Yeyote anaeuza tikiti zikiwa shamba tuwasiliane, nnanunua tikiti kuanzia 500

Tafakuru

Member
Joined
Dec 9, 2011
Posts
83
Reaction score
33
helow
Wadau mm ni mfanyabiashara wa kati, nnaenunua tikiti maji na ku_supply jijini Dar-es-salaam. Kwa yeyote anaefanya kilimo hiki, tuwasiliane tujenge uchumi wetu. Biashara hii inafaida kubwa ila pia inahitaji kuzingatia kanuni za kilimo chake

*IYO 500 NI IDADI NA SI BEI, BEI ZIPO ZINAJULIKANA NA PIA NI MAELEWANO, no hujuma
*I pay in cash
 
mimi nalima tikiti morogoro ila kwa bei ya mia tano kwa tikiti wakati dar linauzwa elfu 3 huu ni ufisadi kumbe wakina EL mko wengi
 
mimi nalima tikiti morogoro ila kwa bei ya mia tano kwa tikiti wakati dar linauzwa elfu 3 huu ni ufisadi kumbe wakina EL mko wengi

mkuu .... taratibu bana .... mleta thread anamaanisha ananua idadi ya tikiti kuanzia miatano na siyo sh. 500

mleta mada correct me
 
Wewe ni muhujumu uchumi adhabu yako ni kifungo,lima wewe tuje kununua kwa mia 5,ningekua na shamba la tikiti hata 2000 sikuuzii.
 
vi heka moja inaweza kutoa tikiti ngapi na vipi gharama za kilimo- sorry out of topic
 
sorry wadau,moro ni maeneo gani yanafaa kwa kilimo cha matikiti maji,nataka nianze fasta nimuuzie jamaa kuanzia mwez wa 6
 
inaeza kutoa tikiti adi 1500 kama yakizaa yote na kutegemea upandaji na uzaaji ila 1500 is maximum...gharama mara nyingi ni laki kama tatu na nusu

Kaka, hiyo maximum umetoa wapi? Hakuna maximum output kwenye kilimo. Inategemea na upandaji na utaalamu wako katika kilimo.

Katika ekari moja unaweza pata matunda 5000, hata na zaidi. Ni upandaji wako na ukubwa wa namna gani wa matunda unataka pamoja na jinsi unavyohudumia shamba ndio itategemea kiasi utakachopata.

Hata ukitaka matunda 9000 unaweza pata. Ila kadiri mche unavyoelemewa na matunda mengi, na ukubwa pia hupungua.
 
Mnunuzi wa matikiti maji nitafute mwakani.

Inshallah
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…