SoC02 Yombo na uhalifu

SoC02 Yombo na uhalifu

Stories of Change - 2022 Competition
Joined
Aug 11, 2022
Posts
16
Reaction score
10
Mambo yamekuwa tofauti sana yombo imekuwa na makundi maarufu sana ya kiharifu ambayo dar es salaam nzima yanajulikana mfano mkubwa panya road ambalo kundi hili linaundwa na vijana ambao asilimia kubwa walipaswa kuwa shule na limekuwa likifanya matendo ya kiharifu hadharani kabisa kundi hili asili yake ni yombo buza lakini pia kuna kundi la pili ni mbwa mwitu nalo nikundi linaloundwa na vijana wadogo kabisa ambao wengi wao ni wa shule ya msingi.

Swali kwanini makundi haya yanajulikana na bado yanaendelea kuwepo na kufanya uharifu ? Je ni kweli yameshindwa kudhibitiwa kabisa? Naomba tuanze na swali la kwanza kundi hili jina limeshakuwa kubwa na kuogopewa na raia ivyo waharifu wamekuwa wakilitumia jina hilo kufanya uharifu wa alaiki nakufanya kuonekana kundi limeshindwa kudhibitiwa .

Swali la pili kundi limedhibitiwa ila waarifu wakuwa ni wengi mno hii ni kutokana na idadi kubwa ya wanafunzi wa sekondari na msingi kushinda chimbo ambako ndio wanakojifunza hata matumizi ya madawa ya kulevya na uvutaji wa bangi hii upelekea wanafunzi kuanza kufanya uharifu mashuleni na hata nje ya shule mfano shule ya sekondari lumo kwa mwaka wa masomo 2020,2021 na 2022 imefukuza wanafunzi kwa makosa ya uwizi shuleni na nyumbani ,uvutaji wa bangi ,uhasherati na ushoga . lakini jambo lakujiuliza ni kwamba uko mtaani wanaenda kufanya nini?

Na hiyo tabia wanajifunzia wapi,,majibu ni kwamba hao ndio baadhi yao wajiunga na makundi ya kiharifu kama panya road na mbwa mwitu lakini hii tabia wengi wanajifunza kutokana na mazingira mabovu ya shule mfano shule kukosa fensi ambayo urahisha wanafunzi kutoroka kirahisi kwa sababu mbalimbali ikiwemo kukwepa adhabu nk.

Pili tabia hii wanajifunza kutokana na mazingira mabovu majumbani mwao ambapo unakutamwanafunzi hukosa uangalifu wa wazazi au walezi wake ivyo kijiongoza mwenyewe au na makundi rika ,,,je nini tufanye ili kupunguza haya makundi ambayo kwa kiasi kikubwa yamekuwa yakiundwa na watoto wa shule.

Kwanza shule zijengewe fens (wigo) hii itasaidia kudhibiti utoro wa rejareja kwa wanafunzi ambao wanaenda chimbo na kufanya mwanafunzi kutoka nje akiwa na kibari maalum kama gatepass.

Pili kuwekwa kwa mfumo ambao utamuwezesha mwanafunzi ambayo anashindwa kuendana na mfumo rasmi wa elimu kupelekwa kwenye elimu ya ufundi mfano kwa mfano mtoto wa akifeli kidato cha pili ni bora aende veta ili miaka miwili iliyobaki asomee ujuzi ambao utamsaidia maishani mwake
Tatu wazazi au walezi wengi hasa wa temeke jukumu la ulezi wa watoto wameliacha kwa mwalimu hivyo wao hawahusiki na malezi ya watoto wao na kuwa bize na kutafuta maisha ivyo wazazi wanapaswa kushiriki ipasavyo kwa kutembelea shule na kujua maendeleo ya wanao ila wazazi wengi wanaona kama usumbufu kuja shule kufuatilia maendeleo ya wazazi
 
Upvote 0
Back
Top Bottom