Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 48,475
- 70,102
Hii ni historia ya aina yake. Alizaliwa mwaka 1961 huko Leningrad leo hii ikiitwa St.Petersburg, miaka ya 1980 kabla hata hajafikisha miaka 20 akapewa hukumu ya kifungo cha miaka 2 na baadaye 13 jela kwa makosa ya ujambazi lakini akatumikia miaka 9 na kurudi uraiani.
Wakati anatoka jela miaka ya 1990 akakuta USSR inavunjika na wajasiriamali wajanja hii kwao ilikuwa fursa ya kunufaika kibiashara kutokana na hali mbovu kabisa ya utawala wa sheria iliyoambatana na mabadiliko ya uchumi kutoka mfumo wa kijamaa kwenda ubepari.
Alianza biashara yake ya kuuza soseji, kidogo kidogo akafungua mgahawa wake uliokuwa maarufu hasa kwa matajiri na tabaka tawala la St Petersburg. Mmoja wa wateja maarufu aliojenga nao urafiki wa kunufaishana sana baadaye akiwa Putin, kipindi hicho akiwa ni naibu meya tu wa St. Petersburg.
Baadaye Putin anakuja kuwa Rais wa Urusi na Prighozin anazidi kusogea karibu zaidi ya kiti cha enzi biashara yake maarufu ya chakula kwa jina la Concord ikipewa tenda nyingi za chakula au tafrija katika matukio makubwa ya serikali kama ugeni wa George Bush na tenda za jeshini. Hapo ndipo anapatia jina lake maarufu la mpishi wa Putin "Putin Chef".
Baadaye Putin anaona anaweza kumtumia bwana huyu kwa mambo zaidi ya chakula. Sehemu mojawapo ni katika uasi uliaosisiwa na Urusi huko Donetsk na Luhansk nchini Ukraine mwaka 2014. Prighozin anatumika kupitia Wagner kama mwanzilishi wake ambayo inatumika kama "front" huko Ukraine na sehemu nyingine nyingi za dunia ambapo serikali ya Urusi isingependa ushiriki au mkono wake uonekane moja kwa moja ili kutunza heshima na taswira yake kama taifa lililostaarabika la kisasa lisilojihusisha na ukatili au mambo mengine ya hovyo.
Haiishi hapo tu, Serikali ya Marekani inamtuhumu kutumika kuanzisha kampuni ya kufanya vurugu za mitandaoni katika harakati za Urusi kuvuruga na ku influence uchaguzi mkuu wa urais wa mwaka 2016 uliompa ushindi Trump.
Wakati Urusi inaivamia Ukraine kwa mara nyingine mwaka 2022 Wagner tayari imezidi kuwa kubwa na kushamiri, wanapewa kandarasi ya kupigana sambamba na jeshi la Urusi hadi na kibali maalumu cha kutumia wafungwa. Vita inapozidi kukolea Prighozin hafurahishwi na utendaji pamoja ni mikakati ya Waziri wa Ulinzi na Mkuu wa majeshi, Shoigu na Gerasimov. Analalamika kwa muda mrefu lakini ni kama Swahiba wake wa muda mrefu ameziba masikio au yuko usingizini katika hilo, anaamua kuwasilisha malalamiko yake kwa nguvu zaidi, kwa uasi kuelekea Moscow.
Akiwa njiani anapigiwa simu nyingi za maonyo ya kila aina, ahadi na kusihiwa, anapatwa na wenge anasitisha safari yake na kukubali kuhama kabisa nchi aliyoishi miaka yote na kuhamia kwa jirani. Hata hivyo huenda huu bado sio ukurasa wa mwisho kwa mpambanaji huyu.