Elections 2010 Yeye hazitaki, Mimi naziomba

Mlachake

JF-Expert Member
Joined
Oct 13, 2009
Posts
4,437
Reaction score
4,618
Muda mfupi nimetoka kwenye mkutano wa Dr. peter W. Slaa hapa Iringa. Kaongea mengi sana. Lililonigusa ni sana ni hilo neno '' yeye kasema hataki kura zenu, mimi nazitaka'' Sijui nyinyi mnasemaje?
 
nadhani kula za wafanyakazi, kweli hatumpi JK kura zetu, mwenyewe anajua
 
Asiyezitaka hatumpi, aombaye atapewa.
 
Mifanyakazi Tanzania na familia zao, mingi KIGEUGEU. Nitakuwa Thomas hadi nione matokeo.

UKO NA MAFISADI AU UKO NA DR.SLAA
 
 
Hivi kuna mfanyakazi mwenye akili timamu ambaye atampa jk (kifa ulongo) kura yake? Itakuwa maajabu ya dunia
 
 
Unajua mie Hesabu ilinipiga chenga wafanyakazi laki 3. Tuchukulie mfanyakazi 1 anategemewa na watu wangapi chini yake sasa wote wakiungana ili kuwa kitu kimoja na mfanuyakazi 1 jumla watakuwa wangapi?? kwa hiyo JK hatokosa kura LAKI atakosa KURA ZAIDI ya HIZO laki 3
 

Kwa extended family za kitanzania sitashangaa kuna kila mmoja anabeba kwa hesabu ya chini sana watu watano, impact itakuwa kubwa sana
 

Haya ndio mahesabu ya Dr. Slaa.
1. Wafanyakazi 350,000 kila mmoja anaweza kuwa na mume au mke. Tayari kura zimeshafika 700.000
2. hawa wapiga kura 700,000 yaani mke na mume,ana familia ya upande wake. yaani kwa upande wa mke kuna familia na kwa upande wa Mume kuna familia.
Kwa mahesabu ya haraka haraka tumeona Chain ya wafanyakazi inaweza kufika over 5,000,000.
kama Kwa wafanyakazi peke yake inaweza tokea Chain kubwa hivi, kwanini asishinde?
 
Mifanyakazi Tanzania na familia zao, mingi KIGEUGEU. Nitakuwa Thomas hadi nione matokeo.

UKO NA MAFISADI AU UKO NA DR.SLAA

kaka utashangaa siku ya Mwisho. Hakuna watu wanafiki kama hawa jamaa wa kijani. Nimekua karibu sana na wazee mbali mbali tena Campaign team ya wabunge wa sisiemu kwenye kura ya maoni, na wavaa fulana No.1. na wameapa hawawezi kumpa JK kura Yao. Siongei ushabiki. Naongea Fact kaka. amin amin nawaambieni lazima Dr. Slaa atashinda. Nyie msio amini, Just mark my words. October 31 sio Mbali. Mtakuja kuuona ukweli. wanachadema msiwe na wasi wasi. wala msitetereke. we are on our way to the white house. Huyu ndiye Kiongozi tuliyechaguliwa na Mungu. Siamini kama Tanzania tumelaaniwa. Mungu atatupa kinachostahili awamu hii. Mungu ibariki Tanzania. Mungu mmabariki Rais wetu ajaye Dr. Peter Wilbroad Slaa
 
Walimu wa shule za msingi wamekuwa wakiisaidia sana CCM kuiba kura kwani wao ndio huwa wasimamizi wa vituo vya kupigia kura. Nimefarijika sana kwenye mkutano mmoja baadhi ya walimu walipotamka bila woga kuwa Slaa ni rais wa wafanyakazi!
 
Ni maombi yetu Wafanyakazi muwe chachu ya mabadiliko hapa nchini. Historia inaonyesha mabadiliko mengi ya kisiasa na kuondoa ukandamizaji huongozwa na Wafanyakazi. Mungu awasaidie mulione hili. Maneno ya kejeli aliyoyasema Kikwete juu yenu yaendelea kusikika masikioni mwenu mpaka saa ya kupiga kura..Amen!
 
Hivi kuna mfanyakazi mwenye akili timamu ambaye atampa jk (kifa ulongo) kura yake? Itakuwa maajabu ya dunia
Kuna wabongo wabishi ndugu yangu, wanaona kama wanapata dhambi kuinyima kura CCM.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…