Ufaransa, wiki tatu nyuma, Zuberi Msabaha wa Radio Free Africa aliongea nae saa4 usiku kwenye kipindi cha Bolingo Time. Kusala(Yondo Sister) alieleza kuwa anaishi Ufaransa, mambo ya watoto na ndoa alikataa akidai kuwa hapendi kudisclose mambo yake ya kifamilia. Kihistoria anasema babu yake ni Mbelgiji kabisa hivyo ni yeye ni halfcast. Alipoulizwa wanamuziki wenzie wa iliyokuwa Soukouss Stars wako wapi na wanafanya nini, nilishangaa aliposema: Balou Canta, Ngouma Lokito, Dally Kimoko, Shimita na wengine bado wako France na wanapiga music na akijibu kuwa mashabiki wa Africa Mashariki, akipatikana mdhamini wako tayari kuja. Alipoulizwa kwa nini anazungumza Kiswahili fasaha alidai KIDOGO TU. Kwa hiyo yupo hai. Ukitaka kumwona mtoto wake Yondo, utamwona kwenye album yake Yondo( Siyo na Soukouss Stars). Album hii ina nyimbo kama: Madi, Africa, Derniere Minute n.k. Huyo binti kafanana nae sana Yondo Sister kwa wakati huo alikuwa ni mnenguaji. Nenda You Tube halafu search: Yondo Sister- MADI, ni wimbo ambao utagundua Dally Kimoko ni mchawi wa Guitar/gitaa.