Yesu si Mungu, Paulo ana kesi ya kujibu

Status
Not open for further replies.
Kwa maana ilishushwa kwa kiarabu.du waarabu walipendelewa
 
KILA GOTI LITAPIGWA.. Bado mnao nafasi ya kumpokea yesu. Yesu ni mungu yesu akisema kitu kuwa nacho kinakuwa, yesu akimwambia mtu ona naye anaona, aliyekufa amka naye anaamka Muhammad hakufanya muujiza wowote, Allah anayedai akisema kitu kuwa kinakuwa alishindwa kumfanya Muhammad asome anamwambia soma Mara tatu mtu wap. yesu alimwambia mtu aliyepooza miaka 38 simama jitwike mzigo wako uende akasimama. Lazaro amka akaamka.
 
Hapa ntakuwa mtazama comments maana kubishana na watu wanaosoma kitabu chao jumapili mpaka jumapili yaani kikisomwa jpili hakifunguliwi tena mpaka jpili
 
Hapa ntakuwa mtazama comments maana kubishana na watu wanaosoma kitabu chao jumapili mpaka jumapili yaani kikisomwa jpili hakifunguliwi tena mpaka jpili
Sasa si bora jpili mlaka jpili, kuliko kuimba kila siku mistari hiyohiyo, halafu huelewi unaulizwa maswali unahanya hanya.
 
Soma bible bro, muombe mungu akuonyeshe ukweli upo wap. anayemkana Yesu tayari amekwishahukumiwa, message ya ukristo ni hiyo hiyo kuwa yesu ni mwana wa mungu,amefufuka katika wafu miaka na miaka tangu 1st century AD.Ukitaka kuelewa bible Fanya a honest study sio kusoma kwa lengo la kucriticize kutafuta verse moja yenye utata halaf verse zinazofuata zinakuprove wrong..Ukitaka kuelewa yesu jifunze kutoka kwa wafuasi wake tangu enzi za Petro,Yohana na kuendelea Fanya honest study ya history of Christianity.. Yesu wa kwenye Quran is unhistorical haexist.
 
Endeleen na akili Mgando kiasi hicho,Mung wetu sis hana mipaka katika lugha,anakubali zoteeee!!!..
 


Nakuuliza tena ,

Kwa kiarabu Kristo Anaitwa nani ???

Kwa kiarabu Mkristo anaitwa nani ????




QURAN 5:72-73

Hakika wamekufuru walio sema: Mwenyezi Mungu ni Masihi mwana wa Maryamu!
Na hali Masihi mwenyewe alisema: Enyi Wana wa Israili! Muabuduni Mwenyezi Mungu, Mola wangu Mlezi na Mola wenu Mlezi. Kwani anaye mshirikisha Mwenyezi Mungu, hakika Mwenyezi Mungu atamharimishia Pepo, na mahala pake ni Motoni. Na walio dhulumu hawatakuwa na wa kuwanusuru.


TAFSIRI:


Wenye kudai kuwa Mwenyezi Mungu yu katika Isa bin Maryam hata akawa yeye Mungu, kama wasemavyo Wakristo hii leo, hakika wamekufuru! Yeye Isa hana dhambi ya haya, kwani hakupata kudai hivyo hata mara moja. Bali yeye aliwaamrisha Wana wa Israili wamsafie imani Mwenyezi Mungu peke yake kwa kusema: Hakika Mwenyezi Mungu ndiye aliye niumba mimi na nyinyi, na ndiye anaye niendeshea mambo yangu yote, na kwamba kila mwenye kumshirikisha Mwenyezi Mungu malipo yake ni kuwa hatoingia Peponi kabisa, bali ataingia Motoni, kwa kuwa amekiuka mipaka ya Mwenyezi Mungu.

Na mwenye kuvunja mipaka yake hataepuka na adhabu.

(Yesu kasema: "Sikia, Israeli, Bwana Mungu wetu ni Bwana mmoja." Marko 12.28.

"Mimi siwezi kufanya neno mwenyewe".Yohana 5.30

"Ninapaa kwenda kwa...Mungu wangu naye ni Mungu wenu." Yohana 20.17 )


Kwa hakika wamekufuru walio sema: Mwenyezi Mungu ni wa tatu wa Utatu. Hali hakuna mungu ila Mungu Mmoja.

Na ikiwa hawaachi hayo wanayo yasema, kwa yakini itawakamata adhabu chungu wale wanao kufuru



TAFSIRI:

Haiwi mwenye kudai kuwa Mwenyezi Mungu ni mmoja katika Utatu, kama wadaivyo Wakristo sasa, awe anamuamini Mwenyezi Mungu.!! Na hakika iliyo thibiti ni kuwa hapana mungu ila Mwenyezi Mungu mmoja pekee. Na ikiwa hawa walio potoka hawatoacha itikadi zao potovu, wakarejea kwenye ut'iifu wa Mwenyezi Mungu, hapana budi ila itawasibu adhabu kali.

(Biblia inasema kuwa ya kwanza katika Amri Kumi alizo pewa Musa ni:

"Usiwe na miungu mingine ila mimi." - Kutoka 20.3.

"Wewe umeonyeshwa haya, ili upate kujua ya kuwa Bwana ndiye Mungu, hapana ila yeye." - Kumbukumbu la Torati 4.35.

Katika Injili ya Yohana 17.3 Yesu anamsemeza Mwenyezi Mungu: "Na uzima wa milele ndio huu, Wakujue wewe, Mungu wa pekee wa kweli na Yesu Kristo uliyemtuma.")
 



Angalia hii documentary kutoka BBC , humo utawakuta hao walioitwa an-Nasaaraa


ZIKO EPISODES 3


 
yesu ni mungu... tukitumia logic zenu waislam kuwa mungu hawez kufa basi yesu ni mungu tayari kwenye islam sababu qurqn 4:157 inasema yesu hakufa msalabani...case closed


Kwa kweli yapo maandiko mengi sana katika Biblia yanayothibitisha kuwa Yesu (Amani iwe naye) ni mtume tu.

Haya hapa chini baadhi tuu ya maandiko hayo:

YOHANA 5:24

"Kweli nawaambieni, anayesikia neno langu, na kumwamini yule aliyenituma, anao uzima wa milele. Hatahukumiwa kamwe, bali amekwisha pita kutoka kifo na kuingia katika uzima.

YOHANA 5:30

"Mimi siwezi kufanya kitu kwa uwezo wangu mwenyewe. Mimi nina hukumu kama ninavyosikia kutoka kwa Baba, nayo hukumu yangu ni ya haki. Nia yangu si kufanya nipendavyo mwenyewe, bali apendavyo yule aliyenituma.

YOHANA 5:36

Lakini mimi nina ushahidi juu yangu ambao ni mkuu zaidi kuliko ule wa Yohane. Kwa maana kazi ninazofanya, kazi alizonipa Baba nizifanye, ndizo zinazonishuhudia kwamba Baba ndiye aliyenituma.

YOHANA 5:37

Naye Baba aliyenituma hunishuhudia. Ninyi hamjapata kamwe kusikia sauti yake, wala kuuona uso wake.

YOHANA 7:16

Hapo Yesu akawajibu, "Mafundisho ninayofundisha si yangu, bali ni yake yeye aliyenituma.

YOHANA 7:28

Basi, Yesu alipokuwa anafundisha Hekaluni alipaaza sauti na kusema, "Ati mnanijua; hata nilikotoka mnakujua! Hata hivyo, sikuja kwa mamlaka yangu mwenyewe; ila yeye aliyenituma mimi ni wa kweli, nanyi hamumjui.

YOHANA 7:29

Lakini mimi namjua kwa sababu nimetoka kwake, naye ndiye aliyenituma."


YOHANA 7:33

Yesu akasema, "Bado niko nanyi kwa muda mfupi, kisha nitamwendea yule aliyenituma.

YOHANA 8:16

Hata nikihukumu, hukumu yangu ni ya haki kwa sababu mimi siko peke yangu; Baba aliyenituma yuko pamoja nami.


YOHANA 8:18

Mimi najishuhudia mwenyewe, naye Baba aliyenituma, ananishuhudia pia."

YOHANA 8:26

Ninayo mengi ya kusema na kuhukumu juu yenu. Lakini yule aliyenituma ni kweli; nami nauambia ulimwengu mambo yale tu niliyoyasikia kutoka kwake."

YOHANA 8:29

Yule aliyenituma yuko pamoja nami; yeye hakuniacha peke yangu kwani nafanya daima yale yanayompendeza."

YOHANA 6:38

kwani nimeshuka kutoka mbinguni si kwa ajili ya kufanya matakwa yangu, ila kutimiza matakwa ya yule aliyenituma.

YOHANA 6:39

Na matakwa ya yule aliyenituma ndiyo haya: nisimpoteze hata mmoja kati ya wale alionipa, ila niwafufue wote Siku ya mwisho.

YOHANA 12:44

Kisha Yesu akasema kwa sauti kubwa, "Mtu aliyeniamini, haniamini mimi tu, ila anamwamini pia yule aliyenituma.

YOHANA 12:49

Mimi sikunena kwa mamlaka yangu mwenyewe, ila Baba aliyenituma ndiye aliyeniamuru niseme nini na niongee nini.

MATAYO 10:40

"Anayewakaribisha ninyi, ananikaribisha mimi; na anayenikaribisha mimi, anamkaribisha yule aliyenituma.

MARKO 9:37

"Anayempokea mtoto kama huyu kwa jina langu, ananipokea mimi; na anayenipokea mimi, hanipokei mimi tu, bali anampokea yule aliyenituma."

LUKA 9:48

akawaambia, "Mtu yeyote anayempokea mtoto huyu mdogo kwa jina langu, ananipokea mimi; na yeyote anayenipokea mimi, anampokea yule aliyenituma. Maana yule aliye mdogo kuliko wote kati yenu ndiye aliye mkubwa kuliko wote."

LUKA 10:16

Halafu akasema, "Anayewasikiliza ninyi, ananisikiliza mimi; na anayekataa kuwapokea ninyi, anakataa kunipokea mimi. Yeyote anayekataa kunipokea, anakataa kumpokea yule aliyenituma."

YOHANA 4:34

Yesu akawaambia, "Chakula changu ni kufanya anachotaka yule aliyenituma na kuitimiza kazi yake.

YOHANA 9:4

Kukiwa bado mchana yatupasa kuendelea kufanya kazi za yule aliyenituma; maana usiku unakuja ambapo mtu hawezi kufanya kazi.

YOHANA 13:20

Kweli nawaambieni anayempokea yule ninayemtuma anaponipokea mimi; na anayenipokea mimi, anampokea yule aliyenituma."

YOHANA 14:24

Asiyenipenda hashiki maneno yangu. Na neno mlilosikia si langu, bali ni lake Baba aliyenituma.

YOHANA 15:21

Lakini hayo yote watawatendeeni ninyi kwa sababu ya jina langu, kwani hawamjui yeye aliyenituma.

YOHANA 16:5

Lakini sasa namwendea yule aliyenituma; na hakuna hata mmoja wenu anayeniuliza: `Unakwenda wapi?`
 
Hakuna hoja ya maana uliyoandika zaidi ya pumba. Mimi sio mgeni na ukristo. Nimezaliwa kutoka kwa wazazi wa kikristo tambua ya kwamba unaongea na mtu mwenye uelewa wake na sio mshabiki wa kidini. Ibada gani utaweza kuitenda china wakati wanaongea kichina na wakati mtu hajui kichina? Hujui kitakacho kuzungumzwa hivyo hutajua nini wapaswa kufanya au kuitikiaje kutokana utofauti wa lugha. Kama ni RC umezoea kusikia kwajina la baba, na la mwana na roho mtakatifu ila ukienda kanisa la mataifa mengine hutosikia kwa jina la baba,....... bali watatamka kwa lugha zinginezo.
 
haijalishi anatafsiri nani. Na ndio maana unakuta matoleo mengi ya biblia lakini yanatofautiana katika misamiati.
 

Kama mungu anatambua kila lugha kuna haja gani Ya kusali lugha Ya mtu mwingine? Wakati kumbe mungu hata lugha yangu anatambua!
Kama suala ni uniformity kuna haja gani ya kutafsiri kwenye miadhara au wakati wa mawaidha?....kwa nini watu wasiongee kiarabu tu?........
 
Endeleen na akili Mgando kiasi hicho,Mung wetu sis hana mipaka katika lugha,anakubali zoteeee!!!..View attachment 410559View attachment 410560View attachment 410561
Unaonesha jinsi gani ulivyo kilaza. Mungu anajua lugha nyingi ila je kawaumba wanadamu wenye kujua na kuongea lugha zote za ulimwenguni bila kujifunza ili anapoenda taifa lolote lile aelewe padri, mchungaji askofu kuwa anazungumza nini? Siongelei kukubali lugha, maana muislam akiomba Mungu kinyakyusa Mungu huipokea dua yake vizuri tu. Nachoongelea mimi ni umoja. Naweza kumchukua mzaramo, mjapani, mfaransa na mkulya pamoja kisha ukamwambia mkulya naomba swalisha kisha akashwalisha mbele ya mjapan na mfaransi. Jambo hilo ni ngupu katika ukristo, ukimwambia mkulya awasalishe watu wa mataifa mengine kama vile mfaransa mjapani, mjerumani,mreno pamoja basi lazima mkulya atumie lugha ya kingereza au kiswahili. Sasa kama mjapani na mreno hajui kiswahili na kingereza basi uelewano hapo hakuna.
 
Paulo anaweza kua sawa tu,kwa MUNGU yote yawezekana kama alivyoweza kumtengeneza popo.wengine wanamuita ndege na wengine humwita mnyama.yamkini YESU alikua BINADAMU na MUNGU pia
Asante sana, jibu fupi lenye kujitosheleza! Sidhani kama kuna mjadaa tena!
 

Kwa taarifa yako ni zaidi ya mara moja katika biblia Mungu anatumia watu walioanguka kama mfano, kuwabadilisha na kufanya Dunia imtambue kwamba yeye ni Mungu kupitia shuhuda za watu wenye mioyo migumu.

Yuda alianguka na kuzaa na mjane wa watoto zake, hapa ndio ukoo wa Yesu ulipoanzia

Samsoni alianguka mara nyingi sana, lakini bado aliendelea kua mnadhiri wa Mungu.

Daudi alianguka na kulala na mke wa mtu na akazaa Sulemani, mfalme mwenye hekima zaidi na aliyetawala kwa Amani kuliko wengine, pia mfano mzuri kwa wakristo kwa namna Ya Mafanikio na kutembea na mungu.Lakini pia, ujenzi wa hekalu umempa heshima hata kwa wayaudi.

Nebkadreza alipigwa na uchizi baada ya kujisifia mji wa Bablon ni wake kajenga kwa nguvu zake, akawa chizi miaka 7 na hapo akatambua ukuu wa mungu.

BOTTOM LINE: Kila jambo Lina wakati wake,na Mungu hufanya kazi kwa njia za ajabu, anawanyeshea mvua wote walio na haki na wenye dhambi, kwa kua ipo siku atamwinua yeyote yule ili kuendeleza kazi yake.

Mitume wa Yesu hawakua perfect, pia...mbona hata mtoza kodi alikuja kua mtume hapo baadae (licha Ya kua mfano mbaya wa watu wapenda rushwa na wanyanganyi)...

Leo hii makanisa mengi yapo Thanks to barua za PAULO kwa mataifa mbalimbali, bila elimu yake kama farisayo (watu wanaojua kusoma na kuandika kipindi hicho) angewezaje kuandika barua zote hizo, maana mitume wengine hawakua wasomi (wengi wavuvi). Lakini kwa nini unamhuku mtu hata baada ya kusamehewa na Yesu mwenyewe?...Huoni yule aliyepinga zaidi akiamini ndio huleta changamoto zaidi hata kwa wale walikuwepo upande wake hapo kabla?
 
Wewe ongea maneno ya ngojera mimi nakupa andiko na wewe toa andiko. Nani alikuambia uislam haukuwepo kwanzia awali? Embu thubutu kunipa andiko linalosema 1. watu kabla ya Yesu walikuwa na dini inaitwa ukristo. Na la pili nipe aya inayosema ukristo ni dini ya Mungu.

Quran 2:213
Watu wote walikuwa ni umma mmoja. Mwenyezi Mungu akapeleka Manabii wabashiri na waonyaji. Na pamoja nao akateremsha Kitabu kwa Haki, ili kihukumu baina ya watu katika yale walio khitalifiana. Na wala hawakukhitalifiana ila wale walio pewa Kitabu hicho baada ya kuwafikia hoja zilizo wazi, kwa sababu ya uhasidi baina yao. Ndipo Mwenyezi Mungu kwa idhini yake akawaongoa walio amini kwendea haki katika mambo waliyo khitalifiana. Na Mwenyezi Mungu humwongoa amtakaye kwenye Njia Iliyo Nyooka


Ukristo ulianza baada ya Yesu kuondoka hivyo kipindi cha yesu na kabla ya yesu hakukuwa na dini inayoitwa Ukristo. Naomba ukipinga pinga kwa andiko sio porojo tu. Mimi nakupa hili. Soma matendo 11:16-26

Matendo 11:25-26

25. Kisha akatoka akaenda Tarso kumtafuta Sauli;
26 . hata alipokwisha kumwona akamleta Antiokia. Ikawa kwa muda wa mwaka mzima wakakusanyika pamoja na kanisa na kuwafundisha watu wengi. Na wanafunzi waliitwa Wakristo kwanza hapo Antiokia.
 
Elewa .nimekwambia Baba Wa imani .huo uislam kauleta mud wenu .katika bible kuna Ibrahim,isaka Na yakobo ambaye ndio Israel.
ndugu yangy nyankundo,yakobo kapewa jina la israel ukubwani,takriban miaka kumi na tano baada ya kuzaliwa ISHMAEL.

POINT hapa ni jina El,
kumbuka wakati waebrania wanakuja caanan kutoja iraq waliwakuta wacaanan wakiabudu mungu alieitwa El,kabla hata ya mungu yehova hajatokea,
maana yake ni kuwa abrahamu alikuwa akiabudu mungu El,
ni uongo kusema mungu alitaja jina lake kwa mara ya kwanza mbele ya yakobo,vinginevyo yakobo angeitwa israyahwh.
El ni jina la mungu huyo yehova ni mungu fake na sasa.
Logic ni kuwa El ndo huyohuyo Allah au pengine hata Elloh.

Sijui kwanini hawa wagalatia kila baada ya miaka 50 wanabadili jina la mungu wanaeabudu,saa hizi wanasema kumbe mungu wao anaitwa yesu na si jehova tena,ha ha ha ha
 
Elewa .nimekwambia Baba Wa imani .huo uislam kauleta mud wenu .katika bible kuna Ibrahim,isaka Na yakobo ambaye ndio Israel.
Nataka unioneshe kwenye biblia kuliko andikwa neno ukristo. Maana umeshindwa kunipa dini ya Ibrahim sasa ni wazi hakuujua ukristo kwasababu dini ya kikristo ilianza baada ya kuondoka kwa Yesu duniani. kwa mujibu wa andiko hili.

Matendo 11:16-26

16. Nikalikumbuka neno lile la Bwana, jinsi alivyosema, Yohana alibatiza kwa maji kweli, bali ninyi mtabatizwa kwa Roho Mtakatifu.
17 . Basi ikiwa Mwenyezi Mungu amewapa wao karama ile ile aliyotupa sisi tuliomwamini Bwana Yesu Kristo, mimi ni nani niweze kumpinga Mungu?
18 . Waliposikia maneno haya wakanyamaza, wakamtukuza Mungu, wakisema, Basi, Mungu amewajalia hata mataifa nao toba liletalo uzima.
19 . Basi wale waliotawanyika kwa sababu ya ile dhiki iliyotukia kwa habari ya Stefano, wakasafiri hata Foinike na Kipro na Antiokia, wasilihubiri lile neno ila kwa Wayahudi peke yao.
20 . Lakini baadhi ya hao walikuwa watu wa Kipro na Kirene, nao walipofika Antiokia wakasema na Wayahudi wa Kiyunani, wakihubiri habari njema za Bwana Yesu.
21. Mkono wa Bwana ukawa pamoja nao, watu wengi wakaamini, wakamwelekea Bwana.
22 . Habari hizo za watu hao zikafika masikioni mwa kanisa lililokuwako katika Yerusalemu; wakamtuma Barnaba, aende hata Antiokia.
23 . Naye, alipokwisha kufika na kuiona neema ya Mungu akafurahi, akawasihi wote waambatane na Bwana kwa kusudi la moyo.
24 . Maana alikuwa mtu mwema amejaa Roho Mtakatifu na imani; watu wengi wakaongezeka upande wa Bwana.
25 . Kisha akatoka akaenda Tarso kumtafuta Sauli;
26. hata alipokwisha kumwona akamleta Antiokia. Ikawa kwa muda wa mwaka mzima wakakusanyika pamoja na kanisa na kuwafundisha watu wengi. Na wanafunzi waliitwa Wakristo kwanza hapo Antiokia
 

Hiyo aya ya.71 wewe smt016 kwenye hiyo safari ya kwenda jehannam umo?¿ lengo la swali ili nijue naongea na muumini muisilamu au kafir?!
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…