monotheist
JF-Expert Member
- Apr 30, 2017
- 830
- 1,449
Kuku wanapatikana kwa Wingi mikoa ya singida na tabora ila nakushauri singidaHabari za siku,
Ningependa kupata ufafanuzi juu ya biashara ya kununua kuku mkoani na kuuza mjini (Dar ea salaam) Ningependa kufahamu yafuatayo;
1)Bei ya kila kuku mmoja ni Tsh ngapi huko vijijini?
2)Mkoa (kijiji) gani ambapo kuku hupatika kwa wingi na wenye maumbo makubwa?
3)Usafiri wa aina gani ni rafiki kwa kuku (Bus au Roli)?
4)Eneo gani hapa Dar naweza kupata soko la uhakika kwa bei ya jumla au rejareja?
5)Changamoto ya biashara hii ( faida na hasara)
Ahsante mkuu, Je uwezejano wa kupata banda (eneo la kuuzia) hapo shekilango upoje?Kuku wanapatikana kwa Wingi mikoa ya singida na tabora ila nakushauri singida
Unaingia chimbo kidogo maeneo Kama itigi, itagata, mitundu, paka mbele huko rungwa
Huko unapata kuku kwa bei poa kabisa kuanzia elfu 6 paka elfu 10 Kutegemea na eneo husika pia convincing power
Unawasafirisha kwa malori paka mjini daslam nauli inategemea na maelewano wanafanya kwa tenga unaweza kuomba tu MI nakupa kiasi kadhaa maybe elfu 50 au unalia nae we paka aelewe
Ukifika dar sasa Unaweza kuuza kwa jumla au rejareja nenda buguruni pale Uliza bei ila kipindi hiyo ilikua elfu 14 au 13 au 12 Kutegemea na Aina ya dalali
Au pia nenda pale shekilango kuna soko liko poa kabisa ulizia bei
Kwa rejareja ndio kuna faida ila unatakiwa uwe na sehemu ya kuuzia au Fanya delivery
Thanks
Hapo ungeenda tu ukapata utaratibu mzima ili ujionee mwenyeweAhsante mkuu, Je uwezejano wa kupata banda (eneo la kuuzia) hapo shekilango upoje?
Pamoja mkuuChangamoto kubwa Ni upatikanaji wa kuku hasa vijijini unatakiwa usiwe na haraka mana kuku wanafugwa kiholela so unazunguka Leo unaweza kupata mmoja kesho ukapata ishirini so inatakiwa ukusanye pia eneo la kukusanyia hapa mwenyeji unatakiwa kumpanga fresh mbaya watu WA singida wakiona umekuja na Dili basi wanajua na wao watatokea hapo hapo kwaio usipokua makini basi utahudumia familia
Garama za maisha kwa ujumla na connection mana Hakuna mtu atakuuzia kuku bila kuwa nawenyeji so tafuta mwenyeji
Kingine usafiri madereva baadhi huwa wandhani ndio Wanatakiwa kupata posho yao kupitia mzigo wako
Madalali wa mjini Kama unataka kuuza kwa jumla Hawa wapuuzi Sana wanaweza kukwambia kuku sisi tunauza elfu 9 wakati ww gharama zako zimezidi lengo ni kukupoteza ila wenyewe wanapiga faida ya hatari mana kwa rejareja kuku ni kuanzia 20 na kuendelea
Angalizo Fanya research ya soko mapema kabla haujaingia chimbo ikibidi wapange kabisa wanunuzi na madalali