Sasa nakuuliza wewe ujibu kwa niaba ya waislamu wenzako wote.
Sisi wakristo,
Tunaamini Yesu ni Mungu mwenyewe katika mwili wa nyama na damu.aliyeuvaa mwili huo aje kufa duniani tumjue na kumfuata.
Wewe ukiwa kama muislamu, unatumia vigezo gani kukataa uungu wa Yesu???? Kwa kudhani ni yule issa uliyefundishwa habari zake tokea madrasa?????
Na tuanzie na sifa za Mwenyezi Mungu ndani ya Qurani na biblia
Kutokuchoka
Kwa kuzingatia udhaifu mkubwa uliomo katika sifa dhaifu ya kuchoka ambayo pia inawakabili viumbe vyake na kwa kuzingatia kuwa yeye hana mfano wa yeyote wala na chochote katika kila hali, ni wazi kuwa siifa kuu nyingine ya Mungu wa kweli ni kutokuchoka (Yaani Mwenyezi Mungu daima ameepukana mbali na sifa ya kuchoka).
Kwa mantiki hiyo basi, ni wazi kuwa sifa hii nayo pia ni kigezo kingine muhimu kinachoweza kuwa hoja ya msingi ya kutofautisha Allah na Yehovah iwapo tu itabainika 'mmoja wao' hana sifa hiyo.
Hata hivyo, tusomapo maandiko ya Qur’ani Tukufu na Biblia takatifu tunaona vyote kwa pamoja vimuelezea Mweyezi Mungu yule yule mmoja aliyejitambulisha kwa Manabii wake mbali mbali kwa majina tofauti kwamba ndiye mwenye sifa hiyo.
Uthibitisho wa hilo tunaupata katika maandikio yafuatayo ya Qur’ani Tukufu na Biblia Takatifu:
Biblia:
"Je! wewe hukujua? hukusikia? Yeye Mungu wa milele, Bwana Muumba miisho ya dunia, hazimii, wala hachoki; akili zake hazichunguziki". (Isaya 40:28).
"Na tumeziumba mbingu na ardhi na vilivyomo kati yao katika nyakati sita, wala hayakutugusa machofu" (Qur’an;an 50:38).
Kulingana na shuhuda hizo juu, tunaona wazi kuwa Qur’ani Tukufu na Biblia Takatifu vyote kwa pamoja vinafundisha kuwa Mwenyezi Mungu yule yule mmoja aliyejifunua kwa Manabii wake mbali mbali kwa majina tofauti ndiye pekee asiyekuwa na sifa hiyo dhaifu ya kuchoka.
Kwa shuhuda hizo, ni wazi kuwa sifa hii nayo pia inadhihirisha kuwa Allah na Yehovah ni Mwenyezi Mungu yule yule mmoja, Muumbaji wa kila kinachoonekana na kisichoonekana, mwenye sifa kamilifu.
Kutokufa (Yu Daima)
Kwa kuzingatia kuwa yeye hafanani na kiumbe wake yeyote wala chochote katika kila hali, ni dhahiri kuwa sifa kuu nyingine ya msingi ya Mungu wa kweli ni lazima iwe kutokufa, hasa kwa kuzingatia kuwa yeye pekee yake ndiye anayetegemewa na viumbe wake wote kwa kila haja, kwa vile yeye peke yake ndiye Mwendeshaji wa mambo yote katika kila sekunde.
Hakuna yeyote wala chochote kinachoweza kuendesha ulimwengu na kukidhi haja zote za viumbe wote katika muda wote ambao Mungu angekufa.
Kwa mantiki hiyo basi, ni wazi kuwa sifa hii nayo pia ni kigezo muhimu na cha msingi kimachoweza, kuwa hoja ya msingi ya kutofautisha Allah na Yehovah iwapo tu itabainika 'mmoja wao' hana sifa hiyo. Hata hivyo, tusomapo maandiko ya Qur’ani Tukufu na Biblia Takatifu tunaona vyote vinafundisha kwamba mwenye sifa hiyo (ya kutokufa) ni Mwenyezi Mungu peke yake aliyejifunua au kujitambulisha kwa Manabii wake mbali mbali kwa majina tofauti.
Maandiko yafuatayo ya Qur’ani Tukufu na Biblia Takatifu yanathibitisha ukweli huu:
Biblia:
"Nitasema, Ee Mungu wangu, usiniondoe katikati ya siku zangu; Miaka yako nitangu kizazi hata kizazi. hapo mwanzo uliutia msingi wa nchi, Na mbingu ni kazi ya mikono yako. Hizi zitaharibika, bali Wewe utadumu; Naam, hizi zitachakaa kama nguo; Na kama mavazi utazibadilisha, Nazo zitabadilika. Lakini Wewe U yeye yule; Na miaka yako haitakoma". (Zaburi 102:24-27).
"Mungu akamwambia Musa, MIMI NIKO AMBAYE NIKO; akasema ndivyo utakavyowaambia wana wa Israeli; MIMI NIKO amenituma kwenu" (Kutoka 3:14).
"Ambaye yeye peke yake hapatikani na mauti, amekaa katika nuru isiyoweza kukaribiwa; wala hakuna mwanadamu aliyemwona, wala awezaye kumwona. Heshima na uweza una yeye hata milele. Amina". (1 Timotheo 6:16).
Qur’an:
"Wala usimuombe - pamoja na Allah (Mwenyezi Mungu) - Mungu mwingine; hakuna aabudiwaye kwa haki ila Yeye; kila kitu kitakufaisipokuwa yeye (Mwenyezi Mungu basi). Hukumu (Yahova mambo yote) iko kwake, na kwake mtarejezwa (nyote)". (Qur’ani 28:88).
Aidha, kwa sifa yake ya kutokuonekana ni wazi kuwa hakuna yeyote wala chochote (na chenye uwezo wa) kumwua.
"Allah (Mwenyezi Mungu) hakuna Mola ila yeye, (na) ndiye mwenye uhai wa maisha, Msimamia kila jambo..." (Qur’an, 2:255).
Kulingana na shuhuda hizo juu, tunaona wazi kuwa Qur’an Tukufu na Biblia Takatifu vyote kwa pamoja vinafundisha kwamba Mwenyezi Mungu yule yule mmoja aliyejifunua au kujitambulisha kwa Manabii wake mbali mbali kwa majina tofauti ndiye peke yake mwenye uhai wa milele (yu daima) - hafi-na kwa ujumla yeye peke yake ndiye mwenye sifa ya kutokufa.
Kwa shuhuda hizo, ni wazi kuwa sifa hii nayo pia inadhihirisha wazi kuwa Allah anayefundishwa na Qur’ani Tukufu ndiye Yehovah anayefundishwa na Biblia Takatifu kwa majina tofauti.
Ukweli huu tunaupata katika Qur’an, Torati, Zaburi, Injili .