila kitu.
إِن تُعَذِّبْهُمْ فَإِنَّهُمْ عِبَادُكَ ۖ وَإِن تَغْفِرْ لَهُمْ فَإِنَّكَ أَنتَ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ ﴿١١٨﴾
118. Ukiwaadhibu, basi bila shaka hao ni Waja Wako, na Ukiwaghufuria(Ukiwasamehe) basi hakika Wewe Ndiye Mwenye Enzi ya Nguvu Asiyeshindika, Mwenye Hikmah wa yote.
[36]