YOM HAKIPPUR: Wanachokifanya WACHAGA DECEMBER ni Sawa na walichofanya WAISRAEL siku ya kumi ya mwezi KISLEU

YOM HAKIPPUR: Wanachokifanya WACHAGA DECEMBER ni Sawa na walichofanya WAISRAEL siku ya kumi ya mwezi KISLEU

mitale na midimu

JF-Expert Member
Joined
Aug 26, 2015
Posts
10,420
Reaction score
17,735
Mwenyezi Mungu aliwaelekeza mara moja kwa mwaka Waisrael wakutane katika mkutaniko na familia zao kupatana nae.

Hii ilikuwa ni Siku ya kusameheana.
Ilikuwa ni Siku ya kuanza upya na Mungu wao.
Wayahudi walisafiri popote walipokuwa duniani na kurudi kwao kwa ajili ya tukio hilo.
Siku hiyo iliambatana na ibada na kafara.

MATOKEO
Familia na taifa lilikuwa imara kuliko kabla.
Waliokuwa wamerudi nyuma na kusahau asili yao walirejezwa.
Waliokuwa wazembe waliweka maagano ya kuanza upya kwa nguvu.
Waliopoteza ndugu zao siku nyingi walitiwa motisha walipopokea habari za maendeleo na mafanikio yao.

WACHAGA ndio kabila pekee kwa Afrika mashariki kama sio afrika lenye huu utamaduni. Kinaweza kuonakena ni kidogo lakini impact yake naamini ndio imelififanya kabila hili kuwa imara Afrika licha ya udogo wa eneo lilnalotokea.

Naamini babu wa mababu wa Kichaga aliiga Ritual hii kutoka kwa waisrael. Ikumbukwe Imetabiriwa Katika Biblia (Isaya )mkoa huu wa kilimanjaro wenye mlima mrefu utatoa watu hodari.


Familia na makabila huu utamaduni ni mwema sana, LAzima familia zikae zijitafakari na Mungu wao, wanakosea wapi na warekebishe wapi.

Taadhari tukio hili ili lilete matokeo yatakayokufanya usimame imara mbele za Mungu siku ya kiyama, Usielekeze ibada kwa wazee, na miti, sanamu na kafara. Ambatanisha Sherehe za tukio hili na ibada kwa Mungu ambaye zamani tulidhani ni Miti ila siku hizi tumeelewa ni yule tunayefundishwa kwenye vitabu vitakatifu.

ni hayo tu.

Muebrania
Mitale na Midimu.
 
Kwanza nikukumbushe kwamba sio wachaga hata wasukuma wanayo sema wao kila koo ina mwezi wake kila mwaka na huitwa fogon'go

Makabila mengine nayo watasema.
 
Kwanza nikukumbushe kwamba sio wachaga hata wasukuma wanayo sema wao kila koo ina mwezi wake kila mwaka na huitwa fogon'go

Makabila mengine nayo watasema.
Wasukuma WA wapi hao ndugu, msukuma akishatoka kwao katika kutudi ni majaliwa ndo mana hawatengenezi mazingira ya kurejea,na kama wangekua wanarejea ungeona pressure kwenye vyombo vya usafiri.

Hui utamaduni upo kwenye jamii nyingine kama wachina WA mwezi wao pia na wamarekani Wana siku Yao wanaitaa thanksgiving, niutamaduni mzuri kwa kweli kurudi nyumbani ni kama kwenda kurecharge na kuchota Baraka mpya. Wazazi wetu wakifirahi milango ya Baraka inafunguka tuu.
 
Kwanza nikukumbushe kwamba sio wachaga hata wasukuma wanayo sema wao kila koo ina mwezi wake kila mwaka na huitwa fogon'go

Makabila mengine nayo watasema.
fogon'go sijawahi kuisikia mkuu.

unaweza kuielezea kidogo. Itakuwa imefifia maana kwa ninavyojua wasukuma walivyotapakaa hadi kusini mwa afrika, nchi ingekuwa inasimama siku yao ya fogon'go
 
Kujilinganisha na waisrael ni dharau. Sio sifa nzuri ata kidogo. Waisrael ni wabaguzi wa rangi, wauaji, walimuu mpaka Masiha, yani ni kujidharau.
 
Back
Top Bottom