Yetkin Gen Mehmen, Meneja wa Yapi Merkezi, kampuni inayojenga SGR ahukumiwa Kisutu

Yetkin Gen Mehmen, Meneja wa Yapi Merkezi, kampuni inayojenga SGR ahukumiwa Kisutu

Nyendo

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2017
Posts
1,336
Reaction score
4,731
1582812186565.png

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemuhukumu Meneja Uwezeshaji wa Kampuni ya Yapi Merkezi inayojenga reli ya kisasa (SGR), Yetkin Gen Mehmen kulipa faini ya Sh100 milioni au kwenda jela miaka mitatu huku ikitaifisha dola za Marekani 84, 850 alizoshindwa kuzitolea maelezo baada ya kukutwa nazo Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere(JNIA)

Mehmen ambaye ni raia wa Uturuki amehukumiwa na mahakama hiyo leo Alhamisi Februari, 27, 2020 baada ya kukiri kosa la kushindwa kutoa tamko ama maelezo ya fedha alizokutwa nazo dola za Marekani 84,850 katika Uwanja wa Ndege wa JNIA.

Akitoa hukumu hiyo Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba amesema kutokana na mshtakiwa huyo kukiri kosa lake mahakama hiyo imemtia hatiani.

"Mahakama inakuhumu kulipa faini ya Sh100 milioni au kwenda jela miaka mitatu pia fedha ulizokutwa nazo ambazo dola za Kimarekani 84,850 zinataifishwa na kuwa mali ya Serikali ya Tanzania," amesema Simba.

Awali Wakili wa Serikali Mkuu, Shadrack Kimaro alimsomea hati ya mashtaka mshtakiwa huyo kuwa Februari 13, 2020 eneo la Uwanja wa Ndege wa JNIA, alikamatwa akiwa na begi la mkononi ndani yake kukiwa na dola za Marekani 84,850.

Kimaro alidai baada ya mshtakiwa huyo kukamatwa na dola hizo maofisa wa polisi walipomuuliza alishindwa kuzitolea maelezo.

Hata hivyo, mshtakiwa huyo bado hajalipa kiasi hicho cha fedha ili aweze kuachiwa huru.
 
Bado haiingii akilini.. Mnafahamu kabisa ni manager wa kampuni kubwa mlioipa tenda ya SGR, sasa kuna ajabu gani kumkuta na hizo fedha? Na maelezo gani hasa mnayoyataka wakati mnafahamu fika ni manager wa kampuni wa kampuni kubwa na yenye tenda kubwa?

Huu ni udictator wa wazi kabisa..

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Kuna sheria zingine zakipumbavu sanaaaa, mtu hela yake afu bdo mnambania

House girl(dada wa kazi) Ni binadamu aheshimiwe, apumzike, apewe Uhuru wa kuabudu pia
 
Bado haiingii akilini.. Mnafahamu kabisa ni manager wa kampuni kubwa mlioipa tenda ya SGR, sasa kuna ajabu gani kumkuta na hizo fedha? Na maelezo gani hasa mnayoyataka wakati mnafahamu fika ni manager wa kampuni wa kampuni kubwa na yenye tenda kubwa?

Huu ni udictator wa wazi kabisa..

Sent from my iPhone using JamiiForums
Nimeona aibu kama ni mimi niliyeandika huu ''utumbo wa bata''
 
Kila kitu kina utaratibu
Bado haiingii akilini.. Mnafahamu kabisa ni manager wa kampuni kubwa mlioipa tenda ya SGR, sasa kuna ajabu gani kumkuta na hizo fedha? Na maelezo gani hasa mnayoyataka wakati mnafahamu fika ni manager wa kampuni wa kampuni kubwa na yenye tenda kubwa?

Huu ni udictator wa wazi kabisa..

Sent from my iPhone using JamiiForums

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama ni za tender kwa nini ashindwe kuzitolea maelezo!? Na kuhojiwa unapokua na fedha nyingi kupita kiasi hufanyika kila Airport! So ilikua simple tu kuzitolea maelezo.........

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bado haiingii akilini.. Mnafahamu kabisa ni manager wa kampuni kubwa mlioipa tenda ya SGR, sasa kuna ajabu gani kumkuta na hizo fedha? Na maelezo gani hasa mnayoyataka wakati mnafahamu fika ni manager wa kampuni wa kampuni kubwa na yenye tenda kubwa?

Huu ni udictator wa wazi kabisa..

Sent from my iPhone using JamiiForums
Mwishowe tutabaki tuu wenyewe kufanya kile kilicho ndani ya damu zetu mfano kufua majembe kwa kuchoma chuma mpaka kiyeyuko; kutengeneza ngoma nk. haya makubwa makubwa yanayohitaji utaalamu toka nje yatasubiri tuwe na huo uwezo.

Hata yule mchina wa rushwa ya US$ 5,000 naona tayari uwekezaji wake uko hatarini maana kwa kodi aya TZS 1.3 billion huenda akakimbia na kuitelekeza kampuni na watumishi wake
 
Mkuu siyo udikteta. Sheria iko wazi mwisho dola 10,000 kusafiri nayo zaidi ya hapo unadeclare. Je alidiclare?
 
Nyendo,
Pesa walizotaifisha zenyewe ni nyingi sana kuliko hizo wanazotaka alipe faini, naamini hakuna haki kabisa basi tu hizi zote ni hujuma, sas kama mtu ni manager wa kampuni inayojenga SGR pesa hizo kuwa nazo ni kitu gani kwani mbona fikra za kimaskini zinatutesa sana wabongoo ? hata kama ningekuwa mm wanikute na pesa ziwezi kuanza kutolea maelezo yeyote .
 
Nyendo,
Si vizuri kulaumu kila kitu kifanywacho na vyombo vya dola kwa ajili ya kulaumu tu. Hata Marekani au Uingereza kuna kiwango cha pesa taslimu ambacho unaruhusiwa kusafiri nacho. Kikizidi hapo lazima utoe maelezo ya kuridhisha kwa nini ubebe fedha taslimu kiasi hicho. La sivyo itachukuliwa ni kutakatisha fedha (money laundering).

Jiulize hivi ni kwa nini mtu usafiri na pesa taslimu kiasi hicho katika ulimwengu wa sasa ambao unahitaji kadi tu kununulia vitu au kulipia gharama za hoteli, n.k. Lazima kulikuwa na kitu cha kumfanya abebe fedha taslimu asizipitishe benki kukwepa kitu fulani. Kama nilivyosema hapo juu, hii ipo kila nchi. Si Tanzania tu.
 
Si vizuri kulaumu kila kitu kifanywacho na vyombo vya dola kwa ajili ya kulaumu tu. Hata Marekani au Uingereza kuna kiwango cha pesa taslimu ambacho unaruhusiwa kusafiri nacho. Kikizidi hapo lazima utoe maelezo ya kuridhisha kwa nini ubebe fedha taslimu kiasi hicho. La sivyo itachukuliwa ni kutakatisha fedha (money laundering). Jiulize hivi ni kwa nini mtu usafiri na pesa taslimu kiasi hicho katika ulimwengu wa sasa ambao unahitaji kadi tu kununulia vitu au kulipia gharama za hoteli, n.k. Lazima kulikuwa na kitu cha kumfanya abebe fedha taslimu asizipitishe benki kukwepa kitu fulani. Kama nilivyosema hapo juu, hii ipo kila nchi. Si Tanzania tu.
Mkuu Uturuki nayo inachangamoto za kiuchumi; huenda zikipita mfumo wa benki zingekwama
 
Bado haiingii akilini.. Mnafahamu kabisa ni manager wa kampuni kubwa mlioipa tenda ya SGR, sasa kuna ajabu gani kumkuta na hizo fedha? Na maelezo gani hasa mnayoyataka wakati mnafahamu fika ni manager wa kampuni wa kampuni kubwa na yenye tenda kubwa? Huu ni udictator wa wazi kabisa.. Sent from my iPhone using JamiiForums
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemuhukumu Meneja Uwezeshaji wa Kampuni ya Yapi Merkezi inayojenga reli ya kisasa (SGR), Yetkin Gen Mehmen kulipa faini ya Sh100 milioni au kwenda jela miaka mitatu huku ikitaifisha dola za Marekani 84, 850 alizoshindwa kuzitolea maelezo baada ya kukutwa nazo Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere(JNIA) Mehmen ambaye ni raia wa Uturuki amehukumiwa na mahakama hiyo leo Alhamisi Februari, 27, 2020 baada ya kukiri kosa la kushindwa kutoa tamko ama maelezo ya fedha alizokutwa nazo dola za Marekani 84,850 katika Uwanja wa Ndege wa JNIA. Akitoa hukumu hiyo Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba amesema kutokana na mshtakiwa huyo kukiri kosa lake mahakama hiyo imemtia hatiani. "Mahakama inakuhumu kulipa faini ya Sh100 milioni au kwenda jela miaka mitatu pia fedha ulizokutwa nazo ambazo dola za Kimarekani 84,850 zinataifishwa na kuwa mali ya Serikali ya Tanzania," amesema Simba. Awali Wakili wa Serikali Mkuu, Shadrack Kimaro alimsomea hati ya mashtaka mshtakiwa huyo kuwa Februari 13, 2020 eneo la Uwanja wa Ndege wa JNIA, alikamatwa akiwa na begi la mkononi ndani yake kukiwa na dola za Marekani 84,850. Kimaro alidai baada ya mshtakiwa huyo kukamatwa na dola hizo maofisa wa polisi walipomuuliza alishindwa kuzitolea maelezo. Hata hivyo, mshtakiwa huyo bado hajalipa kiasi hicho cha fedha ili aweze kuachiwa huru.
Bado haiingii akilini.. Mnafahamu kabisa ni manager wa kampuni kubwa mlioipa tenda ya SGR, sasa kuna ajabu gani kumkuta na hizo fedha? Na maelezo gani hasa mnayoyataka wakati mnafahamu fika ni manager wa kampuni wa kampuni kubwa na yenye tenda kubwa?

Huu ni udictator wa wazi kabisa..

Sent from my iPhone using JamiiForums
Mambo mengine kama huna ufahamu bora unyamaze. Hizo hela ni sawa na million 200 za kitanzania. Unawezaje kuwa na cash kubwa hiyo mkononi kama sio kwa ajiri ya uhalifu? Kisheria za kibenki za Tanzania ukitaka kutoa (withdraw) kiasi cha million 10 lazima BoT ifahamishwe na lazima hiyo account iwe inayoeleweka vinginevyo utasubirishwa saana uku wakikuchunguza.

Sasa RAIA wa kigeni kuwa na hela kubwa hiyo ya kigeni cash uwanja wa ndege ni uhalifu na unahatarisha usalama wa taifa. Nenda nchi yoyote duniani labla ya kuingia au kutoka lazima utolee maelezo kiasi cha fedha ulichonacho na uhalali vinginevyo zinataifishwa!
 
Mwishowe tutabaki tuu wenyewe kufanya kile kilicho ndani ya damu zetu mfano kufua majembe kwa kuchoma chuma mpaka kiyeyuko; kutengeneza ngoma nk. haya makubwa makubwa yanayohitaji utaalamu toka nje yatasubiri tuwe na huo uwezo.

Hata yule mchina wa rushwa ya US$ 5,000 naona tayari uwekezaji wake uko hatarini maana kwa kodi aya TZS 1.3 billion huenda akakimbia na kuitelekeza kampuni na watumishi wake
Acha kuongea usichokijua! Tembea nchi yoyote kabla ya kuingia au kutoka uhamiaji katika viwanja vya ndege lazima utolee maelezo kiasi cha fedha ulichonacho vinginevyo zinataifishwa kama ni kikubwa kuliko kiwango kinachoruhusiwa
 
Kipande cha zile trillion za SGR Manager mturuki naona kajikusanyia fungu lake
 
Bado haiingii akilini.. Mnafahamu kabisa ni manager wa kampuni kubwa mlioipa tenda ya SGR, sasa kuna ajabu gani kumkuta na hizo fedha? Na maelezo gani hasa mnayoyataka wakati mnafahamu fika ni manager wa kampuni wa kampuni kubwa na yenye tenda kubwa?

Huu ni udictator wa wazi kabisa..

Sent from my iPhone using JamiiForums
ndugu sheria iko hivyo duniani kote ukishindwa kuitolea maelezo then your liable
 
Back
Top Bottom