Nafikiri umaarufu wote wa Yondo ulikuwa ni kufanya show ila kama mwana muziki, mhh. Siku zote nyuma yake walikuwa wamesimama imara Wazee/Vijana wa Soukous Stars yaani Lokasa ya Mbongo, Dally Kimoko na Shimita El Diego ambaye kwa sasa naona kaanzisha bendi yake. Kwenye wimbo wa Bazo unasikia kabisa sauti ya Shimita iki-Rap. Hawa jamaa unaweza waona wote hapa na kwenye dakika ya 4 jamaa anaimba kwa Kiswahili. Na mwisho kwenye 7:14 jamaa wa west Africa kama sikosei Mali anakuja na hapo wanaanza kucheza Zugulu (sikumbuki wanaandikaje kifaransa).
Hapa Chini Yondo Sister kama mchezaji kwenye wimbo wa Lokasa ya Mbongo uitwao MARIE JOSE. Ninafikiri hata ni yeye aliimba kwenye background vocal ya huu wimbo.
Lazima nikubali kitu kimoja kuwa mziki wa Soukous hawa jamaa walikuwa wametawala kabisa. Chezaji ya Shimita hadi leo watu wanacheza. Mziki wao hadi kesho vijana wadogo wataiga ili wapate pa kutokea. Mwanzo nilikuwa nasikia Shimita anacheza ila nilikuwa sifahamu hadi nilipokuja kuona hii Video.
Ila nirudie tena, pamoja na mziki wao MZITO, unapokuja kwenye show, basi Yondo Sister alikuwa anafunika. Dada yake (na yeye Half cast) alikuwa akicheza kwenye kundi la Pepe Kalle and Empire Bakuba (nasikia walikuwa ndugu) sijui aliishia wapi?
Kusema kweli mie huyu dada alikuja enzi hizo nimeipenda bendi ya KASSAV na hasa huyu dada Jocelyne Beroad (aliyeimba Coupe Bibamba na Awilo). Huyu mama kwa kweli aliniuwa na hadi leo hii Kassav kwangu wako juu sana. Najuta sintakuja kuwaona LIVE. Anyway itabidi hata kufurahia video zao za LIVE.