Yesu wa Kenya anaenda kusulubishwa, manabii na mitume wa mchongo wakae kwa tahadhari

Yesu wa Kenya anaenda kusulubishwa, manabii na mitume wa mchongo wakae kwa tahadhari

Manabii na mitume tunaowasoma kwenye biblia walikuwa ni watu wa kuhangaika kutokana na kukataliwa na watu na watawala kutokana na ujumbe waliobeba kuwa kama ncha ya upanga kwa kukata na kupenya kunako. Mtume Paulo pamoja na kuwa mtume wa mataifa hatukuwahi kusikia alimiliki utajiri bali alihubiri injili kwa mahangaiko na mateso makubwa.

Lakini hawa kizazi hiki wanaishi maisha ya kifahari, kujenga mahekalu na mahoteli ya nyota kadhaa na kula bata bila kupata msukosuko wowote, tukisema ni wa mchongo tutakuwa tumekosea?
 
Yesu alikimbilia polisi
Screenshot_20230406-112627_WhatsApp.jpg
 
Huko jirani, wadau wanataka kumjambisha yule yesu wa mchongo, wanataka kumsulubisha kwa kadiri ya maandiko wakitarajia ufufuko wake siku ya tatu, je sisi tunasubiri nini? Hawa mitume na manabii wa mchongo inabidi wachezee vichapo.
Kenya ni wajaribishaji wa kila kitu
 
Amani iwe nanyi,

Kazi ya Mungu siku zote ina upinzani mkali. Tumeona Yesu OG, mitume na manabii walivyo uwawa, teswa na kudhihakiwa. Soma maandiko kwa urahisi wa rejea.

Huko jirani, wadau wanataka kumjambisha yule yesu wa mchongo, wanataka kumsulubisha kwa kadiri ya maandiko wakitarajia ufufuko wake siku ya tatu, je sisi tunasubiri nini? Hawa mitume na manabii wa mchongo inabidi wachezee vichapo.

Maandiko yako wazi, hakuna utukufu unaokuja bila mateso.Manabii na mitume walichezea vichapo wakapata utukufu huko kwa baba

Ieleweke, njia ya kwenda mbinguni ni nyembamba, manabii na mitume chukueni tahadhari.

[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Manabii gani wanakula kuku, wana mashavu yamenona, wana magari ya kifahari. Wanaishi kwenye makasri na ukwasi mwingi kuliko wafuasi wao?

Ukiwauliza maswali wanakujibu mbona ibrahim na suleimani walikuwa matajiri, hawa manabii na mitume wa mchongo wamekuwa wengi mpaka wengine wana vikosi vya ulinzi na usalama kama wa rais.

Eti mtu yuko madhabahuni kajiwekea mabodigadi kumzunguka pande zote, wengine wamevaa sare kama migambo.

Ni vituko vingi mpaka misafara ya magari wanaiga kama wa rais, kuna mijitu imevaa miwani nyeusi na suti huku imenyoa vipara.

Hawa manabii na mitume uchwara wangekuwa hata wanajenga hospitali, shule, maji na barabara wangeonekana wa maana japo wakijenga huduma kama za elimu na afya ni zao binafsi ili kujipatia kipato.

Kwa hiyo nao wakae tayari kusulubishwa kama mwenzao wa kenya
Utapeli mtupu. Si wanaona mkono wa Sheria hauwezi kuwafikia ndio maana Kila kukicha Kuna mtume na nabii mpya. Yaani matapeli wamepata a safe haven kwenye kichaka Cha dini/Imani. Hawaguswi na mtu wanatapeli wapendavyo!
 
Manabii na mitume tunaowasoma kwenye biblia walikuwa ni watu wa kuhangaika kutokana na kukataliwa na watu na watawala kutokana na ujumbe waliobeba kuwa kama ncha ya upanga kwa kukata na kupenya kunako. Mtume Paulo pamoja na kuwa mtume wa mataifa hatukuwahi kusikia alimiliki utajiri bali alihubiri injili kwa mahangaiko na mateso makubwa.

Lakini hawa kizazi hiki wanaishi maisha ya kifahari, kujenga mahekalu na mahoteli ya nyota kadhaa na kula bata bila kupata msukosuko wowote, tukisema ni wa mchongo tutakuwa tumekosea?
inabidi sasa tuwaletee shida ila maandiko yatimie, nabii hakubaliki kwao
 
Utapeli mtupu. Si wanaona mkono wa Sheria hauwezi kuwafikia ndio maana Kila kukicha Kuna mtume na nabii mpya. Yaani matapeli wamepata a safe haven kwenye kichaka Cha dini/Imani. Hawaguswi na mtu wanatapeli wapendavyo!
Wakinyooshwa akili zao zitakaa sawa
 
Tatizo watu mnajikuta wajuaji sana. Mtu anamkashifu mwenzake anae amini mitume na manabii wakati huo na yeye kuna mwanasiasa anamuamini na pia ni muumini wa chama fulani.

Wote nyie ni wale wale hamna tofauti. Brain washed!
 
Back
Top Bottom